Kwa sababu hizi 3 nitamchagua Lowasa

Kwa sababu hizi 3 nitamchagua Lowasa

brand udom

Member
Joined
Dec 19, 2014
Posts
40
Reaction score
14
Ingawa dhamira yangu inaniambia Lowasa sio msafi. Kwa nini Lowasa ni fisadi? Kelele za Chadema ndizo zilizofanya Lowasa atambulike kama fisadi rejea List of shame ambamo Kikwete na Mkapa wamo. Ila kelele za baadhi ya wanaccm wanaompinga Lowasa ndizo zilizoaminisha umma kuwa Lowasa ndiye fisadi peke yake nchini.

Mashabiki na vikundi mbalimbali vya CCM vilivyokuwa vikimuunga mkono Lowasa kabla na baada ya kumchukua fomu ya urais kupitia ccm, viliwaaminisha watu kuwa Lowasa si fisadi .

Leo hii Lowasa amehamia Chadema. Hatuwasikii tena waliokuwa wakimtuhumu kuwa ni fisadi. Kadhalika wale wa CCM waliokuwa wakimuunga mkono na kumpa sifa kedekede, leo hii nao eti wanampinga na kumwita fisadi.

Huu ni ugeugeu wa wanasiasa, wao wanasema siasa ni mchezo mchafu, mchafue mwenzio ili wew uwe safi.
Ila mimi binafsi naamini Lowasa ni fisadi anayetakiwa kuwa gerezani, kama alisingiziwa mimi sijui, Kama aliacha ufisadi mimi sijui. Lakini nitampa kura yangu maana naamini yupo kwenye mikono salama.
Kwa nini ni Lowasa?

1.Yeye ni fisadi na watu wengi wameamini kuwa ni fisadi, hivyo naamini Lowasa hawezi kwenda Ikulu ili kuthibitisha ufisadi wake, bali kuwathibitishia wabaya wake kuwa yeye ni tumaini jipya la nchi hii.

2.Lowasa anautendaji uliotukuka, kabla ya kuwa waziri mkuu na kuhusishwa na ufisadi wa Richmond hakuna mahali pengine popote alipoonekana kuwa ni fisadi, bali ulionekana utendaji wake uliotukuka kwa uchache alisimamia vizuri wizara ya mifugo kwa kujenga marambo mengi karibu nchi nzima (kwa jamii ya wafugaji), alisimamia vizuri na kuwezesha marekebisho ya sheria ya matumizi ya maji ya ziwa Victoria ambayo sasa hivi yanatumika hadi Shinyanga, alisimamia ujenz wa shule za kata kwa mafanikio na pia alitekeleza na kuisimamia ujenz wa chuo cha UDOM nk.

3.Wengi wanaompinga Lowasa ni wale walioko/waliokuwa kwenye mtiririko wa uongozi wa nchi hii, ambao kwa namna moja au nyingine wanaogopwa kugawanyika na vyombo vyote vya sheria, Ulinzi na usalama na hata takukuru (untouchables) mfano marais wastaafu. Mimi naamini kwa kuwa Lowasa hatokuwa na maslahi na watu hao akiingia Ikulu anaweza kuwafungulia kesi na kisha kuwafirisi Mali wale wote watakaobainika walitumia vibaya ofisi za umma kipindi cha uongozi wao.

NB: Kesho nitaeleza kwa nini UKAWA ni chaguo sahihi na ni mikono salama kwa mustakabali wa Taifa hili.
 
CCM ina coverage kubwa kuliko chadema hyo ni sababu tosha kushinda uchaguzi wa mwaka huu...
 
mleta mada una akili sana

avatar265011_1.gif
kana akili za kitoto haka kabrand udom
kana uhakika UDOM imejengwa na lowassa au ni akili za kushikiwa? UDOM imeanza lini hadi yeye awe asiamamie ujenzi?
alisimamia vizuri na kuwezesha marekebisho ya sheria ya matumizi ya maji ya ziwa Victoria ambayo sasa hivi yanatumika hadi Shinyanga, alisimamia ujenz wa shule za kata kwa mafanikio na pia alitekeleza na kuisimamia ujenz wa chuo cha UDOM nk.
Mkiti wa CCM mkoa wa Mwanza Di'allo anakataa huo mpango wa maji ya ziwa Victoria
vitu vingine ni ukiherehere mnataka kutuingiza kujibizana bila Data ndio maana nasema ni utoto
 
achen upumbavu ninyi bavicha kila asemalo mbowe n sawa kwenu!!! amken chama kishauzwa ninyi mazuzu
 
