Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,809
- 34,193
KWA MARAFIKI ZANGU NA FAMILIA NZIMA YA FB, TWITTER, INSTAL.., JF NA MF.
Mambo muhimu ya kuepuka usikabiliane na mkono wa sheria ya mitandao inayoangamiza vijana wengi sana hasa wanaotoa "maoni" yaliyo kinyume na watawala.
1. Epuka Kusambaza ujumbe wa uchochezi ama ushawishi wa kisiasa unaoweza kuleta athari kwa jamii yetu kupitia mitandao
2. Epuka Kusambaza au kutunga ujumbe unaoleta uchochezi wa kidini unaoweza kupelekea kuvuruga amani na maelewano kwa jamii kupitia mitandao.
3. Epuka Kusambaza picha ama video za utupu ama zilizokosa maadili kwa jamii kupitia mitandao mbalimbali ( Whatsapp, Facebook, YouTube, Instagram n.k)
4. Epuka Kusambaza picha ama video za uchochezi wa kidini ama kisiasa kupitia makundi mbalimbali ama mitandao ya kijamii.
5. Epuka Kushiriki kusambaza chochote kati ya vilivyotajwa hapo juu (kutuma kama ulivyopokea ) itakugharimu
6. Epuka Wizi kupitia mitandao mbalimbali na mitandao ya simu utakugharimu.
7. Epuka Kumpatia mtu line yako ya simu na kutumika kufanyia wizi ama utapeli itakugharimu.
8. Epuka Kushiriki kumchafua mtu,taasisi,kikundi cha watu kwa namna yoyote kupitia mitandao pia itakugharimu.
9. Epuka Kupoteza simu bila kutoa taarifa na kufunga mawasiliano hayo yanaweza kupelekea kutumika kufanya uhalifu na ukaangukia hatarini.
10. Epuka Kutumia mtandao kwa utapeli kupitia 'brand' ama jina la mtu itakugharimu
Hukumu.
MUHIMU:
Kosa la aina yoyote linalotambuliwa na sheria hii adhabu yake ni kifungo cha miaka kadhaa gerezani ama faini ya fedha isiyopungua milioni 5 kulingana na kosa lililofanyika (au vyote!)
Kutokujua sheria hakuzuii wewe kuadhibiwa ukiivunja.
Ubovu wa sheria sio iwe chanzo cha wewe kuivunja, makali ya sheria yapo palepale mpaka siku RAIS atakapoitengua.
Kwamjibu wa Sheria ya Makosa ya Mitandao ya Kijamii ya mwa 2015, kifungu cha 16, Kila mtanzania ama awaye yoyote anayetumia internet au simu ya kawaida ni mtuhumiwa mtarajiwa, ni muda tu unamsubiri kufikishwa mahakamani.
Juhudi za ukombozi wa nchi hazijawahi kuzimwa kwa sheria kandamizi wala gereza!
chanzo.Na: Yericko Nyerere