Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,703
- 4,697
Ndugu wa-TZ wenzangu, watu wamekuwa wakishangiliwa kutokana na umaarufu wao. Hii siyo tabia iliyoanza awamu ya nne, ni tangu awamu ya pili. Wakati wa mzee rukhsa tuliposhuhudia maeneo ya wazi ktk jiji la Dar yakivamiwa na kujengwa majumba ya kuishi au vituo vya mafuta na hata nyumba za ibada. Viwanja vya shule vilivamiwa kwa mtindo huo huo bila hata serikali kuzuia hali kama hiyo. Kwa ufupi waliokuwa wakiendesha vitendo hivyo ni watu ambao ktk jiji hili la Dar, wanaeleweka kama watu maarufu.
Watu maarufu ktk nchi yetu ni wale wanaofanya vitendo vya hovyo na kwa kiasi kikubwa wakiungwa mkono na wanasiasa waovu. Hiyo ndiyo hali iliyotufikisha hapa tulipo kiasi kwamba kila anayeitwa ni maarufu ni katika kundi la wezi, malaya au wauza mihadarati.
Tanzania hatuna mgunduzi maarufu, au mjenga hoja kama tuonavyo akina P.L.O. Lumumba hapo Kenya. Hatuna tena mwandishi maarufu wa vitabu kama walivyo akina Soyinka au Ngugi wa hapo Kenya. Magazeti maarufu ni yale yanayoandika juu ya umalaya au kutumia picha zao kama biashara. Haya yote ni kwa sababu baadhi ya wanaoendesha jamii, wanasiasa, wameamua kuwa ni watu wa hovyo; ni malaya, ni wezi, ni wauza madawa.
Ukisema hayo wanakuuliza una ushahidi? Lakini ni aibu nchi nzima kumfahamu binti kwa sababu tu anaonekana kila siku ukurasa wa juu wa gazeti. Akikamatwa Afrika kusini kwa madawa, kiongozi wa serikali anafuatilia kumuokoa, ikiwa ishara kwamba wanafahamiana kwa wizi, umalaya au kuuza madawa hayo.
Mmoja wetu aliyejulikana kwa jina la mama Terry aliwahi kuhusisha umalaya unaoendeshwa dodoma na kuwepo kwa Bunge. Akatishiwa na kutaka kuhukumiwa kwa hilo. Lakini, huo ndo ukweli! Tuna watu wasiofaa ktk jamii ambao tumewapa nafasi ya kutulinda ktk jamii na wanadai wawe ni mfano wa kuingwa na waitwe waheshimiwa! Nchi inahitaji kubadilika kwa nguvu yoyote ile. Haitoshi kuwafukuza watumishi waovu, hata wanasiasa wenye upuuzi huu waondolewe kabisa ktk majukwaa ili ifahamike kwamba wao siyo mfano wa kuigwa.
Naomba tuchangie tumpe rais uelekeo wa kunyoosha nchi badala ya kutetea watu tuliodhani ni maarufu.