Kwa viongozi wa cdm baada ya 2015

Kwa viongozi wa cdm baada ya 2015

Jumanne Mkota

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
3,011
Reaction score
1,793
Ndugu wana Jamvi

huu ni mtizamo wangu na pia inawezekana ni elimu isiyorasmi (yaani si ya darasani) ambayo nimeipata kwa babu na bibi zangu na pia kujionea na kujifunza mambo mbali mbali kwa kipindi chote ambacho nimejitambua (childhood to manhood). Tanzania yetu ipo mbioni kukombolewa kutoka kwa mkoloni wa pili, mkoloni mweusi na mkoloni wa ajabu kuliko hata wakoloni waingereza na wajerumani ambao walituelimisha na pia kututibu bure! mkoloni jambazi, mwizi, kibaka, mzinzi nk. Kwa mbali kabisa naiona nyota ya ukombozi imeshaanza kung'aa .

Tuna viongozi wengi makini ndani ya CHADEMA ambao wametufikisha hapa tulipo, hakuna asiyewajua. Nashauri baada ya ukombozi mwaka 2015, mwaka 2020 viongozi wote hasa hawa wabunge waliopo na watakaokuwepo kazi yao ya ukombozi itakuwa imeshakwisha! hivyo ni vyema wakarudi au kubaki kwenye chama kukirutubisha zaidi au kuondoa magugu yaitwayo CCM kwenye shamba letu Tanzania.

Kuna viongozi na wabunge wengi wa CHADEMA ambao wameathirika sana au kuathiriwa na serikali hii ya CCM. Nitamtaja Lema ambaye ni waziri kivuli wa wizara ya mapolis. Huyu Bwana hata tukipata Rais ukimteua kuwa waziri wa mambo ya Ndani litakuwa ni kosa na Lema hata fit hapo. Kwa sababu mapolisi wanaomtesa leo hao hao ndio watakuwa maofisini kipindi cha 2015 - 2020. Kama great thinker unajua nini kitajiri.

Hivyo hivyo Tindu Lisu kama waziri wa sheria ama kuwa AG majaji aliowatuhumu wataendelea kuwa majaji kesi za serikali ya CHADEMA kipindi zitakuwaje? Najua tutakuwa na kipindi cha miaka 2 au mitatu ya kuunda na kuendesha serikali adilifu, Najua tutapigika pia kwa kuwa tutakuwa tunabadilisha mfumo .

Nashauri CHADEMA sasa tuandae na tuibue viongozi wengine wenye mtizamo wa kiuchumi na mahusiano. Tujifunze kutoka kwa nyerere ambaye aliweka wapigania uhuru wengi zaidi kwa miaka 20 ya utawala wake na kinachotokea sasa. Failure kubwa ya CCM ni kuwa ina wapigania uhuru wengi kuliko waleta maendeleo. Ndo maana mnaona mawaziri wanavyopiga dili za kuangamiza kwa sababu hawajui kesho itakuwaje.
 
Back
Top Bottom