Kwa nini muhtasari mpya wa elimu haufai?

Mapigomoto

Member
Jan 21, 2016
19
11
MUHTASARI MPYA WA ELIMU HAUNA MADA WALA MALENGO

Muhtasari mpya kwa ajili ya kufundishia elimu msingi darasa la I - VI una kasoro nyingi. Muhtasari huo ukiruhusiwa utumike, elimu ya Tanzania itashuka sana.

Baadhi ya kasoro hizo ni kama ifuatavyo:

(a) Unasisitiza tu yanayotakiwa kuonekana kwa mtu aliyepata mafunzo fulani. Yaani, inasisitiza umahiri tu. Umahiri umepatikanaje? Muhtasari hauelezei.

(b) Muhtasari hauna mada kufundishwa wala malengo. Katika mazingira kama haya kila mwalimu atafundisha anavyoona. Badala yake muhtasari umetaja madaraja ya upimaji. Unapimaje bila kujua umefundishaje? Hata hivyo kama madaraja yalikuwa ni muhimu, kungekuwa na madaraja mawili tu. Yaani yenye Ndio au Hapana.

(c) Serikali imeagiza kuwa muhtasari wa darasa la kwanza na la pili uhusu Kusoma, Kuandika na Kuhesabu. Muhtasari unaonyesha kuwa baada ya mwanafunzi kusoma kwa miaka miwili awe mahiri katika kuhesabu. Umahiri huo ni kuhesabu hadi 1000. Je, kuhesabu hadi 1000 ni kujua kuhesabu? Tunatakiwa kujua watoto wa darasa la pili kwa siku hizi wana uelewa gani katika kuhesabu.

(d) Katika muhtasari huu kuna maneno mengi yasiyotakiwa kutumika hata kidogo. Kama vile:

(i) Kufikiri na kuhakiki ...... na

(ii) Kufahamu mising ...... .

Kutokana na hali hii, inaonyesha wazi kuwa wizara ya Elimu bado haijatambua kwa nini wanafunzi ni dhaifu katika kujifunza. Njia nyingi za kufundishia na kujifunzia zimefundishwa vyuoni lakini bado hali ya elimu kwa shule za serikali ni mbaya. Tujiulize, kwa nini shule binafsi zinafanikiwa? Je ni mishahara mikubwa tu? Hapana!

Mwisho, tuige ufundishaji kutoka shule binafsi KUOKOA ELIMU TANZANIA.
 
Zipo mbinu nyingi za kuwatawanya kondoo ikiwemo kumpiga mchungaji wao....
 
Kwa ufupi kila kitu tunataka Ku copy and paste kutoka abroad bila kujua athari itakayotokea dah hii ndio elimu ya Ki digital
 
Hello everyone! Some weeks ago I have got papers from the coolest essay-company com writing service that are doing classy assignments and there is nothing to add. Even for my economics tutor has nothing to add about the quality of their work. Maybe economics is really an exciting subject for pupils?! Click on their website if you want to know more information.
 
Kuua kizazi,ili watoto wao waje kutawala tena na tena.Watoto wao wanasoma shule za private.Hebu tuwekee huo muongozo hapa
 
Back
Top Bottom