Kwa Wajuzi wa Mambo ya Bahari, Naomba Kufahamu Hili! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Wajuzi wa Mambo ya Bahari, Naomba Kufahamu Hili!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwendabure, Sep 18, 2011.

 1. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,051
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Habari Wakuu!
  Ni hivi karibuni serekali yetu imekiri kwamba wazamiaji wa kukodi kutoka Afrika Kusini wameshindwa kuifikia Meli iliyozama baharini na kusababisha vifo vya ndg zetu huko Zanzibar. Mimi binafsi kwa uelewa wangu mdogo kuhusu masuala ya bahari ningependa kueleweshwa vema haya yafuatayo.
  1. Ni umbali (kina) gani unaweza kufikika kiurahisi na kwa kutumia vifaa gani?
  2. Kuna tofauti gani ya hali ya bahari kati ya kina kidogo na kina kirefu?
  3. Nimekuwa mara nyingi nikiona ktk sinema au hata baadhi ya vipindi vya TV wazamiaji au watafiti na wapiga picha za bahari wakifika hadi ktk sakafu ya bahari kwa kutumia vifaa kama vile mitungi ya gesi huwa wanaweza kufikia kina gani cha bahari kwa vifaa kama hivyo?
  Natumaini nimeeleweka vema na nitapata majibu murua kwa faida yangu na wengine pia. Binafsi naamini hadi sasa serikali yetu haina mpango wa kutoa elimu au ufafanuzi wa kutosha hasa kwa Mtanzania wa kiwango cha uelewa kama wangu kuhusu kinachoendelea juu ya sakata hili na hatma ya miili ya wapendwa wetu waliopotelea baharini.
  Nawasilisha!
   
 2. Kijuche

  Kijuche JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ngoja tusubiri wataalamu waje wajibu.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,258
  Likes Received: 21,970
  Trophy Points: 280
  wataalam wa South Africa wamefeli, je wa JF wataweza?
   
 4. analysti

  analysti JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 704
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 80
  What is the essence of this question?
   
 5. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,046
  Likes Received: 7,257
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha ha!!!!
  Umenichekesha sana mkuu wangu.
  But wale nahisi walikua watalii tu.
  Otherwise pengine walifika mpaka chini but waliyoyaona bora wakae kimya tu!!
   
 6. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,356
  Trophy Points: 280
  Kiukweli, kina kirefu sana cha bahari matatizo yake huwa ni giza na kiasi kidogo cha hewa ya oxygen. Kama vifaa wanavyo, haina haja ya usumbufu.. Kile kina sio kirefu saaaana kivile, hakiwezi kusumbua kama kuna vifaa. Tatizo lingekuwepo kwenye kuitoa hiyo meli. Kwa kuwa kadiri sikuzinavyozidi kwenda, ndivyo inazidi kuwa ngumu kuitoa kwa kuwa inakuwa inaingia ndani ya oceanic floor kama hiyo oceanic floor ipo kama mchanga mchanga. Pia inazidi kuaribika kwa sababu ya maji ya chumvi. Inaonekana hao wa south afrika, walikuwa ni wanafunzi tu. Hawana ujuzi na vifaa vya kutosha. Ishu ni vifaa.
   
 7. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Waokoaji wa South Africa walijaribu walivyoweza kwa kutumia vifaa vyao vya kitaalamu vya kuzamia. Kutokana na hali halisi ya kina kirefu na hali mbaya ya hewa ukitilia maanani ule ni mkondo mkali sana walishindwa kuifikia meli. Na kama ndivyo basi tayari wote walionaswa ndani ya meli walikuwa wameshakufa maji. Ama kwa majibu ya maswali uliouliza ni kwamba:-
  1. Kwa kutumia chupa za hewa unaweza kucheza kati ya mita 20 hadi 35 kwa mjuzi. Kila chupa moja hewa humalizika kati ya dakika 30 hadi 45 kulingana na mtumiaji.
  2. Tofauti ya kina kidogo na kirefu ni kuwa kila unapozidi kwenda chini hewa inaisha kwa maana ya kwamba kunakuwa na compression kali sana na kupona ni miujiza ya Mungu.
  3. Zile movie unazoziona za madivers na samaki sio za kina kirefu zaidi hazipitishi mita 20.
  Natumai nimetoa majibu
  kwa ufupi ila ndio hali halisi na wengine watachangia.
   
 8. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa hali ya kawaida binadamu anaweza kwenda chini ya bahari si zaidi ya mita 50 ingawa kuna ambao wanaweza kwenda hadi mita 60 -80 kwa kutumia Self-Contained Underwater breathing apparatus (SCUBA) yaani ni ile mitungi ya gesi na vifaa vingine vitakavyomfanya apumue chini ya bahari. Kadri unavyoenda chini ya bahari hewa ya oksijeni inapungua na mkandamizo (pressure) inaongezeka na ndio maana hata wakati wa diving ushauriwi kwenda haraka haraka, unahitaji kwenda step by step.

  Wale unaowaona kwenye sakafu ya bahari wanakuwa eneo ambalo haliwezi zidi mita 50 na mara nyingi ni kwenye corals (matumbawe) ambayo yanakuwa kwenye maji ya pwani na ndio maana unayaona yale maji ni meupe maana yapo kwenye kina kifupi (sometimes less than 30 meters) ambapo mwanga wa jua unafikia yale matumbawe na hewa (oksijeni) inakuwepo ya kutosha.

  Ilipozama ile meli ni kwenye mkondo (yaani kunakuwa na surface water na wakati huo huo chini yake kunakuwa na kama mto wa maji yaendayo kasi) na kina chake mara nyingi ni kirefu kutegemea na ukubwa wa mkondo na kwa pale Nungwi wamekadiria karibu mita 300. Hivyo kwenye kina hicho maji ni meusi (huwezi ona chochote), ya baridi sana, pressure ni kubwa na hakuna hewa ya oksijeni. Hivyo kwa kutumia SCUBA hakuna mtu atakayeweza kwenda kwani utapasua kila kitu kutokana na mgandamizo (pressure) na huwezi ona chochote. Unaweza kufika pale labda kwa zile mashine maalum kama robot ambazo pia mtu inabidi afungiwe ndani yake (haruhusiwi kutoka ndani ya hicho kijichumba) kwa hiyo kwa hali hiyo huwezi fanya chochote maana unakuwa confined.
   
 9. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,051
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Nakushukuru Mkuu Limbani kwa maelezo yako yenye ujazo wa haja ya kiu yangu. Asante sana nimefaidika na kufarijika pia... Senkyu sana!
   
 10. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,051
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Asante Mkuu Timtim kwa majibu sambamba na maelezo ya kutosha na ya kitaalam si haba. Kwa hakika naiona raha ya JF pasi na shaka. Ubarikiwe inshaalah!
   
 11. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,356
  Trophy Points: 280
  Lakini ningependa kujua kile kina kina mita ngapi? Maana south afrika wana rekodi ya kufikia 927 feet (283 m) na
  826 feet (252 m) mwaka 1994! Source www.wikipedia.org/w/index.php?title=Deep_diving
   
 12. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Pale wamakadiria kuwa na kina karibu mita 300, na sio kama hakufikiki. Kunaweza fikika lakini ni kwa kutumia Nyambizi (submarine) ambayo itachukua muda na hivyo kwa uokozi ni kama vile haina maana. Maana mtu mpaka afikie chini kina hicho (wale walioko kwenye meli) ni alishakufa muda mwingi tu. Ndio maana jamaa wakasema labda ije Nyambizi kwa ajili ya kuitoa tu ile meli baadae lakini kwa uokozi haina maana yeyote.
   
 13. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  SIDE B: kila pahala penye mkondo wa bahari huwa na maji yenye virutubisho vingi hivo huwa na biodiverisity kubwa ukilinganisha na maeneo ya bahari ya kawaida. Mkondo bahari wa nungwi unasamaki wengi na waina mbalimbali ambao hawapatikani ktk maeneo mengine duniani: NEED TO FEED THEM FOR SUSTAINABILITY...................................
   
 14. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,356
  Trophy Points: 280
  asante kwa kunipa hiyo data. Ni kweli kazi ya uokoaji hapo haiwezekani tena. Labda kutoa hiyo meli tu.
   
 15. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Serikal si inachama cha waganga kwanin yanapotokea majanga kama haya ya baharin wasiwape tenda yakupasua maji kwa mayai viza.wanaunda tume tume tume wanapeana posho wakati mamia washapoteza maisha
   
 16. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #16
  Sep 19, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,111
  Likes Received: 3,031
  Trophy Points: 280
  oohhh......
   
 17. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #17
  Sep 19, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Preta, jiwe limekupata usoni au mgongoni?, khabari ndo hiyo.......
  <br />
  <br />
   
 18. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #18
  Sep 19, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,574
  Likes Received: 840
  Trophy Points: 280
  slow down
   
 19. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #19
  Sep 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Serikali imeopgopa aibu.......walokufa wanafika 2,000.....ingekuwa disaster kubwa......wale jamaa huzama vina virefu sana
   
Loading...