Kwa mara ya kwanza simu za kiganjani zilitumika mwaka gani hapa Bongo?

Ebu chagua hapo aiseeee
1456684199975.jpg
 
Kampuni ya kwanza ni mwaka 1992 au 1993 tukianza na mtandao wa mobitel. Handset peke yake gharama yake ilikuwa Shs. 1m. Ulifuatia mtandao wa Tritel kabla akina Vodacom kuingia muda mfupi baadae.
Usisahau Tritel ndio ya mwaaanzo kabisa ila haikudumu sana!
 
Kampuni ya kwanza ni mwaka 1992 au 1993 tukianza na mtandao wa mobitel. Handset peke yake gharama yake ilikuwa Shs. 1m. Ulifuatia mtandao wa Tritel kabla akina Vodacom kuingia muda mfupi baadae.
Vocha ilikuwa inauzwa kwa dola na ilikuwa hata ukipigiwa unakatwa na kulikuwa pia na monthly charges hata Kama hujatumia kabisa simu yako
 
Nilianza kutumia nokia 3310 aka jeneza mwaka 2001. kipindi hicho sms zinaanza ikawa bure watu wakawa hawapigi simu ni mwendo wa texts tu. Baadae wakaanza kucharge sms. Nakumbuka kununua line ilikuwa bei mbaya. Kuna siku Shivacom wakatoa line bure za voda pale samora palijaa watu wa kufa mtu. Watu wanatoroka maofisini kwenda kuchukua line ya bure. Dah maisha haya
 
Usisahau na Philips survey mkuu
Hahaha yes kulikua na Philips survey ilikua kubwakubwa hivi nyeusi. Hahaha balaa ilikua enzi hizo. Ilikua ni mwendo wa Phillips, Siemens na Nokia. Halafu ikaingia erricksson. Ila bwana hizo zote zilikua original ya kufa mtu hapakua na mchina pale. Siemens ilikua Germany. Nokia ilikua Hungary na Germany. Erricksson ilikua kutoka Sweden. Phillips nimesau ilikua inatoka wapi.
 
Zile ericksson zenye mwanga wa bluu zilisumbua sana.
 
Ukweli ni kwamba ni mwaka 1994 na huu mwaka siwezi kuusahau coz' nikuwa nimepata ajali August 1994 siku ya mpano kati ya Simba & Pamba! Sasa baada ya kulala kitandani kwa wiki kadhaa, nilipopata nafuu nikawa nainuka kuchungulia dirishani! Hapo nikawa naziona UDA zinapita zimeandikwa MOBITEL! Kila UDA imeandikwa MOBITEL.... nikawa nashangaa tu what's Mobitel!!! Kwahiyi zitakuwa zimeanza ama mwezi August 1994 mwishoni au September 1994!!!!
 
Back
Top Bottom