Ndugu zangu,
Kwa jinsi ambavyo mmeweka matangazo yenu hamna tofauti na yule mshamba mwenye TZS 40,000 ambae ameenda nayo dukani na badala atafute nguo anayoipenda ndio aanze ku-burgain, yeye ameanza tu na kusema "ninataka zile jeans za elfu arobaini".
Cha kufanya, nenda Goba, tafuta kiwanja ukipendacho, zungumza ufikie makubaliano kisha ufanye biashara. Tatizo wengi mmekariri kuwa viwanja (pamoja na kwamba vipo eneo moja) basi vyote vipo sawa. La hasha, viwanja vina tofautiana thamani hata kama vipo eneo hilo hilo. Hivyo kuepushwa kuingizwa mjini, nenda field kijana.