Kwa tuhuma hizi, CHADEMA kifumuliwe na kiundwe upya

Status
Not open for further replies.

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
Wadau, amani iwe kwenu.

Sheria inayounda vyama vya siasa imeweka misingi imara ili mfumo wa vyama vingi uwe msingi wa kuimarisha demokrasia nchini na kuzuia vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani, utulivu na hivyo kuondoa usalama wa nchi. Hata hivyo, pamoja na malengo mazuri ya mfumo wa vyama vingi nchini na dhamira njema ya waasisi wa mfumo huo, baadhi ya vyama vya siasa hutamani mfumo huo uwe sababu ya kujitwalia madaraka kwa njia zisizo za kidemokrasia.

Kuna dalili kwa baadhi ya vyama vya siasa kuanza kutumia vibaya uhuru wa kidemokrasia tulionao na kuanza kupandikiza chuki miongoni mwa jamii. Aidha, baadhi ya vyama vinashutumiwa kwa kuendesha matendo yanayolenga kuhatarisha usalama wa nchi. miongoni mwa vyama hivyo ni Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Chama hiki kimewahi kuhusishwa na matukio kadhaa yasiyo ya kawaida yanayoenda kinyume na misingi ya kidemokrasia nchini. Miongoni mwa matukio yaliyowahi kuripotiwa ni;


1. NJAMA ZA KUTEKA NA KUTESA WATU

Hemedy KANGENZI, Mlinzi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, DK. Wilbroad SLAA aliwahi kuripoti tukio la kutekwa kwake lililotokea tarehe 7 Machi 2015. Utekaji huo uliongozwa na Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob pamoja na makamanda kadhaa wakiwemo Anthony Komu, Benson Kigaila na Dr SLAA na ulifanyika Makao Makuu ya CHADEMA, Kinondoni, Dar es Salaam. Kesi ilifunguliwa mahakama ya Kisutu na mpaka sasa haijulikani imeishia wapi. Kangenzi kwa sasa ameathirika kisaikolojia kutokana na mateso aliyopata siku ya tukio.

2. KUHUSISHWA NA MILIPUKO YA MABOMU MKOANI ARUSHA

Baadhi ya watu waliwahi kukituhumu chama hicho kwa kuhusika na miripuko ya Olasit na Soweto Mkoani Arusha. Kwamba, CHADEMA walihusika na miripuko hiyo kwa lengo la kujipatia umaarufu wa kisiasa na kutaka huruma ya wananchi.

3. KUMILIKI KIKUNDI CHENYE MWELEKEO WA KIGAIDI

Waziri wa Mambo yan Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba aliwahi kukituhumu Kikundi cha Ulinzi cha CHADEMA, REDBRIGADE kuwa ni kikundi cha kigaidi kinachojihusisha na kuteka, kutesa na hata kuua watu. CHADEMA hawajawahi kukanusha madai hayo na Waziri Nchemba hajawahi kufuta kauli yake.

4. KUMWAGIA WATU TINDIKALI

CHADEMA wanatuhumiwa kumwagia tindikali mkazi wa Tabora, Ndugu Tesha wakati wa uchaguzi mgodo Jimbo la Igunga ambapo Dr Dalali Kafumu wa CCM aliibuka mshindi. Mwigulu Nchemba alizunguka na Tesha nchi nzima ili kuonesha Watanzania ukatili aliofanyiwa Mtanzania huyo. Mwigulu yupo na anaweza kuthibitisha madai haya

5. KUPOTEZA WATU KUSIKOJULIKANA

Msaidizi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Ben Saanane amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha. Awali, wakati minong’ono ya kupotea Ben ilipoanza kuripotiwa, mfuasi wa CHADEMA mitandaoni ambaye ni miongoni mwa wafanyakazi wa Redbrigade, HILDA NEWTON MSIGALA alitoa taarifa kuwa Ben Saanane hajapotea bali yupo Afrika ya Kusini alikopewa kazi maalum na Bosi wake (Mbowe). Aidha, Mbunge wa Ubungo, SAED KUBENEA alitumia gazeti lake la Mwanahalisi kuwaeleza Watanzania kuwa Ben yupo hai na anamuona kwenyevijiwe vya kahawa. Kwa muktadha huo, ni wazi kwamba, kupotea kwa Ben kuna mkono wa CHADEMA.



6. KUTISHIA KUANGAMIZA WATU KWA SUMU

Mbunge wa Kigoma Mjini ZITTO KABWE wakati akiwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Bara), aliwahi kumtuhumu Ben Saanane kuwa alitaka kumuwekea Sumu kwenye maji walipokutana kwenye Hotel ya Lunch Time iliyopo mkabala wa Mabibo Hostel Jijini Dar es Salaam. Zitto Kabwe yupo na CHADEMA walinywea baada ya kuwachimba mkwara kuwa atakayemuua, hatabaki hata sisimizi nyumbani kwake.



7. KUENDESHA MAFUNZO MSITUNI NA KUGAWA VYETI

CHADEMA waliendesha mafunzo msituni Novemba hadi Desemba 2016 kipindi alichopotea Ben Saanane. Aidha, Katibu Mkuu wa CHADEMA anaonekana akigawa vyeti msituni na tulipohoji hapa tuliambulia matusi.

Matukio ni mengi na naamini Watanzania wengine wana kumbukumbu ya baadhi ya matukio yaliyofanywa na CHADEMA yanayoenda kinyume na misingi ya chama chao.


Kwa mazingira yaliyopo, CHADEMA hakiwezi tena kwenda sambamba na misingi ya kuanzishwa kwake na kimejiondolea uhalali wa kuwa chama cha siasa. Njia iliyo salama ni kwa CHADEMA wenyewe au Msajili wa vyama vya siasa kukivunja chama hicho ili kiundwe upya.

Nawasilisha
 
Hata mtu kujiunga nao itakuwa shida, kumbe wao wana maovu mengi hivi...

Tusio na vyama 2020 lazima tupige kura.

Naona Magufuli 2020 hiyoooooo bila ubishi.
 
Tatizo umechanganya, mengine Kama vile yana ukweli na mengine ni uongo mtupu. Chambua ubakize ya ukweli tu.
 
Kwenye neno CHADEMA weka CCM!! naona umeamua kutoa uozo wa ccm kijanja!! ungeandika tu ni uozo wa ccm hutajulikana kwani mkuu max ameapa kutulinda na id zetu!
 
Mbona hicho chama kiliisha jifia siku nyingi?. Dr. Slaa aliondoka nacho kwenye briefcase na kukitupilia mbali ktk bahari ya Mediteranean
 
Njia nzuri ya kukanusha tuhuma ni kubainisha ukweli
Ukweli ni kuwa uliyoyasema yote hutendwa na serikali ya COM na wala si tuhuma, hayo yamethibitishwa mchana kweupe! i.e. Sahara la Nape, Bashe na Msukuma n.k. nikuongeze?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom