Kwa Serikali hii Lissu hawezekani

Aug 29, 2017
90
150
Nimebaki mtazamaji wa suala hili kwa muda mrefu nikijaribu kupata mdhahania wa hoja za pande zote mbili, Lissu upande mmoja na serikali upande mwingine.

Tutakubaliana kwamba Lissu ni kati ya watanzania wachache waliobaki wenye uwezo wa kujenga hoja na kueleweka. Lissu ana kipaji cha kutumia ubongo wake kuchekecha na kufikia hitimisho juu ya hoja aina aina na mara zote hufanikiwa kuzitetea, awe sahihi au amekosea.

Kaliba ya aina hii imepatwa kumilikiwa na watanzania wachache tu, mmoja ambaye atakumbukwa kwa wepesi ni baba wa taifa ingawa kiukweli Lissu bado anasafari ndefu kufikia kiwango hiki.

Ziara anayoendelea nayo huko ughaibuni kuelezea mkasa mbaya uliompata Septemba 7 mwaka juzi imeibua watu wengi upande wa serikali wanaojitosa kujibu kufukia ombwe linalokuwa limeachwa na mjibuji aliyetangulia.

Kwa uchache watu hawa ni Sirro, Kangi Lugola, Dr. Bashiru Ally, Humphrey Polepole, Balozi Abdallah Possi, Balozi Wilson Masilingi, Kibajaji, Msukuma, Makonda na hivi karibuni DC wa Kigamboni Lucy Msafiri.

Majibu ya timu hii yamekuwa yanaacha maswali mengi kuliko majibu ndani yake. Katika namna yoyote ile hakuna hata mmoja aliyeweza kujibu aghalabu moja ya kumi ya hoja za Lissu lakini wamebaki kuivua nguo serikali kwa majibu yao yasiyo ya kidiplomadia wala kisheria.

Kuna baadhi ya sehemu ukivulia nguo inabidi uchutame hasa kama sehemu hii ni mbeke ya hadhara, kwa hili serikali ya awamu ya tano imechemka, ikubali kushindwa.

Cha kufanya ni kukaa kimya au kuagiza upelelezi makini utakaoisafisha serikali mbele ya wananchi wake na hata jumuia ya kimataifa.

Serikali inayonuka damu haipaswi kuwepo karne hii ya ishirini na moja.
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
19,864
2,000
Wazee wetu wa zamani walisema tauro likichonjoka tafadhali chutama haraka kulinda heshima; Yaani hutakuwa na namna nyingine yoyote ile zaidi ya kuchutama.
 
Richard irakunda

JF-Expert Member
Oct 23, 2018
3,512
2,000
Mwenye uwezo kidogo wa kupambana na lissu hii awamu ni mahiga pekee ila wengine wote ni wanamjibu ili kumfurahisha jiwe tu

Bashite yeye simlaumu maana najua ana upeo finyu

Kangi lugola nadhani yeye mwenyewe hajuagi anaongea nini

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,777
2,000
Nimebaki mtazamaji wa suala hili kwa muda mrefu nikijaribu kupata mdhahania wa hoja za pande zote mbili, Lissu upande mmoja na serikali upande mwingine.

Tutakubaliana kwamba Lissu ni kati ya watanzania wachache waliobaki wenye uwezo wa kujenga hoja na kueleweka. Lissu ana kipaji cha kutumia ubongo wake kuchekecha na kufikia hitimisho juu ya hoja aina aina na mara zote hufanikiwa kuzitetea, awe sahihi au amekosea.

Kaliba ya aina hii imepatwa kumilikiwa na watanzania wachache tu, mmoja ambaye atakumbukwa kwa wepesi ni baba wa taifa ingawa kiukweli Lissu bado anasafari ndefu kufikia kiwango hiki.

Ziara anayoendelea nayo huko ughaibuni kuelezea mkasa mbaya uliompata Septemba 7 mwaka juzi imeibua watu wengi upande wa serikali wanaojitosa kujibu kufukia ombwe linalokuwa limeachwa na mjibuji aliyetangulia.

Kwa uchache watu hawa ni Sirro, Kangi Lugola, Dr. Bashiru Ally, Humphrey Polepole, Balozi Abdallah Possi, Balozi Wilson Masilingi, Kibajaji, Msukuma, Makonda na hivi karibuni DC wa Kigamboni Lucy Msafiri.

Majibu ya timu hii yamekuwa yanaacha maswali mengi kuliko majibu ndani yake. Katika namna yoyote ile hakuna hata mmoja aliyeweza kujibu aghalabu moja ya kumi ya hoja za Lissu lakini wamebaki kuivua nguo serikali kwa majibu yao yasiyo ya kidiplomadia wala kisheria.

Kuna baadhi ya sehemu ukivulia nguo inabidi uchutame hasa kama sehemu hii ni mbeke ya hadhara, kwa hili serikali ya awamu ya tano imechemka, ikubali kushindwa.

Cha kufanya ni kukaa kimya au kuagiza upelelezi makini utakaoisafisha serikali mbele ya wananchi wake na hata jumuia ya kimataifa.

Serikali inayonuka damu haipaswi kuwepo karne hii ya ishirini na moja.
Hujamtaja musiba kwa makusudi kwa sababu najua umempuuza kama kinyesi cha fisi
 
Mbaya zaidi hii Serikali inanuka damu za watu na bado inalazimisha kupendwa na wananchi
 
PumziNdefu

JF-Expert Member
Dec 14, 2018
566
1,000

Serikali ya Majinga haijaweza kujibu hoja zake hata moja wanaropoka tu kama wapumbavu.
Kwenye hili tukio ni uchunguzi huru ndio unaohitajika, hawa wauaji hawawezi kujichunguza, tumeshaona juhudi zao katika kuondoa ushahidi (CCTV).
 
Allency

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
5,563
2,000
Mwenye uwezo kidogo wa kupambana na lissu hii awamu ni mahiga pekee ila wengine wote ni wanamjibu ili kumfurahisha jiwe tu

Bashite yeye simlaumu maana najua ana upeo finyu

Kangi lugola nadhani yeye mwenyewe hajuagi anaongea nini

Sent using my iPhone using jamiiforum app
Nimecheka sana juu ya Bashite, hivi huwa anajua kuwa yeye ni hamnazo au hata hilo halijui pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyanjomigire

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
6,580
2,000
Serikali hii kamwe haitaweza kujisafisha kutokana na hii kadhia. Naunga mkono uchunguzi huru (Independent Probe) ili angalau ku-restore the government's dented image.

Wakijidanganya kutaka kuwatumia akina Robert Boaz ktk uchunguzi ili kufanya cover up ndio watakuwa wamejimaliza kabisa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom