Kwa Ukubwa wa Hili Begi Atakua Anajua

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,153
13,223

Emerson mchezaji mpya wa 'maximo' alipotua leo Dar, nimefurahishwa na ukubwa wa begi lake kwamba ana uhakika wa kubaki na si kama mwenzie Jaja.................ama badu kama hakujifunza namsihi asije akalisahau chumbani
 
Hao ndio yanga...timu ya magazeti...timu ya kumpigia magoti kanjibhai.....mtaletewa hadi wauza pombe bar kutoka brazil...yaaani yanga ni wa kuonewa huruma......................
 
Maximo amevua za Jaja na huyu nazo anavuna tena
 
Mbona kafanana na Maximo?
ana undugu naye nini?
Halafu umri wake?
manake naona kama anaikimbia arobaini....
 
Yanga huwa ni hodari wa kupokea na wavivu wa kuaga
 
Kuna uhusiano gani wa urefu wa mwili na uwezo wa kucheza soka? Naomba mtaalam anijibu.

Maximo ni mwalimu wa muda mrefu. Nimekuwa nikiuatilia sana uchaguzi wake mara zote ameonekana kukubali watu warefu zaidi ya wafupi.

Mfano Ivo V/s Kaseja.

Naomba scientific reasoning.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…