Kwa utajiri huu wa Afrika, viongozi aina ya Rais Magufuli, Mugabe na Mseveni wataifikisha pazuri

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,581
Inauma sana! Nianze kwa kusema hivyo!

Africa tuna ardhi kubwa yenye rutuba, mbuga za wanyama, madini ya kila aina, misitu ya kutosha, vyanzo vya maji vya kutosha kuanzia Bahari, Maziwa Makubwa, Mito Mikubwa, Mabwawa makubwa , Mbuga za wanyama wa kila aina, Uhuru, Wasomi na siasa safi,lakini bado tunalia njaa, tunalia na kusaga meno, tuna majonzi, tuna stress, tuna hofu na umaskini wa kutupwa kabisa.

1. Uhaba wa hospitali na madawa

2. Uhaba wa madawati na vifaa vya kufundishia

3. Kilimo duni

4. Miundombinu hovyo ya barabara ,reli na maji

5. Maji shida tupu

6. Mishahara ya watumishi midogo mno

7. Ukosefu wa viwanda vidogo vidogo na vya kati

8. Makazi hovyo ya raia wake

9. Ukosefu wa ajira

etc etc.

Ni lazima tuwe na viongozi wenye moyo, wazalendo, wakali na wenye chachu ya kuhakikisha keki za taifa kila mtu anafaidi kwa urefu wa kamba yake. Hatuwezi kuwa na viongozi wa kutuchezea hata kidogo. Tumechoka sana!

Viva viva Rais Magufuli.

Endelea hivyo hivyo. Watasema watachoka
 
Tuangalie yasije tupata ya zimbabwe mkate unauzwa milioni kumi. Waliotangulia ndio waliiuza hii nchi. Msomi mzima unasaini eti nchi ipate mrahaba wa 3%? Shame on us.
 
Kwa hiyo unataka kusema JPM anafuata nyayo za Mugabe ili na sisi siku moja tukafike pale walipofika Zimbabwe, na kufaidi mema ya nchi kama ndugu zetu Wazimbabwe?
 
Viongozi ambao hawajipanga hawawezi kuwapeleka kokote.
Miaka nenda rudi Zimbabwe ipo hovyo. Hizo rasilimali zimewasaidia vipi?
Viongozi wanaokurupuka wanawaletea matatizo lukuki, mfano ubinafsishaji wa nyumba za serikali, kivuko kibovu kilichopelekwa jeshini na wale samaki tulioishia kulipa fidia.
 
Umafananisha au kulinganisha watu ambao hafaelekeani wala kufanana. Mugabe na Pombe wapi na wapi?
 
Hakuna kitu Mugabe kaifikisha wapi nchi yake.

Huyu wetu nae mbwembwe tu nae ni mpigaji.

Afrika tutabaki hapahapa hakuna maendeleo yatakayoletwa na hawa viongozj wetu
 
Kwa kweli tutaendelea...na hasa ukiangalia namna Mugabe alivyoiendeleza na kuikuza Zimbabwe kiuchumi na kimaendeleo kiasi cha Mugabe kuwa mfano bora wa Rais anaesimamia Rasimali za nchi kujiletea maendeleo

[HASHTAG]#NdivyoTulivyo[/HASHTAG]
 
You need INNOVATION ! And then SKILLS to bring what is called INVENTIONS through Technology but remember among population only 2.5% are innovators
 
umemtaja museven hapo
Ni miaka mingapi museven ametawala uganda? lakin hamna kitu
 
umemtaja museven hapo
Ni miaka mingapi museven ametawala uganda? lakin hamna kitu
 
Inauma sana! Nianze kwa kusema hivyo!

Africa tuna ardhi kubwa yenye rutuba, mbuga za wanyama, madini ya kila aina, misitu ya kutosha, vyanzo vya maji vya kutosha kuanzia Bahari, Maziwa Makubwa, Mito Mikubwa, Mabwawa makubwa , Mbuga za wanyama wa kila aina, Uhuru, Wasomi na siasa safi,lakini bado tunalia njaa, tunalia na kusaga meno, tuna majonzi, tuna stress, tuna hofu na umaskini wa kutupwa kabisa.

1. Uhaba wa hospitali na madawa

2. Uhaba wa madawati na vifaa vya kufundishia

3. Kilimo duni

4. Miundombinu hovyo ya barabara ,reli na maji

5. Maji shida tupu

6. Mishahara ya watumishi midogo mno

7. Ukosefu wa viwanda vidogo vidogo na vya kati

8. Makazi hovyo ya raia wake

9. Ukosefu wa ajira

etc etc.

Ni lazima tuwe na viongozi wenye moyo, wazalendo, wakali na wenye chachu ya kuhakikisha keki za taifa kila mtu anafaidi kwa urefu wa kamba yake. Hatuwezi kuwa na viongozi wa kutuchezea hata kidogo. Tumechoka sana!

Viva viva Rais Magufuli.

Endelea hivyo hivyo. Watasema watachoka
Mugabe! Umeshafika Zimbabwe au unasikia propaganda? Nchi ambayo haina sarafu yake ndo unataka twende huko. Mungu pishilia mbali!
 
Hakuna kitu Mugabe kaifikisha wapi nchi yake.

Huyu wetu nae mbwembwe tu nae ni mpigaji.

Afrika tutabaki hapahapa hakuna maendeleo yatakayoletwa na hawa viongozj wetu
Na hivi bunge letu ni la komoakomoa badala ya kusimamia katiba,sheria na sera za kulinda haki na kuleta maendeleo; twafwa huku tunajiona.
 
Back
Top Bottom