Uchaguzi 2020 Kwa vitendo na takwimu zilizotapakaa kwenye kila Sekta inatosha kusema Mitano Tena kwa Dkt. John Pombe Magufuli

mkanta majura

Member
Sep 22, 2020
97
71
Kwa mfululizo wa vitendo vinavyotoa sauti, kuonwa na kusikika na kila mmoja na mfululizo wa takwimu zilizoshiba alizozifanya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa miaka mitano tu ya uongozi wake vinamfanya kila mwananchi akifika kwenye sanduku la kupiga kura siku ya Oktoba 28 kuchukua tu kura yake na kuweka kwa Dkt John Pombe Magufuli ili kazi iendelee.

Kasi kubwa ya utekelezaji wa miradi ya maji 1423 yenye thamani ya trilioni 1.2 nchi nzima ambayo imefanya sasa upatikanaji wa maji kuongezeka maradufu vijijini kutoka asilimia 47 mwaka 2015 hadi asilimia 70.1 na mijini upatikanaji wa maji ukiongezeka kutoka asilimia 74 mwaka 2015 mpaka asilimia 84 mwaka huu. Umoja wa Mataifa (UN) unasema uwekezaji huu mkubwa wa Serikali ya awamu ya 5 kwenye sekta hii muhimu ya maji imefanya nchi kuokoa takriban trilioni 5.2 ambazo Serikali ingetumia kutibu watu magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa maji safi na salama.

Kwenye Sekta ya umeme kila mmoja ameshuhudia kwa macho yake mapinduzi ya kihistoria. Kutoka vijiji 2018 tu vilivyokuwa na umeme toka tupate uhuru na alivyovikuta mwaka 2015, leo kwa miaka 5 tu Rais Magufuli ameshapeleka umeme mpaka zaidi ya vijiji 9570 na kubakiza vijiji chini ya 2500 tu. Hii imefikisha asilimia 85 ya vijiji vyenye umeme kutoka chini ya asilimia 35 mwaka 2015 na kuifanya nchi ya Tanzania kuwa nchi ya kwanza Afrika kwa usambazaji mkubwa wa umeme vijijini. Hii inajumuisha Serikali ya Rais Magufuli kupunguza kwa zaidi ya asilimia 60 gharama ya kuunganisha umeme kutoka 177,000 mwaka 2015 mpaka 27,000 tu, jambo lililowafanya Watanzania wengi sana hata wenye vipato vya chini kabisa kuunganisha umeme.

Hii inaifanya Tanzania kupita maoteo ya Benki ya Dunia (WB) ambayo yalikadiria suala la umeme kwa wote kufikiwa kwenye karne ya 22 kwenye mwaka wa 2101 lakini kwa kasi hii ya Rais Magufuli ambaye ameshasema mpaka kufikia mwaka 2025 vijiji vyote nchini vitakuwa na umeme hivyo kufika kwenye maoteo ya WB kabla hata ya muda wake wa takriban miaka 75 ijayo. Hii inaendana na Tanzania kuongoza kwa bei nafuu ya umeme kwa kaya kwa ukanda mzima wa Afrika Mashariki ambapo Tanzania inauza uniti 1 kwa senti 10, Uganda senti 18, Kenya senti 21 na Rwanda senti 26.

Yote haya yanafanikiwa kwa sababu ya Serikali ya Rais Magufuli kuwa na misingi mizuri ya usimamizi wa fedha ikiwemo kupambana na vitendo vya rushwa, ufisadi, ubadhirifu na uzembe ambapo Jukwaa la Uchumi duniani (WEF) kwenye ripoti yao ya mwaka 2019 iliitaja Tanzania kuwa ya 28 duniani kwa usimamizi madhubuti wa fedha na kuziacha nchi majirani na zingine kubwa duniani kwa mbali sana. Kenya wakiwa nafasi ya 70, Botswana 37, Msumbiji 69, Uganda 100 na Malawi 106.

