Kwa suala la Pierre Liquid, Makonda unastahili pongezi

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,408
Nimesoma kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mweshimiwa mkuu wa mkoa alionekana kukerwa na tabia inayoibuka kwenye jamii yetu ya kuwaibua watu wa ajabu na kuwapatia umaarufu mkubwa kwenye jamii na watu hawa kutumika kama "brand" kufanya promosheni mbalimbali.

Wana jamii wanaweza kutofautiana katika hili kutokana na kila mmoja ana fikra zake na mtizamo wake juu ya "ni kwa jinsi gani kila jambo linastahili kushughulikiwa kwenye jamii"

Binafsi nimefurahishwa na msimamo wa RC kama alivyoeleza kuwa kama tutaanza kuchukua watu wa ovyo na kuwafanya brand, je jamii yetu tunaipeleka wapi?

Jamii yoyote inajengwa na elimu na elimu hii imekaa katika makundi mawili. kuna elimu rasmi inayoteolewa madarasani na kuna elimu isiyorasmi inayopatikana katika mazingira yanayotuzunguka.

Elimu isiyo rasmi ina nguvu sana na hii ndiyo inayosababisha jamii fulani wakawa na ustadi katika jambo fulani liwe ni jambo chanya au hasi. mfano wachaga kusifika kwa biashara, hakuna sehemu utakuta darasa rasmi linalofundisha wachaga kuwa wafanyabiashara au kukuta kwenye mila za wachaga ukute zikizungumzia biashara bali inaonekana kulitokea by chance miaka hiyo katika jamii ya wachaga wakatokea ma brand ambao walifanikiwa kupitia biashara na jamii iliyokuwa ikiwazunguka ikaiga kutoka kwao. kila walipokuwa wakiiga wachache, wakifanikiwa basi na wao wanakuwa ma brand ya kuwaonyesha wachaga wengine na wengi zaidi wakazidi kuiga na jamii ikawa na wafanya biashara mahiri wengi.

Bado tukibaki kwa wachaga hawahawa, kwa sasa tunasikia rombo vijana wengi wametumbukia kwenye ulevi wa kupindukia na kwa sasa wanapuuzia mambo mengi ya shughuli za maendeleo. mtindo utakuwa ni ule ule kwa kutokea watu wakafanya unywaji pombe zisizo na kipimo kuwa ndio sifa na vijana wakaiga mpaka jamii nzima unywaji umekuwa tatizo.

Katika ulimwengu huu wa utandawazi ambapo habari zinawafikia wananchi kwa wepesi sana popote walipo ndani ya mda mfupi, elimu isiyo rasmi nayo inapata nguvu kupitia utandawazi.

Ni vema tukumbuke kwenye jamii yetu tuna watoto ambao hawa wanajifunza kutoka kwa wazazi, walezi, walimu na jamii inayowazunguka lakini pia kuna vijana ambao wanajifunza kwa kuiga zaidi kuliko kusikiliza wazazi na walimu.

Vijana hawa akimuona Joti kanyoa kiduku ni vigumu mzazi, mlezi au mwalimu kumzuia kunyoa kiduku.

Utandawazi ukitumika vizuri utaijenga jamii yetu na ukitumika vibaya utabomoa jamii yetu.

Nguvu ya utandawazi kujenga au kuharibu jamii yetu ni kupitia elimu isiyo rasmi inayopitia kwenye mitandao.

mathalani watu maarufu wanaotumika katika mitandao ya kijamii hufanya kazi mbili. moja ni ile kazi rasmi wanayopewa kuitangaza kupitia mitandao lakini pia watu hawa hufanya kazi isiyo rasmi kwani maisha yao binafsi huigwa na vijana ambao huwatumia kama kioo cha kujitazama.

Leo hii joti kama mtu maarufu anapotumiwa na makampuni mbalimbali kutangaza bidhaa za makampuni vijana wengi wanatokea kuiga yale anayoyafanya joti. vijana wakipata fursa ya kujua joti alianzia wapi akapambana na amefikia wapi leo hii basi inawapapia hamasa ya kupambana.

