Mkuu mahali unapoishi walimu wote wamepanga? Hakuna mwalimu mwenye maisha mazuri?
Pengine unazungumzia walimu zubaifu ila ualimu ni kazi ambayo mtu unaweza kufanikiwa mapema sana.
Mimi ni Mwalimu natamani ungenitembelea.
Unatakiwa kujibana mwanzo ili kutafuta mtaji, ukishapata tu hata 1m hapo tayari umetoboa.
Tatizo wengi mnaishi kwa kutegemea salary, inatakiwa salary ikupe mtaji then fungua magoli tofauti iwe kilimo, ufugaji, uvuvi, duka, genge, mgahawa, mitumba etc.
Watu wengi wanataka wakiajiriwa tu wawe na maisha mazuri, hawataki kujibana kutengeneza kesho yao.
Huo mshahara ni mkubwa sana.
Pale UDSM kuna watu wanafanya kazi ya usafi wanalipwa below 150,000, nyumbani wanafamilia, wamepanga, wanalipa bills za maji, umeme nk ila wanaishi na wengine wamejenga lakini sababu ni kuwa wamejibana na kuplan vizuri. Huwezi kuwa unapokea Sh. 200,000 alafu unatumia 200,000. Au unapokea Sh. 100,000 alafu unaishi nyumba yenye kpdi ya Sh. 60,000 huo ni upumbavu.
Ishi hata nyumba isiyo na sakafu wala umeme wakati unajipanga kutafuta mtaji. Ukidhani degree yako inathamani sana basi endelea kula bata na kulalamika mshahara mdogo....