Lowasa angekua fisadi CCM wangekua wameshampeleka mahakamani kama walivyofanya kwa Mramba, Yona, Liyumba etc! Mi naamin ni kashfa za kumchafua tu. Ila pia kama ni lish of shame hata JK na Mkapa wangetakiwa wawe treated kama Lowasa kwa kuitwa wote mafisadi.
Mi nakuunga mkono kwamba Lowasa akipata urais atataka kuonesha wananchi yeye siyo fisadi na atachapa kazi kweli kweli. Kuna mtu kabisha kwamba maji ya Victoria kwenda shinyanga sio kaz ya Edo! Hana taarifa na uhalali wa kubisha, kibuyu huyo
 
avatar265011_1.gif
kana akili za kitoto haka kabrand udom
kana uhakika UDOM imejengwa na lowassa au ni akili za kushikiwa? UDOM imeanza lini hadi yeye awe asiamamie ujenzi?

Mkiti wa CCM mkoa wa Mwanza Di'allo anakataa huo mpango wa maji ya ziwa Victoria
vitu vingine ni ukiherehere mnataka kutuingiza kujibizana bila Data ndio maana nasema ni utoto

udom imeanza kutoa shahada mwaka 2007,,,kwa mantiki hiyo mchakato wa ujenzi umeplaniwa lowasa akiwa waziri mkuu, na mie nimeanza masomo hapo mwaka 2009, ukiwa ni mwaka wa pili wa masomo kwa udom
 
Ingawa dhamira yangu inaniambia Lowasa sio msafi. Kwa nini Lowasa ni fisadi? Kelele za Chadema ndizo zilizofanya Lowasa atambulike kama fisadi rejea List of shame ambamo Kikwete na Mkapa wamo. Ila kelele za baadhi ya wanaccm wanaompinga Lowasa ndizo zilizoaminisha umma kuwa Lowasa ndiye fisadi peke yake nchini.
Mashabiki na vikundi mbalimbali vya CCM vilivyokuwa vikimuunga mkono Lowasa kabla na baada ya kumchukua fomu ya urais kupitia ccm, viliwaaminisha watu kuwa Lowasa si fisadi .
Leo hii Lowasa amehamia Chadema. Hatuwasikii tena waliokuwa wakimtuhumu kuwa ni fisadi. Kadhalika wale wa CCM waliokuwa wakimuunga mkono na kumpa sifa kedekede, leo hii nao eti wanampinga na kumwita fisadi.
Huu ni ugeugeu wa wanasiasa, wao wanasema siasa ni mchezo mchafu, mchafue mwenzio ili wew uwe safi.
Ila mimi binafsi naamini Lowasa ni fisadi anayetakiwa kuwa gerezani, kama alisingiziwa mimi sijui, Kama aliacha ufisadi mimi sijui. Lakini nitampa kura yangu maana naamini yupo kwenye mikono salama.
Kwa nini ni Lowasa?
1.Yeye ni fisadi na watu wengi wameamini kuwa ni fisadi, hivyo naamini Lowasa hawezi kwenda Ikulu ili kuthibitisha ufisadi wake, bali kuwathibitishia wabaya wake kuwa yeye ni tumaini jipya la nchi hii.
2.Lowasa anautendaji uliotukuka, kabla ya kuwa waziri mkuu na kuhusishwa na ufisadi wa Richmond hakuna mahali pengine popote alipoonekana kuwa ni fisadi, bali ulionekana utendaji wake uliotukuka kwa uchache alisimamia vizuri wizara ya mifugo kwa kujenga marambo mengi karibu nchi nzima (kwa jamii ya wafugaji), alisimamia vizuri na kuwezesha marekebisho ya sheria ya matumizi ya maji ya ziwa Victoria ambayo sasa hivi yanatumika hadi Shinyanga, alisimamia ujenz wa shule za kata kwa mafanikio na pia alitekeleza na kuisimamia ujenz wa chuo cha UDOM nk.
3.Wengi wanaompinga Lowasa ni wale walioko/waliokuwa kwenye mtiririko wa uongozi wa nchi hii, ambao kwa namna moja au nyingine wanaogopwa kugawanyika na vyombo vyote vya sheria, Ulinzi na usalama na hata takukuru (untouchables) mfano marais wastaafu. Mimi naamini kwa kuwa Lowasa hatokuwa na maslahi na watu hao akiingia Ikulu anaweza kuwafungulia kesi na kisha kuwafirisi Mali wale wote watakaobainika walitumia vibaya ofisi za umma kipindi cha uongozi wao.