Hii inathibitika pia kwa namna watu walivyo na imani kubwa na Serikali yao kwa kupambana na rushwa ambapo Taasisi ya Kimataifa ya Uwazi ya Transparency International (Global Africa Corruption Barometer ya 2019) ilisema asilimia 72 ya wananchi wana imani na Rais Magufuli katika vita dhidi ya ufisadi kulinganisha na asilimia 13 tu ya Watanzania ambao mwaka 2015 ndio pekee walikubali nchi yao kupambana na ufisadi.

Usimamizi huu mzuri wa rasilimali fedha ndio umeifanya Tanzania kuwa na uwezo mkubwa wa kutekeleza kwa fedha zake yenyewe za ndani miradi mikubwa ya kimkakati kama Ujenzi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere (Stirglers Gorge) inayotumia trilioni 6.5, ujenzi wa reli ya kisasa na ya mwendo kasi ya Standard Gauge (SGR) inayotumia Dola za Kimarekani bilioni 1.92 na kutoa elimu bila malipo kwa sababu fedha zote zilizokuwa zinaliwa na mafisadi zimekombolewa kwa kudhibiti wizi, ubadhirifu, ufisadi na matumizi yasiyo ya lazima.

Eneo la afya ambalo ni la msingi sana ili kujenga Taifa lenye ustawi, Serikali imeshajenga vituo 1769 vya kutolea huduma ya afya zikiwemo zahanati 1198, hospitali za wilaya 71, za mikoa 10 na za kanda 3 ikiwemo ujenzi wa hospitali ya mkoa wa Mara ambayo ilisimama toka miaka ya 1970, kupandisha bajeti ya madawa na vifaa tiba kutoka bilioni 30 mpaka bilioni 270, kuajiri watumishi 14,479 wa kada za afya na mengine mengi sana.

Mapinduzi haya makubwa kwenye sekta ya afya ndio yaliyolifanya Shirika la Afya Duniani (WHO) kuitaja Tanzania kupunguza maambukizi ya malaria kwa asilimia 50 kutoka asilimia 14.2 mwaka 2014 mpaka asilimia 7 mwaka 2018.

Kutoa elimu bila malipo ambapo Serikali imeshatumia takriban trilioni 1.01 kugharamia ambapo kutangazwa tu kwa fursa hiyo na Serikali, idadi ya wanafunzi wanaojiunga na darasa la kwanza iliongezeka kutoka wastani wa wanafunzi milioni 1 mpaka milioni 1.6, jambo lililookoa malaki kwa malaki ya watoto wa maskini ambao walikuwa wanakosa fursa ya kupata elimu. Kumbuka Takwimu hizi zote zinatolewa na hao hao Wazungu wenyewe ambao mapema mwezi July mwaka huu Benki ya Dunia iliitangaza Tanzania kuingia uchumi wa kati kutoka nchi maskini kabisa. Tanzania iliitangazwa na Benki ya Dunia kuingia Uchumi wa kati kwa haraka zaidi kabla hata ya mpango wake wa maendeleo ambao ulikadiria Tanzania kuingia uchumi ifikapo mwaka 2025.

Sasa kama Wazungu wenyewe wamemkubali Rais Magufuli na Serikali yake, nani tena abishe? Hapo hujaenda kwenye mapinduzi makubwa yaliyopatikana kwenye miundombinu ya barabara ambapo kwa mara ya kwanza toka Tanzania izaliwe ilipeleka fedha za miradi ya barabara kwenye mikoa na wilaya zote nchini. Ununuzi wa ndege 11 baada ya kusugua miaka kwa miaka na mindege ya kukodi na mibovu. Hujaenda kwenye mapinduzi mazito yaliyofanyika kwenye madini, utalii, kilimo na kwingine kwingi. Kwa bahati mbaya ukurasa hautoshi.

Mambo ni mengi sana lakini kwa uchache na kwa kumalizia ni eneo la amani na utulivu ambapo ndipo msingi wa utekelezaji wa mipango yote ya maendeleo. Hapa bado Serikali hii imeendelea kuweka mkazo mzito sana kwa kuifanya Tanzania kuendelea kuwa kitovu na kisiwa cha amani kote duniani jambo lililofanya mtandao wa Global Peace Index unaohusika na kupima hali ya amani duniani kuitaja Tanzania kuwa nchi yenye amani na utulivu wa hali ya juu sana Afrika na dunia kwa ujumla. Kwa mujibu wa ripoti ya mtandao huo mwaka 2020 iliitaja Tanzania kuongoza kwa amani na utulivu Afrika Mashariki, huku ikishika nafasi ya 6 barani Afrika na 52 duniani. Kwa vitendo na takwimu hizi chache tu kati ya nyingi zilizotapakaa kwenye kila sekta inatosha kusema Mitano Tena kwa Dkt John Pombe Magufuli ili kazi iendeleeee.
 
Watu wengi wa CCM huwa mnashindwa kuelewa mambo. Yaani nyinyi kwa akili zenu mnafikiri kuwa kujenga barabara, madaraja, na kununua ndege pekee ndio kigezo cha Rais kupigiwa kura na wakati kuna mambo mengi sana ambayo ni vipaumbele vya wananchi zaidi ya hivyo.
 
Utopolo Mtupu.

Mtu anaomba kura hadi kwa kupiga magoti

Mmejawa na uongo kama selikali ya mashetani.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Watu wengi wa CCM huwa mnashindwa kuelewa mambo. Yaani nyinyi kwa akili zenu mnafikiri kuwa kujenga barabara, madaraja, na kununua ndege pekee ndio kigezo cha Rais kupigiwa kura na wakati kuna mambo mengi sana ambayo ni vipaumbele vya wananchi zaidi ya hivyo.
Kama yapi?
 
Watu hawataki kuona flyover wanataka kuona pesa mitaani, stiglas goji itamsaidia nini mjamzito anayelipishwa pesa ya kujifungua mtoto wa kike.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Watu hawataki kuona flyover wanataka kuona pesa mitaani, stiglas goji itamsaidia nini mjamzito anayelipishwa pesa ya kujifungua mtoto wa kike.
kwani hiyo mimba ilikuja ghafla? Mbona unaongea mambo ambayo wewe mwenyewe huyajui nani alikupeleka shule ya Mapenzi?
 
Mitano watu waendelee kuishi maisha magumu ya ubaguzi, kufungwa kwa uonevu na umasikini wakutupwa? mchangue wewe na familia yako mimi naelekea Kanani
Huyo kibaraka ndio akitawala utakuwa na maisha rahisi?. Watanzania tumieni akili hata kidogo basi. Ugumu wa maisha na umaskini upo Kwenye fikra zako, maana huoni fursa zilizopo. U S pamoja na kwamba ni matajiri ila kuna maskini wa kutupwa kule. Huyu wakala wa beberu anawahadaa kisa yeye tayari ni raia wa Ubelgiji, kwani atawapeleka huko?

Hakuna Serikali inayowawekea pesa wananchi wake mifukoni, hakuna vya bure jombaa. Komaa kamanda. Chadema na genge lake hawana cha kuwapa watanzania, ahadi watoazo wanapiga mgumi upepo. Watanzania makini hawawezi wapa kura kwa Sera ambazo hata wao wanajua hazitekelezeki,na worse enough wanajua kabisa hawawezi kushinda Urais hata jua litoke usiku.

Anyways let say Lissu anashinda, itamchukua miaka 5-10 aweze kuweka mifumo ambayo itamsaidia kutawala maana hatawezana na mifumo ambayo Baba la demokrasia imeiweka tangu uhuru na hapo ndipo tutakaporudi nyuma miaka 50.Nani anamuda wa kupoteza kwa trial and error?

Serikali ya ccm imesha weka misingi na mifumo imara, watanzania ni kuitimia kujiletea maendeleo. Magufuli hata akiongezewa mingine 20 itakuwa Bomba Sana. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CCM.
 
Watu hawataki kuona flyover wanataka kuona pesa mitaani, stiglas goji itamsaidia nini mjamzito anayelipishwa pesa ya kujifungua mtoto wa kike.
Huku mtaani wameua sector binafsi,biashara za watu zimeuwawa kinyama.setikali ndo inataka kufanya biashara yenyewe,tenda zote mpaka za ujenzi miradi ya serikali wanafanya wao hela zitazungukaje huku mtaani.ulinzi kwenye Mali zote za serikali wanawapa suma jkt.mandege ya binafsi wameua ili wafanye wao.

Huku mtaani hali ni ngumu sana hata ukifungua biashara kodi sio rafiki.uatajikuta hata kodi nayo unailipia kodi
 
Huyo kibaraka ndio akitawala utakuwa na maisha rahisi?. Watanzania tumieni akili hata kidogo basi. Ugumu wa maisha na umaskini upo Kwenye fikra zako, maana huoni fursa zilizopo. U S pamoja na kwamba ni matajiri ila kuna maskini wa kutupwa kule. Huyu wakala wa beberu anawahadaa kisa yeye tayari ni raia wa Ubelgiji, kwani atawapeleka huko?....
Beberu ni yule mwanaume.?

Kazi yenu ngumu sana mataga
 
Shule ya mapenzi nilipekwa na Magufuli, anything more?
. Tatizo wewe Ni Mtanzania unayeishi ndani ya Tanzania 2 tembea uone Dunia ilivo mbaya Kama lisu atashinda naomba tujenge urafiki nje na Jf unidai chochote
 
Kwa mfululizo wa vitendo vinavyotoa sauti, kuonwa na kusikika na kila mmoja na mfululizo wa takwimu zilizoshiba alizozifanya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa miaka mitano tu ya uongozi wake vinamfanya kila mwananchi akifika kwenye sanduku la kupiga kura siku ya Oktoba 28 kuchukua tu kura yake na kuweka kwa Dkt John Pombe Magufuli ili kazi iendelee...
Mbona hujasema hela za wahanga wa tetemeko
Wakullma wa korosho mpaka Leo hawajalipwa
Mashekh walio Jazana jela Kwa tuhuma za ugaidi
Tanzanian kwa miaka mitano imeshikilia watuhumiwa wa ugaidi kuliko Afghanistan na Iraq
Bomoa bomoa bila fidia
Mauaji ya halaiki yanayofanywa na watu wasiojulikana
Unyang'anyi wa pesa za wafanyabiashara
Kulipiza visasi
Kinyongo kisichoisha
Udhalilishaji wa wanawake hasa weusi
Funguo za hazina za nchi nzima chini ya mtoto wa dadake
Kandarasi zote kupewa mume mwenza bila zabuni
Ununuzi wa ndege nyuma ya pazia
Kujenga kiwanja cha kimataifa nyumbani
Kujimilikusha ardhi 25000 ya wananchi
Kufukuza zaidi ya wanafunzi 10000 chuo kikuu
Kudhulumu mafao ya wastaafu
Wafanyakazi bila nyongeza ya mishahara
Hizi ni baadhi tu ya dhulma watu walizofanyiwa moja kwa moja
Lakini kujenga vitu fulani Havina faida wala madhara ya moja kwa moja kwa wananchi
 
Mbona hujasema hela za wahanga wa tetemeko
Wakullma wa korosho mpaka Leo hawajalipwa
Mashekh walio Jazana jela Kwa tuhuma za ugaidi
Tanzanian kwa miaka mitano imeshikilia watuhumiwa wa ugaidi kuliko Afghanistan na Iraq
Bomoa bomoa bila fidia
Mauaji ya halaiki yanayofanywa na watu wasiojulikana
Unyang'anyi wa pesa za wafanyabiashara
Kulipiza visasi
Kinyongo kisichoisha
Udhalilishaji wa wanawake hasa weusi
Funguo za hazina za nchi nzima chini ya mtoto wa dadake
Kandarasi zote kupewa mume mwenza bila zabuni
Ununuzi wa ndege nyuma ya pazia
Kujenga kiwanja cha kimataifa nyumbani
Kujimilikusha ardhi 25000 ya wananchi
Kufukuza zaidi ya wanafunzi 10000 chuo kikuu
Kudhulumu mafao ya wastaafu
Wafanyakazi bila nyongeza ya mishahara
Hizi ni baadhi tu ya dhulma watu walizofanyiwa moja kwa moja
Lakini kujenga vitu fulani Havina faida wala madhara ya moja kwa moja kwa wananchi
Mateso tupu
 
Back
Top Bottom