Kwa matokeo haya ya kidato cha nne,Serikali na Wizara husika viwajibike.Tutatengeneza Taifa bovu

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,865
Kwa sasa suala la Elimu ya Msingi na ile ya Upili imekuwa ni jukumu la sekta binafsi
Sekta binafsi ndio inajenga mazingira bora ya elimu na watoto kufanya vizuri kuliko serikali.

Lakini "Social Contract" kati ya wananchi na serikali kila baada ya miaka mitano ya kuomba kura huwa ni malipo ya elimu bora,afya bora na huduma bora za maji na maisha.

Serikali imekuwa mdau mkubwa wa kutokufuata masharti haya ya "Social Contract" kati yake na wapiga kura.Kuwepo na ukosefu wa shule za serikali ktk kumi bora,ni moja ya uvunjwaji mkubwa wa "mkataba wa kijamii" kati ya serikali na wananchi.Na hapa Serikali inapswa kuadhibiwa.

Unawekaje kipimo sawa kati ya mwanafunzi anayesoma kwa kibatari na chemli kule Iselamagazi Tabora na yule anafanya study Tour Uturuki huku akiwa na mazingira bora ya kusoma?

Na hili kudhihirisha hivyo,kwa sasa huwezi kukuta viongozi wa serikali wakipeleka watoto wao ktk shule za serikali kwa maana na wao hawaamini ktk ubora wa elimu inayotolewa na shule za umma.

Ilboru,Tabora Boys,Mzumbe,Kibaha,Weruweru,Tabora Girls,Kilakala,Msalato na Korogwe Girls zimebaki magofu ya historia ya elimu bora ya Tanzania.Majengo ni toka ya mkoloni.Hakuna jitihada za kimkakati za kurudisha ubora.

Elimu imekuwa biashara badala ya Huduma.Na hao watunga sera wanaopaswa kuirudisha elimu ktk mstari mnyoofu ndio wafanyabishara wa elimu.Waziri anamiliki shule,mbunge anayeisimamia serikali nayeanamiliki shule au kuwa na hisa ktk biashara ya elimu.

Katika nchi zilizoendelea,Elimu ya msingi na upili sio biashara,bali ni huduma.Ni huduma kwa sbb ni haki ya kimsingi ya kila mtu kupata elimu ya msingi na ya upili.Ndio maana nchi kama Sweden ni fahari kuwa sehemu ya shule ya serikali kuliko binafsi.

Mazingira ya kielimu ya mtoto aliyeko Kwa Msisi Handeni,ambapo zaidi ya kuwaza masomo,anawaza wapi atapata maji ya kuoga na kunywa si sawa na Marian Girls,ambapo mpaka pedi mtoto anaikutq kati vyoo vya shule,hawa hawawezi kuwa sawa kieleimu na kimtazamo.

Hii ni sawa na kuwaweka ulingoni Dula Mbabe anyecheza ngumi za amacha na Myweather katika mizania sawa ya ngumi.
Its like feather weight boxer vs heavyweight boxer!!Kwa hili tujitathmini upya
 
Nchi hii kila mtu mbabe, kila anayekuja uongozi ukibadilika huleta maafa kwenye sekta hii ya Elimu. Enzi zetu mwanafunzi akifaulu kwenda Ilboru unajua kweli alikuwa kichwa.
 
Nipo najadili hapa....vitu tulivyojifunza kwenye shule za ufundi enzi hizo...leo hii hakuna kitu...shule zote zimekwisha....
Mkuu shule za ufundi zote karakana zimebaki maghofu tu
Ukienda pale Ifunda Tech utalia,achilia mbali Mbwiru na Mbeya Technical.

Wakati huo kijana alikuwa anafika kidato cha nne anaweza kufanya wiring kwenye nyumba,kama aliamua kuchepuka na ufundi bomba,basi anakutengenezea mfumo wa maji ndani ya nyumba.Vijana wa ufundi uwashi na useremala haukuwapiga chenga.

Kuna mahali tumepotea,turudi ktk misingi ya Elimu ya Kujitegemea!!Vinginevyo tutakuwa na Taifa la hovyo sana huko mbeleni.
 
Lema aliposema "watoto wa maDC, maRC, mawaziri, wabunge, matajiri, na watu wenye upeo mkubwa wanasoma kwenye shule nzuri na hata nje ya nchi;watoto wa walala hoi...." mlitukana. Haya endeleeni na shule zenu za majaribio.
Ila msisahau kuchimbua majina na familia za hao wanasimika A's masomo yote kama kuna wale wa wadanganyika basi ni bahati mbaya sana.
 
Enzi za mwalimu tuliaminishwa na kuamini hata sisi walimu kuapa kuwa elimu ni kioo na mstakabali wa taifa. Who cares now?

Tupo hapa kwa sababu ya elimu ya mwendo kasi.
tatizo faza nae alikua muongeaji kuliko mtendaji,ila elimu imeanza kuanguka 98 huku,ilikua inaharibika taratibu,hasa walofaulu kwa tuition halafu leo ndo walimu
 
Kama tatizo ni walimu mahiri wa masomo mbalimbali kwenye hizo shule,serikali itangaze nafasi za ajira au masomo(rectrutment) kujaza upungufu.Mitaani kuna watu wenye uwezo wa kufanya wonders,maarifa na ujuzi wao unapotea bure bila kutumika wakati kuna matatizo ya kutatuliwa huko mashuleni.Shule za binafsi wako panctually na elimu na wanajua na kuthamini uwezo binafsi wa walimu wao(competence).Ni vizuri ajira ya ualimu serikalini ikaombwa kwa kufanyiwa usaili badala ya kupangiwa kituo tu baada ya kufaulu mtihani.Na usaili uwe ni endelevu siyo ukaguzi uliozoeleka.Mwalimu akisikia ukaguzi unakuja shuleni kwake anaji keep busy kuandaa zana za kufundishia,wakiondoka na yeye anabaki katika hali ya business as usual.Sasa kwa hali hii matokeo mazuri yatatoka vipi? Mitaani kuna watu wenye ujuzi waitwe na wapewe kazi kwa faida ya taifa.
 
Siku hizi bila pesa hakuna elimu bora,, hata viongozi wanajua hilo ndio maana wanapeleka watoto wao shule binafsi.. mwenye nacho anazidi kuongezewa.. twafaa
.
 
Nakumbuka yule mtoto aliyekuwa wa kwanza kwenye mitihani ya kidato cha nne alivyopolekwa hadi Bungeni ili kuzima hoja kwamba shule za kata hazikidhi viwango vya kutoa elimu.
 
Kwa sasa suala la Elimu ya Msingi na ile ya Upili imekuwa ni jukumu la sekta binafsi
Sekta binafsi ndio inajenga mazingira bora ya elimu na watoto kufanya vizuri kuliko serikali.

Lakini "Social Contract" kati ya wananchi na serikali kila baada ya miaka mitano ya kuomba kura huwa ni malipo ya elimu bora,afya bora na huduma bora za maji na maisha.

Serikali imekuwa mdau mkubwa wa kutokufuata masharti haya ya "Social Contract" kati yake na wapiga kura.Kuwepo na ukosefu wa shule za serikali ktk kumi bora,ni moja ya uvunjwaji mkubwa wa "mkataba wa kijamii" kati ya serikali na wananchi.Na hapa Serikali inapswa kuadhibiwa.

Unawekaje kipimo sawa kati ya mwanafunzi anayesoma kwa kibatari na chemli kule Iselamagazi Tabora na yule anafanya study Tour Uturuki huku akiwa na mazingira bora ya kusoma?

Na hili kudhihirisha hivyo,kwa sasa huwezi kukuta viongozi wa serikali wakipeleka watoto wao ktk shule za serikali kwa maana na wao hawaamini ktk ubora wa elimu inayotolewa na shule za umma.

Ilboru,Tabora Boys,Mzumbe,Kibaha,Weruweru,Tabora Girls,Kilakala,Msalato na Korogwe Girls zimebaki magofu ya historia ya elimu bora ya Tanzania.Majengo ni toka ya mkoloni.Hakuna jitihada za kimkakati za kurudisha ubora.

Elimu imekuwa biashara badala ya Huduma.Na hao watunga sera wanaopaswa kuirudisha elimu ktk mstari mnyoofu ndio wafanyabishara wa elimu.Waziri anamiliki shule,mbunge anayeisimamia serikali nayeanamiliki shule au kuwa na hisa ktk biashara ya elimu.

Katika nchi zilizoendelea,Elimu ya msingi na upili sio biashara,bali ni huduma.Ni huduma kwa sbb ni haki ya kimsingi ya kila mtu kupata elimu ya msingi na ya upili.Ndio maana nchi kama Sweden ni fahari kuwa sehemu ya shule ya serikali kuliko binafsi.

Mazingira ya kielimu ya mtoto aliyeko Kwa Msisi Handeni,ambapo zaidi ya kuwaza masomo,anawaza wapi atapata maji ya kuoga na kunywa si sawa na Marian Girls,ambapo mpaka pedi mtoto anaikutq kati vyoo vya shule,hawa hawawezi kuwa sawa kieleimu na kimtazamo.

Hii ni sawa na kuwaweka ulingoni Dula Mbabe anyecheza ngumi za amacha na Myweather katika mizania sawa ya ngumi.
Its like feather weight boxer vs heavyweight boxer!!Kwa hili tujitathmini upya
Umenena lakini hili halitatatuliwa kwa kuzivuta shule binafsi zije kwenye level zilipo shule za umma kama inavyotaka kufanyika. Bora tuziache tu hizi taasisi binafsi bila kuzibugudhi kutoka kwao tunaweza kuokoa mawili matatu. Serikali ikumbuke elimu bora ni gharama na hii iwe kwa wazazi pia. Tuwekeze kwenye elimu bora, bure ni ghali.
 
Back
Top Bottom