Kwa Tanzania yangu

Kwa Tanzania yangu

Chanya

Senior Member
Joined
Mar 2, 2011
Posts
133
Reaction score
22
Niamkapo asubuhi bila matumaini ya kuimaliza siku hii. Naifikiria nchi yangu ni Tanzania. Inaenda wapi? Imepotezwa mwelekeo na inaelekea bondeni,korongoni kunako umauti nimemsoma Mkwawa,Mirambo,Machemba,Mangi meri wa kibosho na kinjeketile na Tekelo walioongoza vita ya majimaji wakitaka uhuru wa taifa hili wako wapi leo hii ee Tanzania.

je viongozi wetu wanaweza kufunga mianya ya utoroshaji nyara na madini yetu kama alivyofanya Mkwawa kufungaia misafara ya waarabu kupita katika dola yake. HAPANA.

Nani ataamua kutoa uhai wake kwa watu hawa masikini wa Tanzania kama Abushiri? Je ni Nape,Mwigulu au Nchimbi?

Viongozi wamesaliti kama wabena kwa Mkwawa. Sasa tunahitaji Mkwawa na mirambo mpya wa kuongoza mapambano ya kulikomboa tena taifa hili. Vijana wenye uwezo ndio hawa wanaopokea elfu 7 kuvunja mioyo wenzao,ndio hawa wanaotungia kesi wenzao ooh Tanzania. Mbona walezi wako hawakupendi? Wanakuuza kwa wageni.,wanakukamua utajiri uliopanga kulisha wajukuu zako.

Pole Tanzania yangu ila Bado kitambo tu ukombozi unakuja ndipo wale wazee wachawi waliokua wakikupiga ndumba usiendelee watakapoanguka kwa hamaki,wale vijana wazembe waliokua wakikwamisha usitoke utumwani watakoanguka mbele zao.

Na wale masikini waliokua wakionewa wataruka kwa furaha wakifurahi mavuno mapya maana wezi na majangiri watakua wamefunikwa udongoni kurutubisha ukombozi wako.

Nakuaga Tanzania kwani ninaenda kutafuta rizki ila usilie kwani si vijana wote tuliokusaliti wapo kundi kubwa walio tayari kuweka mkono wao katika ukombozi wako poor Tz.

If we must die. Let us die fighting for you beloved Tz. See you later.
 
Back
Top Bottom