Guus
JF-Expert Member
- Jul 16, 2013
- 1,167
- 907
Salamu kwenu nyote.
Nadhani wengi tumekuwa tukishuhudia "video clips" zinazowaonesha watoto wanapokuwa wamekosea katika namna ambayo si ya kufundisha (mara nyingi zikiwa na mlengo wa kufurahisha/kuchekesha watazamaji). Mimi nimekuwa najiuliza, ni nani anawapa mamlaka hawa watu kurekodi na kusambaza hizi "clips"? Je, hii ni haki kwa watoto, ambao sisi wenyewe tunajua ndicho kipindi cha wao kufundishwa waelewe badala ya "kubezwa"? Je, miaka kadhaa mbele huyu mtoto anapokuwa mtu mzima na kuona hizo "clips" atazipokeaje, huu si mwanzo wa kuharibu saikolojia zao mbeleni?
Sijui wanaforum mnalionaje hili? Binafsi silioni hili kama ni jambo la kufurahia tunapoziona "clips" hizi zinazowaonesha watoto. Nadhani tunawajibu wa kuzipinga kabisa katika jamii.