Kwa mwenye ufahamu apite hapa kuhusu hili la Joe Biden, Rais wa Marekani

omtiti

JF-Expert Member
Jun 19, 2019
1,022
1,590
Chanjo ilitolewa duniani, na kuna baadhi ya viongozi mashuhuri duniani tuliona hadharani wakichanjwa kama kuonyesha umuhimu wa chanjo na uwajibikaji pia.

Ninavyofahamu mimi layman katika masuala ya afya ni kwamba chanjo ni kinga dhidi ya tatizo husika, ikiwa na maana ukichanjwa unakua umepata kinga kamili.

Swali: Joe Biden Rais wa USA, kachanjwa kinga dhidi ya covid-19, na inasemekana kachanjwa mara mbili, japo ninavyofahamu mimi kachanjwa mara moja. Kwanini yeye na mkewe bado wanakomaa na barakoa?

Je, si ni kuonyesha kwamba hana hakika na chanjo aliyochanjwa? Kama anahakika kwanini avae barakoa?

Kwasababu alitakiwa aachane na barakoa kwa vile tayari kachanjwa "which means he's is free against covid 19" na ndipo angefanya tuamini chanjo hiyo ni salama?

Swali la pili, jana Chama Omary Matata mtangazaji wa BBC alichanjwa kwa mujibu wa mahojiano aliyofanya na Salim Kikeke wa BBC.

Alisema alipofika kituo cha chanjo aliulizwa aina ya chanjo, sizikumbuki majina kiufasaha akachagua moja wapo. Kwanini aulizwe ipi anapenda wakati zote dhamira yake ni moja na zimethibitshwa WHO?

Swali la tatu, kwanini baada ya Chama Omary Matata kuchanjwa aliuliza side effects za chanjo hiyo aliambiwa kwamba anaweza kuhisi homa akaambiwa akijisikia hivyo ameze Panadol.

Kuna mjuzi hapa atusaidie tupate elimu?

Swali la nne mkurugenzi Mkuu wa WHO nilimnukuu akisema chanjo hiyo si hisani, alimaanisha nini?

Nimalizie kwa kusema au ndio maana Rais Magufuli alitutahadhalisha na akasema kuna mengi anayajua sisi hatuyajui?
 
Swali no 3. Dawa zote zina side effects, hata za malaria ukisoma maelezo yake imeandikwa side effect kwamba unaweza kuhisi kizunguzungu,kichefu chefu nk. Wanasema ukiona hizo side effects achana nazo nenda hospitali umwone daktari. Dawa nyingine zimeandikwa asimeze mama mjamzito au mwenye kisukari nk....
 
Shukrani sana
 
Swali la kwanza,

Kinga waliyopatiwa ni ya Coronavirus ile ya kwanza,Virus hufanya mutation kama ulivyosikia huko South Africa na England,so unaweza ukawa na kinga ila ukaipata ile new strain,halafu unaweza ukawa carrier of the virus and will pass it onto to others even if he is protected from infection.

Nobody is safe until everyone is safe.
 
Swali la kwanza,
Kinga waliyopatiwa ni ya Coronavirus ile ya kwanza,Virus hufanya mutation kama ulivyosikia huko South Africa na England,so unaweza ukawa na kinga ila ukaipata ile new strain,halafu unaweza ukawa carrier of the virus and will pass it onto to others even if he is protected from infection,
Nobody is safe until everyone is safe.
Je wakati anapokea chanjo si alipimwa na alikuwa free against covid-19?,u Carrier utoke wapi ?,kama swali halijaeleweka nisamehe
 
Je wakati anapokea chanjo si alipimwa na alikuwa free against covid-19?,u Carrier utoke wapi ?,kama swali halijaeleweka nisamehe
Mkuu,anaweza akawa na kinga ila akaambukizwa corona ambayo ni kali zaidi,anaweza akawa na kinga ila akawaambukiza watu wengine,Chanjo haikufanyi usiambukizwe bali ni kinga ya ugonjwa ukiupata usidhurike,ndio maana unaona vaccine zote mpaka sasa hakuna iliyo 100%
Kitu muhimu ni watu kupata vaccine ili kuutokomeza huu ugonjwa kabla haujafanya mutation na kua mkali zaidi ya ulivyo sasa.
 
Back
Top Bottom