Kwa nini maendeleo ya watanzania mwendo kinyonga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini maendeleo ya watanzania mwendo kinyonga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwanitu, Apr 8, 2012.

 1. M

  Mwanitu JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 634
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 80
  Wtz wenzangu
  nimekuwa nikijaribu kutafakari, kwa nini nchi yetu haisongi mbele kama ambavyo ingetakiwa kutokana na Mwenyezi Mungu alivyotujalia Utajiri Mwingi Nchi hii.
  baadhi ya matatizo yetu nadhani ni haya.
  Umeme mgao kwa hiyo gharama za kuzalisha bidhaa ziko juu sana.hii inachangia kuuwa viwanda vilivyopo nchini.
  waalimu ni kama hawalipwi ,kwa hiyo elimu inazidi kushuka
  wanasiasa kujiingiza kwenye maamuzi ya kitaaluma. mfano ununuzi wa mashine mbovu za kupimia ukimwi
  wezi wakubwa kutowajibishwa,hivyo wakubwa kushindwa kuwawajibisha waliochini yao, na hivyo ugonjwa kuendelea
  dawa zilizochakachuliwa zinauzwa waziwazi. uliza kwa nini wafugaji wa kuku wengi wameacha kufuga siku hizi?
  hakuna mchujo thabiti wa vipaji vya watoto.wakubwa wanalazimisha wanao hata wasio na uwezo kuandikishwa
  hakuna miundombinu ya kilimo cha uhakika cha umwagiliaji
  mabenki riba zinatisha. haziko kumnyanyua mwananchi
  kufanya biashara ni kero waulize wasafirishaji vyakula toka mikoani wanavyonyanyaswa na traffic
  mitaala ya elimu imekuwa ikibadilika badilika sana.mara tufundishe kwa kiswahili.mimi ninavyojua sisi tunategemea technologia za wenzetu katika karibuni kila kitu. kujilinganisha na wachina au warusi ni makosa.technologia itangulie halafu ndio lugha ifuate.tutawachanganya watoto na hasa dunia ya leo ya utandawazi.
  kwa maoni yangu tutaendelea tuu iwapo viongozi wetu watakuwa na uzalendo na kufuata misingi ya utawalw bora.
  Mfano mzuri ni Rwanda,angalia jinsi inavyosonga mbele licha ya kuwa imepita juzijuzi kwenye mauwaji ya kimbari.mabadiliko ja jamii kwetu waafirika huwa yananzia juu.Rwanda ni mfano hai
  Ni matatizo gani mengine yanayotukwamisha?naomba mchango wenu.
   
Loading...