Jamani wanajamii mimi kuna kitiu kinanishangaza sana kwa haya makampuni ya vinywaji unakuta wanamrestrict mwenye bar kuuza vinywaji vyao tuu ili wampe viti na meza sana sana hii nimeiona kwa kampuni ya pepsi na coca je ni sahihi hili kwa wateja?kwa makampuni ya bia bado sijaona hili likiendelea.wanajamii hii kweli ndio mambo ya marketing au ni ujinga wetu.
Kwa sababu mnawanyima uhuru wanyaji au wateja
Kwanza mimi nina kesi na hao coca, nimenunua soda ndani ina kizibo ambapo imeni-risk saana. ninayo na nitaita press conference nitoe madai ya kampuni hiyo kuniuzia soda ambayo ipo sealed na sijaifungua, kizibo kipo ndani.
BACK KWENYE MADA: Makampuni hayo yapo kiushindani zaidi na wana strategic limitations sokoni ndio maana unaona hivyo.
Jamani tujitahidi pia kupitia vitabu vya sheria mbalimbali. Cha kwanza mwenye biashara yake akiamua kuuza bidhaa za aina moja tu hakatazwi na wala hakamatwi na mtu. Almuradi idhibitishwe hakuna mkataba wowote wa ki maandishi unaomlazimisha afanye hivyo. Atakuwa anajipunguzia tu revenue zake. Kuhusu kukutwa kitu kwenye chupa ya kinywaji chochote,hauna uwezo wa kudai ulipwe damage yeyote kisheria mpaka itakapothibitika kitaalamu na kisheria kuwa ni kinywaji hicho na kitu kilichomo ndani yake(na si kitu kingine whatsoever) ndivyo vilivyo kudhuru afya yako. Ukiita press kitakachofanyika atakuja public relation manager na QC manager, wataelezea vizuri ni jinsi gani probability ya kukuta kizibo au kitu chochote kwenye kinywaji huwa inatokea na atakupa mpaka degree of confidence kuwa huwa inakuwa + or - something ambayo TBS na TFDA huwa wanaikubali kitaratibu zao. Haujamaliza nauli za kwenda na kurudi mahakamani hapo?. Labda katiba mpya inayokuja itaangalia kiundani pia consumer rights hapa tz na kurekebisha vipengele ambavyo vipo loose.