Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,353
- 38,544
Huwa sielewi mantiki ya kila likifanywa jambo na Rais John Magufuli ambaye ni rais wa watanzania wote, watu wanaojinasibisha kama mashabiki wa CCM humu JF hukimbilia kumfananisha na Lowassa. Mashabikia hao huuliza "Lowassa angeweza kufanya hiki ama kile?" kama vile kila jambo linalofanywa na Magufuli linafanywa kama ni mashindano kati yake na Lowassa.
Kama ni kwa kuwa Lowassa aligombea Urais mwaka 2015 pamoja na Magufuli, mbona wapo na kina Dovutwa na Rungwe lakini hawalinganishwi na Magufuli? Kwani Magufuli anafanya jambo ili kuonesha kwamba yeye ni zaidi ya Lowassa ama huwa anafanya mambo kwa maslahi ya taifa zima bila ya kujali itikadi za vyama vya siasa?