Kutokana na hali ya usalama kuzidi kutikisika siku hadi siku.,ni vyema tukauangalia upya mfumo wetu wa kiutawala nchini.
Ni wazi Mfumo wa nyumba kumi ni lazima uingizwe kwenye sheria za nchi,kwamba ngazi ya chini kabisa ya kiserikali sasa ianzie na nyumba kumi baadala ya ngazi hiyo kuanzia kitongoji.
Kitongoji ni kikubwa sana,ni eneo la kiutawala lenye kaya karibu 250.,Hivyo kutokana na uduni wa teknolojia kwa nchi yetu.,ni rahisi kuthibiti mambo ya maendeleo na usalama kwa kaya kumi( nyumba kumi).
Mfumo huu ulitumika kipindi cha chama kushika hatamu,mfumo huu umebaki mikononi mwa chama cha Mapinduzi kwa lengo la kisiasa,tofauti na kipindi cha chama kimoja ambapo lengo lilikuwa masuala ya kiusalama na kisiasa.
Ninajua vyama vyote vya siasa,vinaupenda mfumo huu kwa maslahi ya kisiasa.
Kutokana na unyeti wa eneo la ulinzi na usalama wa nchi yetu na kutokana na hatari kubwa ya kutoweka kwa amani nchini.
Naomba bunge la katiba litambue nyumba kumi kuwa ngazi ya kwanza ya serikali.
Ni rahisi kiongozi wa nyumba kumi kuzijua nyumba zake kumi,kupashana habari ndan ya nyumba kumi.,kuhamasisha maendeleo kwa nyumba kumi.,lakini kubaini biashara za madawa ya kulevya,ugeni wa mtu atiliwaye shaka nk.
Sitegemei matusi,tulijadili kwa afya ya nchi yetu.