Kwa mara nyingine tena, hapa ndipo anapokosea Rais Magufuli

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,226
3,290
Mwanzoni tulifikiri labda anaweza kujirekebisha baadae lakini hadi sasa anazidi kuharibu. Tanzania tokea kuingia madarakani kwa rais Magufuli kumeibuka maamuzi mengi yanayotikisa na mara zote tunaaminishwa kuwa hufanywa maamuzi hayo kwa uzalendo mkubwa wa Rais wetu.

Alianza na kutumbuwa bandarini, na kuna wafanyakazi walisimamishwa wengine kwa maamuzi ya hadharani na kunasibishwa na upigaji dili kabla ya uchunguzi kufanyika. Kuna makosa yalifanywa watu waliharibiwa wasifu wao na kuchonganishwa na jamii kwa kauli tu zisizostahi utaratibu wa kiutumishi. Hili pia liliwagusa watendaji wengine kadhaa ama kwa kutenguliwa na wengine kuahidiwa kupangiwa kazi nyengine.

Lengine ni sakata la ufisadi na kuundwa kwa mahakama hiyo. Rais alituaminisha kuwa kuna ufisadi wa kutisha na kuunda mahakama kwa gharama na kwa haraka lakini baadae wenye dhamana wakaja hadharani kutwambia hakuna kesi za mafisadi. Rais JPM anafanya kosa la kukurupuka kila wakati ambapo kwa maoni yangu anaanzisha jambo kwa nguvu zote na kuaminisha jamii kwamba yuko vizuri na hatimae anapoteza credibility kila uchao.

Huu ufisadi umemshinda na kinachoonekana ni visasi tu. Mifano iko mingi ya waliohusika na ufisadi na wizi na hata kusemwa katika vyombo vya dola kama bunge na kutolewa maazimio. Mimi nilifikiri haya ndiyo ilikuwa aanze nayo mfano kuna ESCROW. Liko wazi kabisa lakini kalikwepa.

Kuna kishindo cha vyeti feki ambapo watu kadhaa walichukuliwa hatua na Rais aliahidi kuwashughulikia wote. Lakini kwanza kazi hii nayo imeguswa na kuachwa na tayari imeharibika kama ilivyoharibika ajenda ya ufisadi. Kuna kupendeleana na ubaguzi. Baadhi ya kada haziguswi na taasisi nyeti zimeachwa. Hakuna usawa na uzalendo kuna majungu na visasi kwa baadhi ya makundi. Katika hili tunaambiwa leo eti wanasiasa hawamo, baadhi ya vikosi vya ulinzi havimo na kuna undumi lakuwili. Polisi wanachunguzwa na taarifa zinatolewa lakini jeshi la Ulinzi wao haliwahusu. Huo uzalendo wa kuwagawa watu unatoka wapi ?

Kuna suala la madawa ya kulevya nalo limeharibiwa tayari, ilitumika nguvu kubwa kuliibua na limeishia isivyotarajiwa, Bado tatizo lipo na ile misingi haijaguswa. Rais JPM kalirukia hili suala nyeti na kuliharibu na sasa linaelea.

ANAPOKESEA RAIS JPM

Mara zote anakosea kujua pa kuanzia. Inawezekana hana nia ya dhati au hashauriki na hivyo huamua kujitosa yeye mwenyewe kwa kuliibua jambo ambalo halina mikakati. Mara ngapi Rais anaibua issue lakini hafiki hatua hata mbili kunaonekana mapunguifu ama ya kisheria au ya kiutumishi na suala hilo hupoteza haiba kwa haraka ?

Hapo ndipo anapokosea Rais wetu. Hatimae mambo makubwa yanapotea bure kwa kukosa mikakati na kujuwa pa kuanzia.

Hajui pa kuanzia na hatimae hajuwi pa kumalizia. Kwa ufupi Rais wetu amekosa mwelekeo yote aliyoanzisha hayana misingi na kitu kikikosa misingi hakidumu kitapotea na kuanguka tu.

FAIDA.

Rais anaibuwa hoja na hatatuwi tatizo huu ndio ukweli. Na kwa kuibuwa hoja hizi bado hajaonesha mpya, akumbuke wapinzani walishaibua zamani na walipuuzwa na akiwemo yeye Magufuli wakati alipokuwa anatetea chama (CCM) kuliko nchi. Wakati ule alikuwa kimya leo anatuaminisha kuwa ni mambo mapya. Rais hapa anafanya siasa za kizamani. Rejea hoja za mikataba ya madini, Ufisadi n.k.

UZALENDO.
Kwani nani mzalendo ? jee mzalendo ni Rais tu kwa kuwa ndio kawa Rais ? hii dhana inavurugwa ili kujinufaisha kisiasa. Uzalendo ni pamoja na kusimamia sheria, kuziandaa sheria kulinda rasilimali za nchi na kutenda haki. Uzalendo si kupitisha sheria fyongo halafu ukaja kulia baadae eti nchi inapigwa. Kwani ulikuwa wapi ? Uzalendo ni asili ya mtu si maigizo kwa kuwa umekuwa Rais, mbunge au jaji. Uzalendo unaishi na haupotei kwa matukio.