NB: Kesho nitaeleza kwa nini UKAWA ni chaguo sahihi na ni mikono salama kwa mustakabali wa Taifa hili.

ANGALIZO KWA DR SLAA NA LOWASA
Kabla sijaanza kuelezea lolote napenda kumukumbusha Slaa ambaye ana taalum ya upadri.
Katika kitabu cha matendo ya Mitume kuna ushahidi kwa Sauli alikuwa muuaji na tena alikuwa anauwa mitume lakini alipata padiliko la kweli na kujiunga na mitume wengine.

Wakati Sauli anafanya hivyo Mitume wengine walianza kumunyanyapaa na kumuogopa lakini katika bibilia , imethibitishwa kwamba hadi leo Paulo (aliyekuwa Sauli) ndiye aliyefanya kazi kuliko Mitume wote.

Bila shaka kuna watu ndani ya Chadema na hata nje ya chadema wanataka kujenga hoja ya kumunyanyapa LOWASA ati ni Fisadi , hata mimi niliingia mtego huu lakini napenda kuhojhi yafuatayo:
(1)Lowasa amehama CCM na kwa hatua hiyo ameingamiza nafsi yake kwa kiwango Kikubwa.
(2)Lowasa yupo tayari kutumia Pesa yake na mali yake kubomoa CCM
(3)LOWASA anahasira kali na CCM na miungu watu ndani ya CCM
(4)LOWASA kama waziri Mkuu mstafu ametake risk ya Kifo kiasi kwamba anataka kupiga CCM kwa Nyaraka zito za Siri ambazo Slaa hawezi kuzielezea
(5) Lowasa anajua mikakati ya Wizi wa Kura ndani ya CCM kwa miakazaidi ya 40
(6) Ndani ya CCM hawakutarajia wala hawakuwahi kupanga kuwa mtu kama Lowasa ambaye amewshijka nafasi nyeti kama waziri mkuu anaweza kuasi serikali kiasi hiki
Huu uasi unatisha na haujawahi kutokea, na hata pale ulipojaribu kutokea wahusika hawakubaki hai
(7)Kwa sasa CCM wanahaha sana juu ya Lowasa kuchukua form. Mikakati ya CCM iliielekeza Nguvu kumshambulia Slaa lakini Mungu amebadili Plan ghafla na kumuleta Lowasa amabaye hawajajipanga nan i Pigo kubwa
(8)Kwa sasa Uasi uliojitokeza CCM ni vigumu kujua nani yupo kwa nani
Angalia mtandao wa Lowasa ndani ya CCM unatisha na umetulia Kimia.
Mtandao huu jumlisha nguvu ya Umma ni lazima CCM ibaki kama KANU
MAONI KWA SLAA.
(1)Wakati unagombea urais ulikuwa na Rozi Kamili ukamwacha na kumuoa Josephine
Rozi Kamili alikubali ujio wa Josephine lakini leo Josephine huyo amekuwa kikwazo kwa maamuzi yako.
(2)Mambo ya Chama huwezi kumuhusisha Mwanamke, huo ni udhaifu mkubwa na kama kweli unamsikiliza mwanamke basi ujue hutapata nafsi ya kurudi kwenye jamii na wakakuamini na kukupa heshima kama walivyokupa.
Mke ni mshauri wake kwa mambo yote lakini kikao kama kamati kuu kinapopitisha maamuzi harafu mkeo anapinga maana yake mke huyo hafai kuwa First Lady na hata wewe hufai kuwa Kiongozi
MAONI KWA LOWASA
(1)Umeitwa Mwizi kwa siku nyingi sana na hata mimi nimekuita hivyo , sasa huu ni wakati wa wewe kutuambia mwizi halisi ni nani na utoe Ushahidi
(2) Zipo taarifa kwamba CCM wanapanga kukata jina lako kwenyenye tume ya uchaguzi hivyo nakusihii usikate tama .Muombe Mungu .Hii ni safari ya ushindi na si matumaini tena
(3)Usiogope kushambulia Ikulu kwa kuwa Mussa alikaa Ikulu ya Farao na kulelewa hapo lakini Mungu alimupa kazi ya kumuangamiza Farao.
Hivyo Lowasa umepewa kazi ya Kuingamiza CCM hivyo fanya kweli ujue kwamba Slaa hajui haya.
 
