Kwa Mhe. Tundu A. Lissu

Zakaria Lang'o

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
2,593
2,768
Mabalozi wa Mashina ya CCM wapigwe marufuku kujihusisha na masuala ya serikali.


Mods naomba maoni haya yamfikie Mhe. Tundu Lissu kama mwanasheria na mpigania haki na utawala wa Sheria katika nchi yetu.

Kwa miaka mingi tangu ujio wa vyama vingi, Chama cha Mapinduzi kimekuwa kikiwatumia Mabalozi wa mashina ya Chama kwa shughuli za kiserikali isivyo halali. Mabalozi hawa ambao hawamo katika mlolongo wa uongozi wa serikali kikatiba na kisheria wamekuwa wakifanya yafuatayo isivyo halali:

  • Kusikiliza kesi na mashauri katika maeneo yao huku wakijuwa wazi kuwa hawana mamlaka kisheria ya kufanya hivyo. Tabia hii imesababisha Chama cha Mapinduzi kupitia kwa mabalozi hawa kupoka mamlaka ya viongozi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji.
  • Kushiriki kuuza maeneo kwa kugonga mihuri yao ya shina katika karatasi za mauziano yanayofanywa na wananchi kinyume cha utaratibu. Miongoni mwa lawama wanazotupiwa viongozi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji juu ya matumizi mabaya ya mihuri kwa hakika wahusika wakuu ni mabalozi waliojivika majukumu ya kiserikali kinyume cha utaratibu wa kikatiba na kisheria.
  • Kutambuliwa na taasisi mbalimbali za kiserikali na za kibinafsi kama polisi, mahakama, mabenki n.k ni ishara mbaya ya vyombo vyetu kutojali kanuni za utendaji wa serikali, hivyo kusababisha mkanganyiko wa kuchanganya utendaji wa viongozi wa Chama cha Siasa na ule wa serikali. Inashangaza kwamba hata mahakama ambayo ndiyo inapaswa kusimamia tafsiri ya sheria, huweza kumwita balozi wa shina kutoa ushahidi wa masuala ambayo yanatakiwa yasimamiwe na viongozi wa serikali wa eneo husika.
  • Kurubuni wananchi wakati wa chaguzi mbalimbali kwa kuwa kichocheo cha rushwa. Hapa itoshe kusema tu kuwa ikiwa kuna Mwana JF ambaye nyumbani kwao/kwake balozi wa shina hajawahi kufika na furushi la chumvi n.k. ili kuwashawishi kutoa kura kwa wagombea wa CCM, ajitokeze na awe mkweli mbele za Mwenyezi Mungu.
Ieleweke kuwa kipindi cha utawala wa TANU hawa mabalozi walitumika kiserikali wakiitwa "Wajumbe wa Nyumba Kumi". Hii maana yake ni kwamba serikali ilianzia kwenye nyumba kumi. Mwaka 1977 CCM ilipoanzishwa iliweka kwenye katiba yake neno 'Shina' ikiwa ni kikao cha mwanzo cha chama. Kiongozi wa Shina akaitwa 'Balozi'. Eneo lililokuwa la utawala wa 'Mjumbe wa Nyumba Kumi' likaguzwa na kuwa 'Shina la CCM', likiwa chini ya 'Balozi'. Kwa kuwa wakati huo CCM ilikuwa Chama Dola hakukuwa na tatatizo la mgongano wa kiutawala.
Mwaka 1992 vilipoanza vyama vingi ilipendekezwa kuwa viongozi hawa warudishwe serikalini kama ilivyokuwa wakati wakiwa Wajumbe wa Nyumba Kumi ili serikali ianzie hapo, lakini kwa mshangao wa wenye akili CCM na serikali yake walikataa na kuendelea kuwatumia kufanya kazi za kiserikali kinyemela.
Wakati umefika na ni sasa, kwa wanasheria nguli kama Mhe Lissu kupeleka hoja mahahakamani ili watu hawa wapigwe marufuku nchi nzima kujihusisha na masuala ya kiserikali huku mitaani hadi hapo serikali itakapokubali kuanzisha utaratibu wa kisheria unaohuruhusu serakali za mitaa kuanza kwenye ' Nyumba Kumi'.
Nchi ni lazima iongozwe na Katiba na Sheria kuanzia chini hadi juu ili kuepuka kuwafanya watu wasiyotambuliwa kikatiba kuwa sehemu ya uongozi wa nchi bila utaratibu.

Ijulikane kuwa katika maeneo mengi ambayo wenyeviti wa mitaa/vijiji kutoka upinzani walichukua madaraka, mabalozi hawa wametumika na serikali na chama chao kudhoofisha demokrasia kwa kiwango kikubwa. Kuendelea kuwatumia mabalozi kinyume cha sheria ni kuendeleza uhuni na ubabe wa maccm. Haikubaliki!!!
 
Hawa mabalozi ni wa kuwapuuzia, ikiwa na shida muuone mwenyekiti wa Kitongoji, Kijiji au Mtaa.

Tusimchoshe Rais wa TLS, tumwachie mambo makubwa.

Sent from my TECNO P5 using JamiiForums mobile app
 
Yap hilo nalo neno! Yafaa wapatikane kwa njia ya kujichagua wenyewe kwenye hizo nyumba kumi na sasa yafaa ziwe 50 maana idadi ya watu imeongezeka halafu jina la aliyechaguliwa liwasilishwe kwenye serekali ya Mtaa ili atambuliwe na Mtaa husika kwani sasa hivi wajumbe wake wanaorodha kwenye serekali ya Mtaa.
 
Hawa mabalozi ni wa kuwapuuzia, ikiwa na shida muuone mwenyekiti wa Kitongoji, Kijiji au Mtaa.

Tusimchoshe Rais wa TLS, tumwachie mambo makubwa.

Sent from my TECNO P5 using JamiiForums mobile app
Ndugu yangu MBIIRWA labda hujasoma vizuri post hii na kuijua hoja ya msingi. Tunataka utawala wa sheria. Serikali inaanzia kwa Mwenyekiti wa Mtaa au kitongoji, ni kweli, lakini wale wanaotokana na ccm wamekuwa wakiwatumia hawa mabalozi kiserikali hadi taasisi kama mabenki, shule, vyuo na hata polisi huweka sharti la mabalozi kutambulisha watu katika nyaraka za kiserikali. Hii imewafanya mabalozi kudhani wao ni viongozi wa serikali. Hivyo zuio la kimahakama ni muhimu ili ikiwa serikali na taasisi mbalimbali zinauona umuhimu wa watu hawa basi itungwe sheria inayoruhusu wawe sehemu ya serikali. Huku si kumhangaisha Lissu. Tunataka atimize wajibu huu muhimu wa kuhakikisha utawala wa sheria unafuatwa kuanzia chini hadi juu!!!
 
Yap hilo nalo neno! Yafaa wapatikane kwa njia ya kujichagua wenyewe kwenye hizo nyumba kumi na sasa yafaa ziwe 50 maana idadi ya watu imeongezeka halafu jina la aliyechaguliwa liwasilishwe kwenye serekali ya Mtaa ili atambuliwe na Mtaa husika kwani sasa hivi wajumbe wake wanaorodha kwenye serekali ya Mtaa.
Hii inawezekana tu ikiwa watatambuliwa na sheria itakayotungwa na Bunge ili kuzifanya serikali za mitaa zianzie kwa 'wajumbe wa nyumba kumi' na chaguzi zao zishindaniwe na vyama mbalimbali kuliko ilivyo sasa ambapo wanatumika kinyemela wakati kiuhalisia ni viongozi wa chama na si serikali.
 
Back
Top Bottom