BungelaKatiba2014tz
JF-Expert Member
- Feb 18, 2014
- 1,231
- 649
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepitisha jina la Vicent Mashinji kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho. Mashinji ni mwenyeji wa Sengerema Mkoa wa Mwanza, mkoa unaounda Kanda ya Ziwa ikiwemo, Mara, Shinyanga, Geita na Kagera. Hii ni Kanda ambayo kisiasa ina umaarufu wake hususan wakati wa Uchaguzi Mkuu unaofanyika kila baada ya miaka mitano kutokana na kuwa na idadi kubwa sana ya wapiga kura.
Tayari yameanza kusema maneno kwamba, Mbowe ameamua kuteua Katibu Mkuu wa chama hicho kutoka Kanda ya Ziwa kwa sababu rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daktari John Pombe Magufuli anatokea Mkoa wa Geita, Kanda ya Ziwa ili kukabiliana na nguvu ya chama cha Mapinduzi kisiasa katika kanda hii. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, Mbowe ameshtushwa sana na kasi ya rais hivyo kuingiwa na hofu ya chama hicho kufutika kabisa katika Kanda hiyo.
Pengine niseme Mbowe kaona mbali, LAKINI, kwa jinsi ambavyo siasa za Tanzania kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu kumalizika oktoba mwaka 2015 zilivyojipambanua , itakuwa ni vigumu sana maono haya ya Mh. Mbowe kuzaa matunda. Wakati wa Kampeni na wakati wa utoaji wa matokea ya urais, ukanda, ukabila ulijidhihirisha wazi katika katika kanda ya Kaskazini ukilinganisha na maeneo mengine ya nchi. Idadi za kura alizopata mgombea wa Chadema, Edward Lowassa na mgombe wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli katika mikoa ya Kilimanjaro na arusha ilikuwa inadhihirisha hilo.
mtazamo wangu: Kama watu wa Kanda ya ziwa watataka kulipiza kisasi katika chaguzi zitakazofuata, kwa maana kwamba wakawa na kauli mbiu yao ya "KANDA YA ZIWA KWANZA , CHAMA BAADAYE" hakika uteuzi huu wa kuingia kichwakichwa unaweza kugeuka kuwa shubiri kwa Mbowe na chama kwa ujumla.
Mbegu iliyopandikizwa Katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro hasa baada ya Lowassa kujiengua CCM na kuhamia CHADEMA na hatimaye kuteuliwa kgombea urais kupitia chama hicho, imeota, imekuwa na sasa mazao yake tunayaona huko mitaani leo hii pamoja na kwamba uchaguzi ulishapita na tunachotakiwa kufanya ni kushikamana na rais mteule ili kuijenga Tanzania. Leo hii ukiwa kwenye vijiwe, kwenye kumbi za burudani , kwenye baa na maeneo mengine yenye mikusanyiko ya watu, utasikia Magufuli , Magufu, Magufuli. Anasifiwa sana. Lakini akatokea mtu mmoja anapinga kasi ya mzee wa HAPAKAZITU, utasikia watu wanajibu, tumeshakujua wewe, Mchagga au mtu wa arusha. Na ukifanya uchunguzi unagundua ni kweli mtu huyo aidha ni mchagga au anatokea arusha tena Maeneo ambayo Lowassa anajulikana sana. Hawana sababu ya msingi ya kumkosoa Magufuli katika harakati zake za kuijenga Tanzania mpya, ni chuki tu kwa sababu Lowassa hakua rais na Chadema haikushika dola.
Mbowe amuombe sana Mungu watu wa Kanda ya ziwa , milango yao ya fahamu isije ikafunguka kama ambavyo watu wa Kilimanjaro na arusha ilivyofunguka. Dalili zipo kuwa milango yao ya fahamu inaweza kufunguka, tusije tukashangaa kadri siku zinavyokwenda , Lowassa na Mbowe kukanyaga Kanda ya ziwa wakaona kama wanakwenda GWANTANAMO