Kwa staili hii ya CCM kweli tutafika?

Kwa staili hii ya CCM kweli tutafika?

TEKNOLOJIA

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2014
Posts
4,305
Reaction score
2,563
Taifa letu la Tanzania hivi sasa lipo kwenye kipindi kigumu lakini muhimu cha kutengeneza mustakabali wake upya kupitia RASIMU ya Katiba mpya inayojadiliwa Bungeni ili hatimaye ije kuwa Katiba rasmi ya nchi. Rasimu ya Katiba ya Tume ya Jaji Warioba ina mambo mazuri sana ndani yake,Mambo ambayo yanatoa matumaini kwamba sasa taifa hili linaelekea kwenye njia iliyo sahihi kabisa kimaendeleo.Miongoni mwa mambo yanayovutia ndani ya rasimu ya Katiba mpya ni uwepo wa TUNU za taifa kama vile;Uadilifu na Uwazi (Vipengele hivi vimefutwa na wajumbe wa Katiba wanaotokea CCM)

1) Uadilifu-Kilikuwa ni kipengele muhimu sana kuwepo ndani ya Katiba mpya ijayo hasa kwa wakati huu ambao taifa limejawa na wanasiasa wasiokuwa waadilifu. Kipengele cha maadili kilikuwa kinawabana wanasiasa wote waliokuwa na matatizo ya kimaadili huko nyuma wasiweze kupata nafasi za uongozi za ngazi yoyote ile ndani ya nchi.Kwa mfano,Kuna baadhi ya wanasiasa walikumbwa na kashfa mbalimbali za ufisadi nchini kama vile EPA,KAGODA,MEREMETA,RADA,nk.Ha wa wote chini ya kipengele cha maadili walikuwa wameshapoteza sifa za kugombea nafasi yoyote ya ile uongozi hapa Tanzania.Lakini kwasababu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa si Chama kinachopigania maslahi ya nchi tena bali ni ngazi inayotumiwa watu flani wenye tamaa ya madaraka na utajiri wa haraka kupanda kwenda kuvuna utajiri huo kwa manufaa yao binafsi kimeamua kukichomoa kipengele hicho kisiwemo kwenye Katiba mpya ijayo.Watu hawa wenye nguvu ya kifedha na ushawishi wa kisiasa ambao wamekiteka nyara Chama Cha Mapinduzi wameshaanza kampeni ya kukiondoa kifungu hiki cha maadili kwani kwao kinaonekana kuwa kizingiti kikubwa katika harakati zao kulihujumu hili taifa.

2) Uwazi-Kama kilivyokuwa kipengele cha maadili,Uwazi nao ni kipengele muhimu sana kinachofaa kuwemo ndani ya Katiba mpya ijayo (Hata hivyo nacho kimeng'olewa na WanaCCM) kwasababu kitaziba mianya ya Mikataba ya ajabu ajabu inayosainiwa na viongozi wa nchi ambayo huishia kuliingizia taifa hasara.Chini ya kipengele cha uwazi,Mikataba mingi ambayo serikali inasaini ingepaswa kupelekwa Bungeni kwa mijadala ya kina zaidi,Hii ingesaidia kudhibiti madudu yanayofanywa na serikali wakati wanaingia mikataba na Mataifa mengine au Makampuni ya kigeni.Uwazi usingeishia tu kwenye kuweka mikataba mbalimbali inayoingiwa na serikali hadharani bali ungejielekeza hadi kwa Waandishi wa habari ambao chini ya kifungu hiki wangeweza kupekuwa habari za ndani kabisa za viongozi na kuzianika hadharani ili umma wa Watanzania ufahamu kinachoendelea ndani ya nchi yao.

Chini ya utaratibu wa sasa waandishi wa habari wakiripoti habari za kichunguzi kwenye vyombo vya habari wanafunguliwa mashtaka sambamba na kuitwa wachochezi na watawala,Na hata baadhi ya vyombo vya habari kufungiwa kama ilivyokuwa kwa magazeti ya M.w.a.n.a.h.a.l.i.s.i na Mtanzania.Waandishi na Maripota wengi wanaofanya habari za kichunguzi wangeweza kulindwa na uwepo wa kipengele hiki.Si hivyo tu,Chini ya kipengele hiki vyombo vya habari vingekuwa na haki ya kikatiba ya kupata taarifa kutoka serikalini na kwenye matawi yake,Kwa kuwepo kwa kipengele hiki inamaama kwamba serikali ingekuwa inafanya shughuli zake katika mazingira ya uwazi zaidi sawa sawa na familia inayoishi kwenye nyumba ya vioo tupu ambapo watu wa nje wanaona kila kitu kinachoendelea ndani ya nyumba.

