sio maana hiyo, vibamia na vyote hivyo, vyote ukipata matatizo umepata. central point hapa ni kwamba, ukioa au kuolewa kufuata ngono, utadondokea pua. ndoa sio ngono tu kuna maisha mengine mengi zaidi ya ngono. kama ndoa ingekuwa ngono peke yake, watu wasingeishi kama unavyofikiri. asilimia 50 ya wanandoa wote huanza vizuri, lakini nusu inayobaki hupata matatizo njiani na mtu ataishi na tatizo hilo hadi anakufa, hivyo kama wewe ni mume au mke wake, itabidi ulihudumie hilo tatizo hadi mzeeke mfe. ndoa ni upendo, ndoa ni kusaidiana, ndoa ni kutafuta watoto pamoja, ndoa ni kusomesha watoto, ndoa ni kujenga nyumba, ndoa ni kutafuta utajiri, ndoa ni kufarijiana, ndoa ni kupangusana mimmavi ukiugua hata kidole hakinyanyuki mwenzio akupeleke choooni akutawaze huko nyuma kwako huko, ndoa ni kushika matapishi ya mwenzako kwa upendo pindi anapoumwa hajiwezi kabisa, ni kupambana pamoja. ni kuwa umemtafuta na kumpata companion wa maisha mtakayesaidiana kupambana na maisha ya hapa duniani. ngono ni kitu kidogo sana, ndio maana kuna wana ndoa wanalala pamoja lakini muda wa kufanya ngono wiki nzima hawajapata....ni kwasababu vichwa vimechoka, stresss, matatizo lukiki hata hamu ya tendo haipo, na kinachohitajika pale sio ngono, ni kutiana moyo, kufarijiana na kupambana na hali iliyopo kwanza ndio ngozi zije baadaye....kwenu ninyi watoto wadogo ndio mnaamini ndoa ni ngono tu. akili zenu zipo makalioni.