kwa Nini Waafrika ndio Tunapenda Kuwacheka watu wasiojua kiingereza?

Quinine Mwitu

JF-Expert Member
Oct 19, 2014
5,266
5,663
Wasalaam,
kama kichwa kinavyojieleza hapo juu,kwa nini waafrika wengi mtu anapokuwa hawezi kuongea kiingereza huwa tuna muona kama si lolote si chochote,Kuna Kipindi nimewahi kufanya hizi kazi za utalii kwa hiyo niliweza kugundua mawili matatu juu ya lugha ya kiingereza
1.Mzungu hata ungeongea kiingereza brocken vipi hawezi kuhisi vibaya au kuacha kuongea na wewe hata kama huongei vizuri lugha husika yaani kiingereza,ila ataacha mawasiliano na wewe kama atakuwa amekuuliza kitu na ukamjibu isvyo sahihi
2.Wazungu wachache sana wanaoipa lugha ya kiingereza kipaumbele,kuna wazungu wnaweza kuwa kadhaa hata ishirini ila akawepo mmoja tuu(tour Leader) ndio anajua lugha tena kwa kuunga unga kwa ajili ya kuwasiliana na mwenyeji wao,na wao huwa wanaamini kwa kuwa lugha yetu si kiingerza si ajabu ukakuta wengi hatujui lugha husika
3.Ni wabongo tuu ndio tuna hukumu sana masuala ya lugha hasa kuwacheka wasio jua lugha vizuri,yaani Tanzania usomi ni pamoja na kujua kuongea kiingereza,kitu ambacho havina uhusianao kabisa
Je wakuu kwa nini hali hii inatokea sana nchini kwetu?
 
Nilishatembea sana nchi za watu. Kuna nchi hawataki hata kukijua hicho kiluga. Mbali zaidi kuna nchi ukifanya manunuzi kwa dola hawataki kabisa hiyo mambo ya dola sitaki niseme ni wapi maana bado napata ugali wangu.
 
Daa wabongo tunachekana balaaa
 
Wasalaam,
kama kichwa kinavyojieleza hapo juu,kwa nini waafrika wengi mtu anapokuwa hawezi kuongea kiingereza huwa tuna muona kama si lolote si chochote,Kuna Kipindi nimewahi kufanya hizi kazi za utalii kwa hiyo niliweza kugundua mawili matatu juu ya lugha ya kiingereza
1.Mzungu hata ungeongea kiingereza brocken vipi hawezi kuhisi vibaya au kuacha kuongea na wewe hata kama huongei vizuri lugha husika yaani kiingereza,ila ataacha mawasiliano na wewe kama atakuwa amekuuliza kitu na ukamjibu isvyo sahihi
2.Wazungu wachache sana wanaoipa lugha ya kiingereza kipaumbele,kuna wazungu wnaweza kuwa kadhaa hata ishirini ila akawepo mmoja tuu(tour Leader) ndio anajua lugha tena kwa kuunga unga kwa ajili ya kuwasiliana na mwenyeji wao,na wao huwa wanaamini kwa kuwa lugha yetu si kiingerza si ajabu ukakuta wengi hatujui lugha husika
3.Ni wabongo tuu ndio tuna hukumu sana masuala ya lugha hasa kuwacheka wasio jua lugha vizuri,yaani Tanzania usomi ni pamoja na kujua kuongea kiingereza,kitu ambacho havina uhusianao kabisa
Je wakuu kwa nini hali hii inatokea sana nchini kwetu?

Ni kwa sababu Mwafrika anakwenda Shuleni kujifunza Kiingereza tu na hakuna kingine, ndio maana hivyo kila kitu kimezunguka hapo kwenye hiyo Lugha, kwa Mwafrika Kiingereza ni zaidi ya lugha, lkn cha ajabu pmj na kuwa ndiyo watu tunaojifunza Kiingereza muda mwingi klk wote Duniani ukiondoa wenye lugha wenyewe bado hatukijui hicho Kiingereza, watu wanaowezaa kutumia lugha ya Kiingereza kwa ufasaha Korea kwa mfano ni wengi klk Kenya au Uganda ingawaje Korea hawatumii Kiingereza kama lugha ya kufundishia isipokuwa kama somo tu!
 
71c0ad353c9bbff2a8fdf74c5d406930.jpg
 
kwa style hii ya Harmorapa "mimi ni strong woman" bora tuendelee kuchekana tu..
 
Attachments

  • VID-20170420-WA0030.mp4
    2.9 MB · Views: 32
Usiseme waafrika wala usiseme watz Bali sema wale wanaojifanya kumchukia raisi magufuli na kwa vile rais hajaweka kiingereza kipao mbele na wao wameifanya kama hoja ya msingi..
Upumbavu ni janga kubwa mno kwa baadhi ya watanzania
 
Back
Top Bottom