Kwa situation hii anaweza kupata wapi mkopo?

kindili kindili

JF-Expert Member
May 27, 2013
244
225
Wana jamvi, kuna mtu kaniuliza nimekosa majibu, hope atapata hapa.. anafanya kazi mahala fulan mshahara wake take home ni 650,000,.Ofice hy ya muhindi amezuia wafanyakazi kukopeshwa kabisa, wana pokea mishahara kupitia DTB..kwa vile kuna waliowah kuajiriwa wakakopa alafu wakaacha kazi kiajabu akapata shuruba nyingi so hataki itokee tena...sasa huyu ndugu yangu anatafuta mkopo, hana shamba wala nyumba, anaweza kukopa kwenye taasisi gani? anahitaji mkopo wa minimum mil 5...eti bandugu msaada.
 

NAMTUMBA

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
1,940
2,000
Ngumu kupata.
Benki zote ili mfanyakazi ukopeshwe lazima iingie mkataba na kampuni au mwajiri wako. Ili mkataba ukubalike lazima mwajiri au kampuni ipeleke Financial statements za miaka miwili au mitatu kwa baadhi ya benki. Kama mwajiri hataki mukopeshwe hakuna benki yoyote itakayokubali kukukopesha bila mkataba na mwajiri wako.

Kwa mshahara huo maximum amount ambayo kama angekuwa anasifa angekopeshwa ni 650,000*12= 7,800,000/= tu. Marejesho angetakiwa kurejesha ndani ya miezi 36 hadi 60 kwa baadhi ya benki.

Ushauri wangu ajaribu kukopa kwa ndugu au marafiki lakini kwa benki hakopesheki, hana sifa. Otherwise ajichange mdogomdogo mpaka kieleweke.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom