Kwa nini inaitwa Vita Kuu ya Kwanza/Pili ya Dunia?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Hili jambo limekuwa likinitatiza na kwamba nashindwa kuelewa ni kwa nini hasa hivi vita vimepewa namba? Ni kwa nini wanaita Vita ya Kwanza na Pili? Kwa maana kwangu mimi kama ukisema hii ni Vita ya kwanza, na hii ya Pili ina maana kuna ya tatu, 4, 5 ... sasa kwa nini?

Na vilianzwa kupewa namba lini? Je ni kabla ya Vita ya kwanza kutokea au baada?
 
Inaitwa vita ya kwanza na ya pili kwa sababu ilipiganwa sehemu kubwa ya dunia kuanzia,ulaya,asia hata huku kwetu vita ya kwanza iligusa.
 
Sijaulijza kwa nini viliitwa Vita vya Dunia hilo naelewa, ila ambacho sielewi ni hiyo namba, ni kwa nini vipewe namba? Na vilianza kupewa namba lini kabla au baada ya vya Kwanza na Pili?
 
Kwanini ya kwanza au ya pili ni namna kuieleza ungeweza hata kuita vita ya A na B. Lakin its matter of number and naming. Kuna vita nyingi zilipigwa na zikaitwa kulingana either eneo, wahusika,source. Mfano wa vita ya majimaji.
 
unajishaua hapa,jibu lako utalipata kwa yule msomi wa pale udom,sisi ni vilaza umetusahau?????
 
We unapendekeza/ungepedekeza jina gani AF historia huandikwa kaba au baada
 
Lakini tatizo nililonalo ni hiyo namba, kwangu mimi ukisema hii ni Vita ya kwanza, hii ya Pili ina maana kuna ya tatu na nne n.k na hapo ndipo naposhindwa kuelewa!
 
Sijaulijza kwa nini viliitwa Vita vya Dunia hilo naelewa, ila ambacho sielewi ni hiyo namba, ni kwa nini vipewe namba? Na vilianza kupewa namba lini kabla au baada ya vya Kwanza na Pili?
Kama unaelewa kuwa vilikua ni vita vya dunia, then lazima uelewe ilibidi vipewe majina, Ili iwe rahisi kuvitambua.
 
Lakini tatizo nililonalo ni hiyo namba, kwangu mimi ukisema hii ni Vita ya kwanza, hii ya Pili ina maana kuna ya tatu na nne n.k na hapo ndipo naposhindwa kuelewa!
Ahaa bac subiri wana historian wakujibu binafc cjui
 
Sijaulijza kwa nini viliitwa Vita vya Dunia hilo naelewa, ila ambacho sielewi ni hiyo namba, ni kwa nini vipewe namba? Na vilianza kupewa namba lini kabla au baada ya vya Kwanza na Pili?
Mimi nafikiri kabla ya Vita ya 1939-1945 ambayo inatambulika Kama vita ya pili ya dunia, ile ya kwanza ilikuwa inatambulika tu kama vita ya dunia. Baada ya kutokea ya pili ndio wakazipa namba ili ziweze kutofautishwa kihistoria.
 
Kama nimekuelewa vile?,hebu ni pm CV yako fasta!
 
simple, hiv ikitokea ukamuambia mtu kwamba japan ilikuwa nchi ya mwisho kusurrender kwenye vita ya dunia, afu huyo mtu akakuuliza vita ya dunia ipi? chukulia sasa hapo hazipewa namba wewe utajibu vipi? bila shaka kama ni iliyoanza utasema 'ile ya kwanza' tayari ulishaipa namba, kama iliyofuatia utajibu ni 'ni ile ya pili/ya mara ya pili' tayari ulishaipa namba.
 
Hili jambo limekuwa likinitatiza na kwamba nashindwa kuelewa ni kwa nini hasa hivi vita vimepewa namba? Ni kwa nini wanaita Vita ya Kwanza na Pili? Kwa maana kwangu mimi kama ukisema hii ni Vita ya kwanza, na hii ya Pili ina maana kuna ya tatu, 4, 5 ... sasa kwa nini?

Na vilianzwa kupewa namba lini? Je ni kabla ya Vita ya kwanza kutokea au baada?
Jina limepatikana kutokana na vita ya miaka1914-1918 iliyoona mapambano kati ya Ujerumani na wenzake dhidi ya nchi nyingi. Vita ya 1914/1918 iliitwa "Vita Kuu ya Dunia" kwa sababu mapigano yalienea pande nyingi za dunia yote tofauti na vita zilizotangulia. Kwa namna fulani vita iliyoanza 1939 ilikuwa marudio ya vita iliyotangulia. Hivyo imekuwa kawaida kuzitaja vita hizi kama Vita Kuu ya Kwanza na ya Pili ya Dunia.
 
Back
Top Bottom