Lowasa angekua fisadi CCM wangekua wameshampeleka mahakamani kama walivyofanya kwa Mramba, Yona, Liyumba etc! Mi naamin ni kashfa za kumchafua tu. Ila pia kama ni lish of shame hata JK na Mkapa wangetakiwa wawe treated kama Lowasa kwa kuitwa wote mafisadi.
Mi nakuunga mkono kwamba Lowasa akipata urais atataka kuonesha wananchi yeye siyo fisadi na atachapa kazi kweli kweli. Kuna mtu kabisha kwamba maji ya Victoria kwenda shinyanga sio kaz ya Edo! Hana taarifa na uhalali wa kubisha, kibuyu huyo

unajua shida ya maji iliyoko shinyaga,,
 
lowasa ni mafya kawapa sumu mwakyembe hawezi kuw rais,
 
CCM ina coverage kubwa kuliko chadema hyo ni sababu tosha kushinda uchaguzi wa mwaka huu...

Inawezekana mkuu siwezi kukubishia. Lakini nadhani labda wew umetoka Peripheral kuliko nilipotokea mimi brand udom huko vijiji vya Lumuma Kilosa ambako wananchi wenzangu wanahamu kubwa sana ya madiliko na chadema imeshika kasi sana tu.
Nikiwa njiani kuelekea mjini Kilosa au Mikumi nakutana na vijiji vya Chabima, Myombo, Zombo, Ulaya, Mhenda nk, kote huko habari kuu ni chadema tu.
 
Inawezekana mkuu siwezi kukubishia. Lakini nadhani labda wew umetoka Peripheral kuliko nilipotokea mimi brand udom huko vijiji vya Lumuma Kilosa ambako wananchi wenzangu wanahamu kubwa sana ya madiliko na chadema imeshika kasi sana tu.

Ubunge sawa mtashinda baadhi ya majimbo lkn overall ccm lazima iwabuluze...ukweli unauma.
 
CCM mtashinda JF Ila watanzania kila Kona ni lowasa. Kwani sio nyie mlimpa wajumbe 870000?
 
unajua shida ya maji iliyoko shinyaga,,

Kuna shida ya maji kwa kuwa ule mradi wa maji ya ziwa viktoria haijafika Shinyanga au kwa kuwa serikali imeshindwa kuendeleza na kusimamia usambazaji wake kama alivyokusudia Lowasa na serikali ya kipindi kile?
 
Ubunge sawa mtashinda baadhi ya majimbo lkn overall ccm lazima iwabuluze...ukweli unauma.

Ndo Ndo Ndo, ndoo hujaa mkuu. Pia haba na haba hujaza kibaba.
Kwa hiyo hao watakaopiga kura kumchagua mbunge wa UKAWA hujui pia ndio watakaompigia rais wa UKAWA pia,?
 
1. Richmond ni ya kikwete yuko ccm ( hajakanusha tuhuma)

2. Epa ni ya chenge yupo ccm

3. Escrow ni ya tibaijuka yuko ccm

4. Kiwira ni ya mkapa yuko ccm

5. Kuuza nyumba za serikali na skendo ya ufisadi wa bil 255 wizara ya ujenzi ni ya magufuli yuko ccm

sasa hapo upinzani na lowasa siwaoni kwanini nisimpe kura yangu?????
 
Back
Top Bottom