Kwa vijana wenzangu wa kiume

Prince Naahjum Alsina

Senior Member
Jun 13, 2016
136
124
5df6e3648b98c6aa4c31c861199d016f.jpgNawaandikia ninyi vijana wenzangu wa kiume na wanaume wote, maana tuna nguvu na mmejaliwa na mwenyezi Mungu utashi, hekima na busara.

Yote hayo ni ili tuweze kutawala kila kitu tokea kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu. Tuwekeni wivu pembeni na tuyafuate haya;

1. Oa mwanamke ambae unaweza KUSALI nae na sio kwa sababu anajua KUFANYA MAPENZI vema.

2. Mwanaume bora KAMWE hapimwi kwa idadi ya wanawake alionao au aliotembea nao BALI kwa idadi ya wanawake aliowaambia "Mimi ni mume wa mtu" au ninae mtu tayari.

3. Kuna aina ya wanawake unatakiwa kuwaepuka kabisa kwa gharama yoyote ile, "wanawake wamaodhani uzuri wao ndio bora zaidi kuliko tabia zao"

4. Kila mwanamke anavutia akivaa nguo fupi inayoonesha maungo yake wazi, ila kama utakuta mwanamke amevaa nguo ndefu au za kusitiri mwili wake na bado anavutia, huyu ni dhahabu! Anathamini mali za mumewe!

5. Kamwe usimpe mwanamke mimba ya mtoto kabla hujampa mimba ya malengo na ukayatimiza.

6. Tafuta mwanamke ambae atakupa challenge ya maisha na kuongeza uwezo wako wa kufikiri na sio mwanamke wa kila kitu Ndio mzee!

7. Wanawake wakamilifu hawapatikani popote duniani, ila wanawake bora wapo kila mahali.

8. Mwanamke anaweza kukusaliti, ila Mungu hawezi kukusaliti, hivyo basi kabla hujapata mwanamke Mpate Mungu kwanza. Kuna raha sana kuwa ndani ya Mungu asikwambie mtu!

9. Kama unajijua umefikisha miaka 25 na kuendelea epuka mambo ya kivulana, kuvaa suruali katikati ya makalio, kuvaa hereni, kubadili badili wanawake kama unachambua mitumba ya karume etc

10. Usitumie kichwa chako kunyoa kiduku, tumia kichwa chako kuwaza mambo yenye tija ikiwemo kutafuta pesa na kuongeza hazina ya maarifa.

"Being a male is a matter of birth, being a man is a matter of age, but being a gentleman is a matter of choice. A best choice indeed!"

SharePRINCE NAAHJUM ALSINA
The Great Pioneer
 
Number 6 kiukweli hapo umeongea kabisa. Because women always mistaken kindness with weakness
 
Ni vyema umenena, ila najaribu kuunga dots ili nipate picha vizur kati ya namba 9 na hiyo picha yako.
 
Back
Top Bottom