kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,086
UHALIFU umekuwa ni adui mkubwa wa maendeleo kwa mtu binafsi, familia na hata Taifa kwa ujumla. Pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama kukabiliana na uhalifu huo, lakini pia wahalifu nao wamekuwa wakibuni mbinu mbalimbali za kutekeleza uhalifu.
Utakubaliana nami kwamba eneo lolote lenye uhalifu uliokithiri, hata maendeleo yake yamekuwa ni ya kusuasua. Tumeshuhudia hata katika baadhi ya nchi za wenzetu ambazo uhalifu umekithiri, wame kuwa wakirudi nyuma na hivyo kuhitaji misaada kutoka maeneo mengine.
Ni ukweli usipopingika hata katika maeneo yenye rasilimali nyingi, iwapo utajitokeza uhalifu basi maeneo hayo hurudi nyuma kimaendeleo na mwishowe kudidimia kabisa na badala ya kuwa maeneo tegemewa hugeuka tegemezi.
Pamoja na jitihada zinazofanyika za kukabiliana na uhalifu, lakini pia kumekuwa na tabia ya watu wanaojitokeza kufanya uhalifu sehemu moja na kukimbilia nyingine au hata nchi moja na kukimbilia nchi nyingine.
Hata hapa kwetu, wapo wahalifu ambao wamekuwa wakitoroka na kukimbilia nchi zingine, baada ya kuona kwamba hali imekuwa mbaya. Hali hii ndiyo imelifanya jeshi la polisi nchini, kuamua kusaini mkataba wa ushirikiano wa kuzuia na kupambana na uhalifu haswa katika masuala ya ugaidi, dawa za kulevya, utakatishaji fedha na makosa mbalimbali yanayovuka mipaka.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro alisema makubaliano hayo wamekuwa wakiyafanya na nchi mbalimbali, ambapo kwa Msumbiji walisaini jana. Alisema makubaliano hayo yamelenga kuhakikisha Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla ni salama.
Pamoja na hayo, Sirro alisema kubwa zaidi wamekubaliana kubadilishana taarifa kwa lengo la kuhakikisha Watanzania na wana Msumbiji, wanaishi kwa amani na utulivu. Tunapongeza majeshi haya na tunaamini kwamba ushirikiano wao na makubaliano yao yataleta matokeo chanya katika masuala ya ulinzi na usalama.
Kuna usemi niliusikia kwamba ‘Usipoziba ufa utajenga ukuta’ na mimi nilielewa kwamba ukifumbia macho jambo dogo lenye kuhatarisha, mwishowe gharama yake huwa ni kubwa. Ndivyo tunavyoona hata kwa baadhi ya wenzetu, mambo yanayowatokea, mengine yalifumbiwa macho.
Siyo kweli kwamba machafuko yote au hata makosa yote yanayojitokeza huko ni kwamba yalilipuka tu, ila mengine yalianza kidogo kidogo. Majeshi yetu yameyaona haya mapema na tunaamini kwamba masuala ya matukio ya ugaidi, utakatishaji fedha, dawa za kulevya na mengine ya uhalifu yanayovuka mipaka yanahitaji ulinzi wa pamoja ili hata wanapodhibitiwa sehemu moja wasiweze kuhamia sehemu nyingine.
Naamini dhana hiyo ya ushirikiano wa pamoja, itasaidia kudhibiti wale wahalifu, ambao wamekuwa wakitoroka, kwa kuwa hata katika matukio yaliyotokea Kibiti, Ikwiriri na ukanda huo, wahalifu wake wengine tuliambiwa wamekimbilia Msumbiji baada ya kudhibitiwa katika maeneo hayo.
Hivyo tunaamini kwamba ushirikiano huo, utasaidia hata wale waliokuwa wamekimbilia maeneo hayo, kudhibitiwa na kuzifanya nchi kuwa salama na wananchi kuishi kwa amani na utulivu.
Tunaamini kwamba endapo ushirikiano huo, utaendelezwa masuala ya uhalifu yatakoma na wananchi watafanya kazi na kujipatia vipato halali na kujiletea maendeleo yao wenyewe na Taifa kwa ujumla.