Kwa tabia hizi wanawake wengi huwatengenezea wadada wa kazi mazingira ya kuvuruga ndoa zao bila wao kujua

moyafricatz

JF-Expert Member
Nov 27, 2015
2,900
4,865
Kwa kukaa kama Sanamu.

MUME: darl ninakikao mkoani kesho naomba niandalie vitu plz

MKE: dada zile nguo za baba pmj na soksi ulifua?

DADA: ndio nimepanga kabatini.

(Mama anarudi chumbani na
kumuomba hubby wakacheki TV
sebulen,, lakn baada ya muda mama anamuita dada akapange suruali kadhaa na mashati kwa ajili ya safari ya kesho,,

dada anapanga kila kitu anatoka.)

MKE: kama tayari hakikisha unarekebisha yale mashuka pale kitandan weka na maji bafuni.
(Dada anafanya na kwenda zake

kulala,, asubuhi dada anaamka
mapema na kuandaa kila kitu
ikiwamo na chai,, baba anakunywa chai na kutaka kuondoka.)
MKE: dada msindikize baba ili ufunge geti sababu bado ni giza

DADA: sawa mama.
(Dada anatoka na begi la baba hadi nje kwavile mkewe yupo ndani,, baba anamtaka dada abaki vizuri na watoto,, dada anaitika na kusema nawao wanamuombea safari njema.
Baada ya muda baba anarudi toka safari.)

MKE: (huku akitabasam) dada si umemuona baba amerudi vipi chakula tayari?

DADA: ndio.

MKE: haya kapange meza vizuri mimi nandaa juice.

(Baada ya muda wanakula na baba anagundua juice sio nzuri anaamua kuiacha na kusema leo wamesahau kuweka baadhi ya vitu hivyo hataweza kuinywa. Baadae baba anakumbuka kuwa aliacha boxer zake kwenye ndoo ya maji chumban na kufunika mfuniko, anamuuliza mama vipi zile nguo zangu kwenye
ndoo zilifuliwa? Maana nilisahau
kusema kama zina maji.)

MKE: (dada njoo hapa) hivi zile nguo za baba chumbani ulifua?

DADA: ndio mama
(lakin hasemi kama alianua na kuweka chumbani kwake akidhan atakunja baada ya kazi
kupungua)

MKE: darling zilifuliwa.

MUME: na watoto vipi wameshalala?

MKE: anajibu wamelala darl.

MUME: vipi dereva wao alifika kuchukua pesa yake?

MKE: dada eti uncle Hassan amechukua pesa yake?

DADA: hapana wamembadilishia gari uncle Hassan amesafiri kwa muda.

MKE: tutampatia darl siku akirudi acha dada aendelee kuitunza

MUME: basi vizuri, ehee vipi na tution walienda leo?

MKE: ndio walienda
(anamgeukia dada, si eti ee walienda si eti)

DADA: hapana Kelvin anaumwa leo siku ya pili nilinunua dawa dukan nimempa lkn hajambo.

MKE: (anashangaa) heeE! mtoto mgumu huyu kumbe jana alikua
mgonjwa halafu wala!!! alikua anacheza tu jamani watoto!! Asante dada umefanya vizuri!!

MUME: haya mimi niwaache nataka nikapumzike lkn darl nitaomba zile boxer nichome kabla ya kulala sababu zimeanza kuchoka!
(mke anaingia chumbani anafungua kabati na kuzikosa lkn kabla hajajieleza anamuona dada analeta mzigo wa boxer zikiwemo chupi za mama na mataulo)

MUME: basi dada zirudishe tutachambua kesho nenda kafanye kazi zako.

(mume anainuka na kuelekea kulala, lkn anagundua mke wake alimwaga nguo
itandan wkt anatafuta boxer hivyo anaamua kurudi sebuleni ili aombe kuandaliwa kitanda,,
kwavile chumba cha dada kipo jiran na chao anagundua dada ameacha mlango wazi,, anaamua kuufunga ili mbu wasiingie lkn anaona baadhi ya mashati na suruali zake zikiwa zimenyooshwa na kuwekwa pemben huku kitanda kikiwa kimetandikwa kwa ustadi anaamua kufunga mlango na kutoka,, anafika sebuleni anakuta mama anatazama tamthilia anamwambia akatandike kitanda.)