Kwasababu serikali ya CCM inachukia uwazi imewaagiza makada wake kwenye Bunge maalum la Katiba wakiondoe kipengele cha uwazi,Hii inamaanisha CCM kwa makusudi wameamua kulirudisha taifa kwenye zama za USIRI ambazo zimeligharimu taifa kiuchumi,kiusalama na kijamii. Ili taifa la Tanzania liweze kuwa kule kila mmoja wetu anatamani liwe kimaendeleo ni lazima CCM waondoke madarakani 2015,Hakuna njia.Ili CCM wang'oke madarakani ni lazima Vyama vya Upinzani viungane.
 
Kikwete kamega nchi vipande vipande kwa uroho ake wa madaraka dharau zake kwa wazee watume zitambutumbkia nyongo hawezi kuvuruga nchi kiasi hiki halafu akabaki salama
 
Warioba kalikoroga alipojipachika unabii wa nchii kwa kudai wengi wanataka serikali tatu jambo lisilotakiwa na wananchi wengi.warioba credibility yake imeshuka kutokana na twakwimu alizotoa sio credible
 
Warioba kalikoroga alipojipachika unabii wa nchii kwa kudai wengi wanataka serikali tatu jambo lisilotakiwa na wananchi wengi.warioba credibility yake imeshuka kutokana na twakwimu alizotoa sio credible

Hoja ya hapo juu haihusiani na serikali tatu bali inazungumzia kuchomolewa kwa vipengele vya UWAZI na UADILIFU kwenye Katiba mpya, Je wewe unawaunga mkono CCM kwa kuviondo vipengele hivyo kwenye TUNU ZA TAIFA?
 
Teknolojia,ni kweli tuko kwenye kipindi kigumu na kibaya nafuu hilo Bunge lingevunjwa tu,tukabaki na Katiba ya zamani,waje wajukuu na vitukuu watengeneze Katiba waitakayo.

Kimefanya hata vijana wameshindwa kujadili Rasimu ya Katiba tunaishia kulumbana kwa matusi,vijembe,dharau nk,sababu tu tunatofautiana mitazamo.Sijui kama kuna mwisho mzuri,hasa baada ya upande wa pili kutoka.

Na pia ni ukweli suiopingika kinachopingwa na wajumbe waliowengi wala si MUUNGANO bali Rasimu nzima imeongelea ukweli unaouma na namna ya kuondokana na viongozi waovu na wabaya,namshukuru Judge Warioba ameweza japo kidogo kumfunga paka kengele ili panya tusiendelee kumalizwa,lakini ndiyo hivyo yupo peke yake tulionje tumsaidie.

Kweli kabisa Muungano siyo tu chenye maana zaidi ya vipengele vingine ndani ya Katiba hiyo,lakini kwa vile viongozi wetu wengi wamepata mali isvyohalali wanaogopa kitakachowatokea kesho,na ukiangalia wanapenda kukaa madarakani mpaka siku yao ya kuingia kaburini.
 
Warioba kalikoroga alipojipachika unabii wa nchii kwa kudai wengi wanataka serikali tatu jambo lisilotakiwa na wananchi wengi.warioba credibility yake imeshuka kutokana na twakwimu alizotoa sio credible

tumia akili yako basi ,,sio kila mara lazima ufikiriwe na ccm, hivi wewe unaona yanayo fanywa na ccm katka katiba mpya? Lengo la luto uadilifu na uwazi ninini?
 
Ccm ndugu zangu insikitisha matusi yenu, kejeli zinawacanganya wananchi, kikwete alimchagua walioba kukubali kwake kuwa mweyekiti ni kosa jamani, kila mtu aiyepewa kukusanya maoni katika nchi hii ni mbaya kwenu , muongo huyu mzee wa watu mutamuu bure kama mnataka selkali mbili toeni hoja za msingi wanachi wataelewa kuliko matusi , fedheha na kejeli zenu kumshambulia walioba ni dhambi kubwa hakujipeleka mwenyewe ila kwakua zanziba wamevunja katiba na kero zingine basi tatueni muingize katika katiba mpya
 
Hatutaki tena hoja yakuwa takwimu za warioba sio sahihi wakati hata CCM wanazotaka kuingiza hazina uharali kuingizwa kwasababu hayakutolewa maoni na hawajamhiji mtanzania yeyote na akapendekeza mbili wanazoshabiakia
 
Back
Top Bottom