Jamii inapomchukua mtu ambaye sifa yake ni kunywa pombe na yeye akijigamba na mitandao ikimsifia kwa unywaji pombe na kuwa unywaji pombe ndio unampatia fursa na kumtoa kimaisha tunatafuta vijana ambao bado hawaoni mwanga bali wao wanajifunza kwa mastaa wanaowaona wajifunze nini?

Nahisi wizara inayohusika na utamaduni na michezi inatakiwa kutunga miongozo ya watu wa aina hii ili sifa hasi zichukuliwe kama background kwenye matangazo mengine na kuiharibu jamii yetu
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
IMG_20190401_114054.jpeg
IMG_20190401_114057.jpeg
IMG_20190401_113732.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: rr4
Jiulize yeye aliibuka kivipi kwanza, historia ni kitu cha ajabu sana.
 
  • Thanks
Reactions: rr4
Hongera mtoa mada japo akili yako inachakata vitu taratibu mno.

Makonda has been right since day one alipoteuliwa. Mengine ni mapungufu ya kibinadamu
 
Hata mimi nashangaa jamii tuliyonayo ya kukumbatia vitu vya ovyo, hata rc mwenyewe ni zao la vitu vya ovyo kwa sababu ya kukumbatiwa na jamii hii hii

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hata kama komedian kuna vitu tuwe serious unampa promo mtu kama huyo watoto wetu wanajifunza Nini na ndio maana ukifungua mitandao utaona akina lokole na wenzie wapo bize na ushoga wao hii ndio tz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makonda yuko sahihi tatizo ni namna ya kuwasilisha hoja na muda aliouwasilisha.

Pia kwenye kadamnasi kama ile kumtaja mhusika moja moja wakati yupo pale pale kuwa ni mtu wa hovyo haikuwa busara.

Mfano angesema tu kuwa media ziwape kipaumbele watu wanaoleta impact kwenye jamii, kisha angeishia hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi yule ni comedian au mlevi, namuunga mkono Makonda kwa hili japokuwa lugha aliyo tumia sio sahihi.
 
Vipi kuhusu aliyeagiza pombe zishushwe bei hakumaanisha watu walewe?
 
comedians wapo kila nchi na wala sio watu wa ajabu,ndiyo maana ukraine hivi sasa comedian anaongoza kwenye uchaguzi wa rais,acha kuongea vitu usivyovijua

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani tunashindwa kuelewana, hoja hapa sio kuwa commedian bali hoja hapa ni background information gani anabeba? Piere kama piere hakuna mwenye pingamizi naye bali anabeba background meseji gani?

Tatizo hapa ni " kuwa mlevi na ulevi wake kuonekana ndio unaompa dili"

haya maneno yanasemwa kila mara kwenye promosheni zake.
 
Mtoa mada una hoja thabiti ila nikuulize swali | ulevi ni illegal hapa Tanzania, basi kama sii illegal kwanini useme no background mbaya, uwoni kwa promo ya mtu kama mzee was liquid anachangia watu kuwa walevi hivyo mapato ya makampuni ya pombe yanaonhezeka then kodi kuongezeka.

Je kuna tatizo hapo, kama lipo basi kuanzia leo tupitishe kuwa pombe is illegal Tanzania.

Tatizo sio illegal au vinginevyo.
Tatizo media zipo kwa interest zao binafsi kutafuta trend YouTube na viwers na subscribe so wanajikuta wanabase kwenye vitu visivyo vya maana ili kutengeneza attention na vitu kma hvo.
Mimi na blame sana hizi online TV hazipo kwa ajili ya kujenga wao ni biashara tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mweshimiwa mkuu wa mkoa alionekana kukerwa na tabia inayoibuka kwenye jamii yetu ya kuwaibua watu wa ajabu na kuwapatia umaarufu mkubwa kwenye jamii na watu hawa kutumika kama "brand" kufanya promosheni mbalimbali.

Wana jamii wanaweza kutofautiana katika hili kutokana na kila mmoja ana fikra zake na mtizamo wake juu ya "ni kwa jinsi gani kila jambo linastahili kushughulikiwa kwenye jamii"

Binafsi nimefurahishwa na msimamo wa RC kama alivyoeleza kuwa kama tutaanza kuchukua watu wa ovyo na kuwafanya brand, je jamii yetu tunaipeleka wapi?

Jamii yoyote inajengwa na elimu na elimu hii imekaa katika makundi mawili. kuna elimu rasmi inayoteolewa madarasani na kuna elimu isiyorasmi inayopatikana katika mazingira yanayotuzunguka.

Elimu isiyo rasmi ina nguvu sana na hii ndiyo inayosababisha jamii fulani wakawa na ustadi katika jambo fulani liwe ni jambo chanya au hasi. mfano wachaga kusifika kwa biashara, hakuna sehemu utakuta darasa rasmi linalofundisha wachaga kuwa wafanyabiashara au kukuta kwenye mila za wachaga ukute zikizungumzia biashara bali inaonekana kulitokea by chance miaka hiyo katika jamii ya wachaga wakatokea ma brand ambao walifanikiwa kupitia biashara na jamii iliyokuwa ikiwazunguka ikaiga kutoka kwao. kila walipokuwa wakiiga wachache, wakifanikiwa basi na wao wanakuwa ma brand ya kuwaonyesha wachaga wengine na wengi zaidi wakazidi kuiga na jamii ikawa na wafanya biashara mahiri wengi.

Bado tukibaki kwa wachaga hawahawa, kwa sasa tunasikia rombo vijana wengi wametumbukia kwenye ulevi wa kupindukia na kwa sasa wanapuuzia mambo mengi ya shughuli za maendeleo. mtindo utakuwa ni ule ule kwa kutokea watu wakafanya unywaji pombe zisizo na kipimo kuwa ndio sifa na vijana wakaiga mpaka jamii nzima unywaji umekuwa tatizo.

Katika ulimwengu huu wa utandawazi ambapo habari zinawafikia wananchi kwa wepesi sana popote walipo ndani ya mda mfupi, elimu isiyo rasmi nayo inapata nguvu kupitia utandawazi.

Ni vema tukumbuke kwenye jamii yetu tuna watoto ambao hawa wanajifunza kutoka kwa wazazi, walezi, walimu na jamii inayowazunguka lakini pia kuna vijana ambao wanajifunza kwa kuiga zaidi kuliko kusikiliza wazazi na walimu.

Vijana hawa akimuona Joti kanyoa kiduku ni vigumu mzazi, mlezi au mwalimu kumzuia kunyoa kiduku.

Utandawazi ukitumika vizuri utaijenga jamii yetu na ukitumika vibaya utabomoa jamii yetu.

Nguvu ya utandawazi kujenga au kuharibu jamii yetu ni kupitia elimu isiyo rasmi inayopitia kwenye mitandao.

mathalani watu maarufu wanaotumika katika mitandao ya kijamii hufanya kazi mbili. moja ni ile kazi rasmi wanayopewa kuitangaza kupitia mitandao lakini pia watu hawa hufanya kazi isiyo rasmi kwani maisha yao binafsi huigwa na vijana ambao huwatumia kama kioo cha kujitazama.

Leo hii joti kama mtu maarufu anapotumiwa na makampuni mbalimbali kutangaza bidhaa za makampuni vijana wengi wanatokea kuiga yale anayoyafanya joti. vijana wakipata fursa ya kujua joti alianzia wapi akapambana na amefikia wapi leo hii basi inawapapia hamasa ya kupambana.

Jamii inapomchukua mtu ambaye sifa yake ni kunywa pombe na yeye akijigamba na mitandao ikimsifia kwa unywaji pombe na kuwa unywaji pombe ndio unampatia fursa na kumtoa kimaisha tunatafuta vijana ambao bado hawaoni mwanga bali wao wanajifunza kwa mastaa wanaowaona wajifunze nini?

Nahisi wizara inayohusika na utamaduni na michezi inatakiwa kutunga miongozo ya watu wa aina hii ili sifa hasi zichukuliwe kama background kwenye matangazo mengine na kuiharibu jamii yetu
Naona umemtolea sna mfano joti kwa hiyo na wewe ukamkuta mwanao wa kiume anaigiza kama shoga au mwaamke mapepe utafurahia kwa kuwa ni brand yake ? So watoto wa kiume wajifunze kuwa wanawake sio
 
Back
Top Bottom