MKE: dada njoo... (kwa sauti ya kunong'ona) naomba ukatandike
kitanda haraka

DADA: tayari nilipeleka viatu vya baba nikaamua kutoa na zile nguo
(mke anaamka na kwenda kuhakikisha anarudi na kumwambia mumewe tayari aende akalale...
mume anaenda kulala lkn huku akijuiliza sana ni nini amfanyie huyu dada kwa ukarimu anaowafanyia hapo nyumban,,
kwanza anajua ni vitu gani baba anabeba akiwa safarini,,

ndio pekee anaemtakia safari njema na kumuombea,,

ndio anaefua boxer zake na kutunza vizuri,,

ndio anaepika chakula kitamu,,

ndio anaetandika kitanda chake,,

ndio anaejua juice gani baba anapenda,,

ndio anaejua kama watoto wamerudi vipi kutoka shule,,

vilevile ndio anaejua kama watoto wake wanaumwa ama vipi....)

Sasa Unafikiri baba atamzawadia nini huyu binti.. ???

Na mama amebakisha kumfundisha nini dada ili kesho asimsumbue tena mume wake ambae kila kitu lzm amuulize dada...?????

tunajifunza nini!!

wanawake wengi huwatengenezea wadada wa kazi mazingira ya kuvuruga ndoa zao bila wao kujua...
sambaza ujumbe huu kwa wanandoa wote na wanaojiandaa kuoa na kuolewa...
 
Wake zetu huwa wanadhani tuliwaoa ili waje kututimzia haja zetu za mwili na kutuletea kero.

Wanawake mjue kuwa ngono hata makahaba wanazo.
Unatakiwa kuwa na zaidi ya offer ya ngono
Yaani Kuna mke mtu akiwa naye hata hamu inamuisha.
Na nyie wamama fundisheni mabinti zenu kuwa mama wa familia sio wagawa ngono.
Unakutana na mdada
Kupika hajui
Kufua hajui
Hata nguo zake za ndani anafua hg
Kauli ya mdomoni chafuuuu!!
Haya, kazi anafanya hakuna hata anachopelekea familia zaidi ya kufunga katani kichwani.
 
Lakini hata sisi wanaume tunatakiwa kujifunza kitu hapa kiuhalisia wanawake waliumbwa ni wategemezi na wasaidizi kwa wanaume na sisi wanaume ndo tuliambiwa tule kwa jasho letu bali wao hawakuambiwa hivyo kwa maana kwamba sisi wanaume ndo tunatakiwa kutafuta pesa na kuwahudumia wake zetu pamoja na watoto wetu na familia kwa ujumla

Sasa shida inakuja hapa siku hizi dunia imebadilika sana yaani wanaume tumefikia hatua ya kutaka wanawake watusaidie majukumu yetu sawa kwa sawa yaani eti nao watafute pesa ili wajihudumie na watusaidie kutuhudumia sisi pamoja na watoto na familia kwa ujumla na imeshaanza kuonekana ni kawaida wanawake kufanya hivyo

Sasa kinachoshangaza ni kwamba mbona sisi hatutaki kubeba majukumu yao ya kupika kufua kuosha vyombo kufanya usafi kumtunza mume na kulea watoto na ikaonekana ni kawaida sisi wanaume kuyafanya yaani bado tumeng'ang'ania kuwa hayo ni majukumu yao na siyo yetu wakati ya kwetu wao wanayafanya

Kwahiyo hapo ni kama tunawatwisha mizigo tu na watakuwa wanafanya zaidi yetu maana sisi tutafute hela na kuhudumia familia tu ila wao watafute hela wahudumie famili walee watoto na bado wafanye kazi za ndani sasa hapo nani atakuwa na majukumu mengi? Ukiniambia eti wapo wanawake wanaofanya hivyo na mimi nitakwambia pia wapo wanaume wanaofanya hivyo na kumbuka kuwa wanawake wengi wanaofanya hivyo siyo kwamba wanapenda ila wanafanya tu sababu wanaogopa kuachika lakini kuhalisia wanabebeshwa majukumu mengi yasiyo yao na wanaume ni kama hatujali hilo
At least umetutetea muda mwingine tunachoka hatufanyi makusud mtuvumilie
 
Back
Top Bottom