Kwa nini wajane/wagane wanaendelea kuvaa pete za ndoa kwa muda mrefu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini wajane/wagane wanaendelea kuvaa pete za ndoa kwa muda mrefu?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mzeelapa, Apr 23, 2012.

 1. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 992
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Ninavyofahamu mimi wakati wa kufungishwa ndoa wanandoa wanaambiwa ndoa yao ni mpaka kifo kitakapowatenganisha, sasa kwa nini mmoja wao anapofariki anayebaki anaendelea kuvaa pete hiyo kwa muda mrefu?1. Anawafanya wanaomtamani washindwe kumsogelea kwa kufahamu kwamba mume/mke wake yupo2. Anaendelea kuishi kwa majonzi wakati Dini inaruhusu kutafuta na kufunga ndoa nyingine na mtu mwingine3. Wana matumaini kwamba watakutana mbinguni, anajuaje kama bado atakuwa na mapenzi na naye, kwa mfano huku duniani anayebaki akiolewa/akioa mwingine atakayempenda kuliko aliyefariki anadhani atamjali tena? Kwanza atamwambia "mahusiano yetu yalikuwa duniani mkataba wa ndoa ulikwisha duniani baada ya kifo changu, take time pse. usinijue!!"Wafiwa, hasa ambao bado vijana msiishi kwa upweke, tafuteni wenza wengine mapema kwa raha zenu wala msiogope mtu (ila mjihadhari na UKIMWI)
   
 2. TsafuRD

  TsafuRD JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2013
  Joined: Sep 29, 2013
  Messages: 295
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sorry! Naomba nikurekebishe kidogo. Mbinguni hakuna habari kuoa wala kuolewa, kinachoenda mbinguni siyo mwili bali roho safi. Imeandikwa, binadamu ametokana na mavumbi, na mavumbini sharti atarudi lakini roho iliyo punzi ya Mungu humrudia Mungu. Kwa suala la kuendelea kukaa na pete ya ndoa nadhani si sahihi tena maana imeandika hadi kifo kiwetenganishe.
   
 3. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2013
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 992
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Asante kwa kunirekebisha. Sasa mbona watu wanaishi kwa matumaini ya kukutana (roho) Mbinguni/paradiso? Tutafufuliwa siku ya mwisho, ok, roho ndio zitakazofufuliwa raha zenyewe tutazipataje au zikoje?
   
 4. Ndugu yangu

  Ndugu yangu JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2013
  Joined: Aug 3, 2013
  Messages: 583
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Soma bibliya
   
 5. habari ya hapa

  habari ya hapa JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2013
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 8,693
  Likes Received: 3,932
  Trophy Points: 280
  Mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa, huko wote ni mabibi harusi si wanaume wala wanawake wote watavaa mashela
   
 6. m

  mhondo JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2013
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 969
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kuna miili ya mbinguni ambayo haitofautishi kama huyu ni mwanamke na yule ni mwanaume.
   
 7. Sista

  Sista JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2013
  Joined: Sep 29, 2013
  Messages: 3,216
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ndoa zao zinakwisha kutokana na sababu za kifo wanakuwa bado wanapendana
   
 8. Varbo

  Varbo JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2013
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 914
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Baba yangu alifariki siku nyingi hata sisi tulikua tayari ni wakubwa maana wakati mzee anafariki mtoto wa mwisho alikua na 14yrs and I was 18!! Baadae mama alipata mtu mwingine akaolewa na alichokifanya hakuitoa ile Pete ya marehem baba yangu!! Sasa anapete mbili ktk kidole Kimoja!!mie hua sielewi maana yake sijui kwa kumpenda Sana mzee wangu au vip!!
   
 9. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2013
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 992
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Huu mtihani!! Kama una ubavu muulize mwenyewe mama halafu utuletee majibu jamvini. Labda Mch. Msigwa kama pia anapitia mtaa huu atujibu. (Hakosi jukwaa la siasa ingawa kwa jina bandia)
   
 10. Karucee

  Karucee JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2013
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 10,425
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  Am thinking its difficult to let go just yet. I wouldnt wanna be in their shoes kwa kweli.
   
 11. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2013
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,310
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wajane/wagane wanaendelea kuvaa pete za ndoa kwa kuenzi na kukumbuka mapenzi,fadhila na mema aliyokuwa anayapata kutoka kwa mwenzi wake....kisaikolojia kwa kuendelea kuvaa bado anajifariji kuwa yupo pamoja naye. Km utabahatika kuoa ama kuolewa na mfiwa, jitahidi kumuenga na kummiminia mahaba kuliko mpendwa wake aliyetangulia mbele za haki...Ukifaulu mwenyewe ataivua pete ya awali kwa mkono wake. Vinginevyo umeshindwa kumpa mahaba kiasi cha kukumbuka yaliyopita
   
 12. Daud omar

  Daud omar JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2013
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,463
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama kuna tatatizo, Tatizo langu kwa wale wanaovua pete kwenye kidole cha ndoa na kuvaa kwenye vidole vyengine wakiwa sehem sehemu zao, ilihali wapenzi wao wapo hai na wanaishi nao
   
 13. Latifaa

  Latifaa JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2013
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 455
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  bora'hata'hao'wajane'wengine'wanatalaka'chaajabu'bado'wanaendelea'kuvaa'hizopete
   
Loading...