Kwa nini formula hii ni ngumu kwa Afrika?

Kwa nini formula hii ni ngumu kwa Afrika?

Sijali

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
2,700
Reaction score
1,857
Ukisoma na kufuatilia maendeleo ya nchi nyingi dunia ya tatu, utakuta zimefuata formula moja inayofanana. Wameanza kuendeleza uwezo wa watu wao kwanza (siyo large scale exploitation ya resources zao). Kisha walipopata uwezo ( Wataalamu wa kutosha wa fani na tasnia mbali mbali) ndipo waka exploit resources zao wenyewe.

Kama tungeanza hivi, hakuna sababu leo ya kumwita Mzungu atuchimbulie madini, gesi yetu achukue 9 atuachie 1.
Kwa nini viongozi wa Afrika hawana subira? Kana kwamba kila mmoja katika kipindi chake ataka amalize kila kitu? Nchi siyo kama nyumba ya mtu, itaendelea kuwepo miaka kadhaa.

Mwaka 1979 Iran ilipofanya mapindzi haikuwa na uwezo hata wa kutengeneza bunduki.Lakini waka invest katika kuendeleza uwezo wa watu wao na leo wanapeleka satalaiti na makombora, pia wanatengeneza matrein, dams, helikopta nk.

Kwa kweli maendelo ya nchi siyo kitu kigumu. Ni kiasi cha kuwa na siasa safi, uongozi bora na kujiamini. Hii China nimeiona ikiwa maskini wa kutupwa katika maisha yangu, leo ni dola kubwa.
 
hata mim huwa nashangaa,,, kwanin hawa viongoz hawajifunzi huu mfumo,,,
 
Iran ilikuwa imeendelea toka enzi za PM Mussa Musadik,alitaifisha visima vya mafuta toka kwa WAINGEREZA mwaka 1951.Mwaka 1953 fitina Mwingereza aliipeleka kwa AMERIKA wakampindua na kumuweka SHAH MOHAMED REZA PAHLAVI.Wairani ni wasomi toka enzi za MESOPOTAMIA(miaka 2500 kabla ya kristo).
Afrika inakuwa ngumu viongozi wamebanwa sana na pia ulimbukeni wa wazungu.
 
Wenzako wanajinufaisha wenyewe, na mimi nikipata nafasi nitaiba mpaka mkome.
 
Back
Top Bottom