Kwa nini timu ya taifa isiitwe tanganyika stars?

Mkorosai

Member
Nov 17, 2010
65
0
Timu yetu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars itaendelea kufungwa na kufanya vibaya ktk mashindano mbalimbali hadi tutakapo tambua haya yafuatayo:
1. Kwamba ile ni timu ya Tanganyika (Tanzania Bara) na rangi za bendera ya Tanganyika zilikuwa kijani, njano na nyeusi tu.
2. Kwamba kuendelea kutumia jezi zenye rangi ya blue ni mkosi kwa timu hiyo kwa kuwa Zanzibar haihusiani kabisa na hiyo timu.
3. Kwamba ni lazima ipewe jina linalo itambulisha na itofautishwe na Taifa Stars.
4. kwamba ni utumwa kuendelea kujifanya kusahau asili na historia
5. nk

mnasemaje wadau?
 
kwani jina nalo linacheza mpira? hata waitwe jina gani au wavae nguo yenye bendera yoyote unayojua wewe ila kama timu ni mbovu kipigo kitabaki palepale.. kwa ujumla mpira wa miguu hauangalii jina wala jezi bali ni kiwango, hata ukicheza peku au kifua wazi lakini kama mnaweza kukipiga lazima mtafanikiwa, so my take: hizo changes unazozungumzia mkuu haziwezi kubadilisha matokeo ya hii timu.
 
Back
Top Bottom