Kwa ufisadi huu, katiba ya sasa ingetufaa sana.

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Pamoja na mapungufu na kasoro nyingi kwenye katiba ya sasa,lakini lazima tutambue kuwa kwenye masuala ya ufisadi na uhujumu uchumi katiba inafaa sana kwani imetoa madaraka makubwa kwa mkuu wa kaya.Kwanini nasema hivi.Sababu ni moja tu nayo ni udhaifu wa mkuu wa kaya mwenyewe kutumia rungu zito alillopewa.

Rungu kwa sasa linaweza kumfanya mkuu wa kaya kuwa hata dictator.Sasa angeamua kuwa dictator kwa mafisadi na wahujumu uchumi wa nchi hii watu si wangenyooka.Siku zote watuhumiwa wengi wa ufisadi ni wateule wake na yeye tu ndie mwenye maamuzi na wengine ni washauri tu na ana haki ya kukubali ushauri au kukataa.Ndio maana taifa zima kuanzia bungeni mpaka kijiweni tumebaki walalamikaji tu kwani mwenye rungu lake kalipa likizo au tuseme kaliweka mfukoni.

Ushahidi wa rungu kuwa likizo ni msamaha kwa wezi wa EPAA tena alioutangaza pale mjengoni mwaka 2008 mbele ya waheshimiwa na ikabidi mh.spikaaa wa speed na viwango vya tbs amtake awe mkali kidogo.Jamani si mnakumbuka ile kauli au mmesahau?Na hapa hata rungu lake hakulitendea haki kwani katiba inampa mamlaka kusamehe wale tu waliopatikana na hatia na kufungwa na sio watuhumiwa kama wale wa EPAA.

Rungu hili angepewa mtu kama mh.John Makufuli nadhani mafisadi wote wangekuwa ndani ila basi tu tuwe wapole mpaka jamaa amalize muda wake, ila sipati picha tutakavyoendelea kupigika mpaka atakapostaafu na kufaidi pensheni yake nono.
 
...rungu analitumia, ila kinyume chake. Mf. Kusamehe wezi,
 
Back
Top Bottom