Kwa nini tunamsahihisha mwenyezi mungu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini tunamsahihisha mwenyezi mungu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Power G, Aug 26, 2011.

 1. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Wapenzi wana JF, vitabu vitakatifu vinatuambia kwamba Mungu alimuumba binadamu kwa mfano wake. Na wakati huo huo kuna msemo kwamba kazi ya Mungu huwa haina makosa. Kama hayo ni kweli na tunamheshimu Muumba wetu, kwa nini kumsahihisha kwa kufanya modifications kwenye kazi alizofanya kwa mikono yake?

  Naomba nitoe mifano michache hasa kwa kutumia makabila ya hapa kwetu Tz jinsi wanaadamu wanavyojitahidi kumfanya Mungu aonekane alichofanya siyo bora kwa kuweka ulemavu wa kudumu kwenye kazi alizofanya:-
  Nikianza na ndugu zetu wamasai kwa mfano wana utaratibu wa kuondoa idadi fulani ya meno ya chini mdomoni na kubaki na uwazi katika safu ya meno. Kwa maana nyingine wanamuona Mungu kuwawekea meno 32 alikuwa na makosa makubwa sana.
  Ndugu zetu Wajaluo, wao hutoa meno 6 ya juu na kubaki na meno 26. Lengo hapa bado ni kumsahihisha Muumba. Hapo hapo wazanaki wao wanayachonga meno yote na kuyafanya yawe na ncha kali.
  Ndugu zetu Wakurya, Wagogo na Wamasai waliona maumbo ya masikio waliyoumbiwa na mwenyezi Mungu hayafai wanafanya kazi ya kuyapasua na kuyarefusha mpaka mabegani
  Ndugu zetu wamakonde waliona Mungu kuwaumbia mdomo usio na dirisha ni makosa wakaamua kutoboa na kuweka ndonya
  Ndugu zetu wakurya, wagogo, wanyaturu, wamasai nk walimuona Mungu alikosea sasa kuwaumbia wanawake kale kadudu ambako kako kwenye maeneo nyeti ya miili yao wao wakaamua kufanya modification kwa kukakata na kuwaacha akina mama hawana ashiki.
  Ndugu zetu wajita na wakerewe, wao badala ya kufahamu kwamba hako kadudu kanakokeketwa Mungu alikaumba kawe na urefu maalum kwa madhumuni maalum, wao wanafanya modification ya kukavuta kwenye maji ya ziwa na kukarefusha hadi kufikia urefu wa inchi 6. Modification nyingine ambayo kwa sasa inafanyika karibu na makabila mengi ni ile ya kuuondoa mfuniko ambao mwenyezi Mungu aliuweka kwenye 'mkia' wa mwananume.

  Jamani kama tunaona mwenyezi Mungu hafahamu kazi yake vizuri ni vema kila kabila likatengeneza template yake jinsi linavyotaka liumbwe halafu tumpe Mungu awe anatufyatua tukiwa hivyo hivyo. Inasikitisha kuona gari linatoka kiwandani likiwa benz lakini likifika duniani linafanyikiwa modification na kuonekana suzuki.
   
 2. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,080
  Trophy Points: 280
  Hapo kwa wajita na wakerewe nimebaki mlango wazi!!!!!
   
 3. Ze burner

  Ze burner JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 460
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  mmmmhh!!!!
   
Loading...