WAPI PA KUANZIA NA NINI KIFANYIKE.
Pa kuanzia panaeleweka na naamini hata Rais JPM anapaelewa. Kuna pahala kama nchi tumejikwaa tukiri CCM ilituingiza Chaka huo ndio ukweli. Tatizo ni CCm na vyombo vyake kuanzia kwenye chama, bunge na wasomi wake. Chama kilishindwa kuiongoza serikali kuweka misingi ya kulinda nchi na rasilimali zake. Bunge lilishindwa kudhibiti ukada na likapitisha miswaada ovyo na kukomoa wapinzani hatimae nchi leo imeliwa. Wasomi wa CCM walishindwa kukosoa.

Tufanye na tutunge katiba mpya yenye mwelekeo mpya wa kuijenga Tanzania. Kupitia hili viwanda vitapatikana na rasilimali zitalindwa. Rasimu ya warioba irejeshwe na iboreshwe ikionekana kuna haja. Nje ya hapa Kingozi yoyote anaetokana na CCM amepoteza uhalali wa kuhoji ufisadi, kuporwa, mikataba na rasilimali zetu. CCM kaeni kimya na rais JPM anyamaze.

Tunahitaji jambo jipya kama taifa walau CCM na JPM zungumzeni Katiba mpya watanzania watawaelewa. Ufisadi, mikataba mibovu, rushwa, madawa ya kulevya na vyeti feki hayo ni matunda ya CCM kwa kuongoza nchi hadi sasa.


Rais Magufuli anapajuwa anapokesea. Akipatia wote tutamsifu lakini si kwa haya ya machozi ya mamba.


Kishada.


cc Lizaboni and Co.
 
Huyu bwana hii nchi keshahiaribu kbsa. Ajira kafuta, uhakiki ulifanyika kwa ubaguzi (hapa keshagawa taifa), fao la kujitoa halipo, rambi rambi zina.liwa hadharani bila aibu, increment nayo ilipigwa panga mchana kweupeeeeeeee ni shida. Huyu bwana keshahiaribu hii nchi, tunaishi basi tu
 
Inaonekana unajua sana kukosoa, nakushauri jiandae 2020 upate nafasi ya kugombea ili uje uongoze nchi hii
 
Atleast wewe uliyeleta mada umejitoa muhanga kumfunga kaka kengele.....nashukuru pia umejitahidi kuonyesha mapungufu katika kila move anayoichukuwa mkuu....
Kinachonisikitisha ni aina ya watu na hasa makada wa chama kumwona mkulu kama mungu mtu na hatakiwi kukosolewa sababu hajazaliwa wala kuumbwa kufanya makosa.
Ni ujuha wa kiwango cha juu sana kuendelea kumwamini mtu ambaye kila move anayoifanya inakuwa na mapungufu kimkakati hata kama haijatekelezwa...tutazidi kama taifa kuangukia pua na kurudi nyuma kiuchumi kama hatutokubali utamaduni wa kukosoana na kukubali mawazo mbadala.
 
Tatizo kubwa mi ccm yote wanamwogopa mno Magu
Kwa kuwa hasikizi wapinzani basi huko fisiemu hakuna wa kumwambia chochote zaidi ya kumsifia na kumuacha apuyange na kututokomeza kusiko julikana
 
Atleast wewe uliyeleta mada umejitoa muhanga kumfunga kaka kengele.....nashukuru pia umejitahidi kuonyesha mapungufu katika kila move anayoichukuwa mkuu....
Kinachonisikitisha ni aina ya watu na hasa makada wa chama kumwona mkulu kama mungu mtu na hatakiwi kukosolewa sababu hajazaliwa wala kuumbwa kufanya makosa.
Ni ujuha wa kiwango cha juu sana kuendelea kumwamini mtu ambaye kila move anayoifanya inakuwa na mapungufu kimkakati hata kama haijatekelezwa...tutazidi kama taifa kuangukia pua na kurudi nyuma kiuchumi kama hatutokubali utamaduni wa kukosoana na kukubali mawazo mbadala.
Ok.

Kuna watu hawajui tunajadili nini hapa.
 
Nchi hii ina maajabu kweli. Hivi leo rais Magufuli anamlalamikia nani kuhusu kupigwa kwa nchi ? hawajui waliokuwa na dhamana ? Halafu anataka kuiingiza nchi kusikojulikana wakati tatizo analijuwa na analiacha. Baya zaidi anataka tumeze neno UZALENDO kuwa ni kila anaehoji maigizo au maamuzi yake.

Hangaikeni na chanzo cha tatizo sio matokeo.
 
Back
Top Bottom