Uchaguzi 2020 Kwa umati uliofurika leo Viwanja vya Matogoro Mjini Tandahimba, ni wazi hakuna wa kumzuia Tundu Lissu kuwa Rais

Ben Bella

JF-Expert Member
Dec 3, 2019
529
1,856
Wakazi wa mji wa Tandahimba na vitongoji vyake walikusanyika kwa wingi kwenye viwanja vya shule ya msingi Matogoro ili kumpokea mgombea urais anayeiwakilisha CHADEMA Mh. Tundu Lissu.

Kwa hakika umati ulikuwa mkubwa haijapata kutokea. Hamasa ilikuwa juu sana.

Huku watu wakiendelea kumiminika, ikaletwa taarifa kwamba Tundu Lissu hatafika kwenye hadhara hiyo kwani hana kibali cha kufanya mkutano wa kampeni katika jimbo la Tandahimba.

Kwa taarifa hiyo wananchi walitakiwa kutawanyika mara moja kurejea makwao. Ila ilichukua muda wa nusu saa watu kuondoka toka viwanjani hapo kwani wengi wao walisikika wakiilaani serikali ya CCM na wengi wao waliapa kumchagua Lissu kwa kishindo kikuu ifikapo tarehe 28 Oktoba mwaka huu.

Nadiriki kusema kwa umati ulioshuhudiwa viwanjani hapo leo, hakuna wa kumzuia Lissu kuingia Ikulu ya Chamwino.

Credit: kwa rafiki yangu aliyeko Tandahimba, kwa taarifa.
 
Ungepiga picha na kuitupia hapa.

Ama ikawaje watu wakakusanyika kumsubiri Tundu Lissu huku ikijulikana hana ratiba ya kufanya mkutano eneo hilo?

Viongozi wa eneo hilo hawana mawasiliano na mratibu wa kampeni za mgombea Urais kwani?
 
Kujidanganya ni jambo zuri kiafya. Husaidia kuongeza chembechembe hai nyeupe za damu mwilini.


Zawadi yako hii


1603447018041.png
 
Back
Top Bottom