Kwa mahitaji ya nyumba au chumba cha kupanga Mwenge, Sinza, M/nyamala na Mbezi

Tunzo

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
4,065
2,362
TMPDOODLE1495634587583.jpg Kama unahitaji nyumba maeneo hayo ya chumba au nyumba ya kuanzia chumba na sebule au kuanzia vyumba viwili na kuendelea usisite kunitafuta, maeneo ni hayo ya Mwenge, Kinondoni, Sinza, Kijitonyama na Mbezi Tangibovu mpaka Makonde na Makongo juu, Tabata, Tegeta, Bunju, wazo,

Pia Shekilango, Urafiki na Ubungo maziwa zipo, Baruti, kimara, temboni, Mbezi mwisho goba wote karibuni

Chumba kimoja moja kipo, chumba na sebule, master, nyumba nzima zipo karibuni.

Namba 0713415537 (ipo whatsapp). Fremu za biashara zipo pia.

TUSOME HUU UJUMBE

Habari wana jamvi!

Nimeona leo kulizungumzia japo kwa ufupi kuhusu swala potofu juu ya madalali wa nyumba za kupanga, kumekua na malalamiko mengi kuhusu madalali wa nyumba/vyumba kupandisha bei halisi ya nyumba au chumba ili kupata cha juu, niwaambie tu dalali yoyote wa nyumba ya kupanga hahusiki kabisa kwenye bei ya pango, dalali wa kupanga si kama wa kiwanja, nyumba ya kuuza au magari nk. Dalali wa nyumba yakupanga anachoangalia ni mteja kuingia apate ile ya mwezi mmoja kulingana na bei ya nyumba kwa mwezi, wakati mwingine dalali anahusika kumshawishi mwenye nyumba ili ampunguzie mteja kama mteja kafikia kiwango flani, na wakati mwingine anamwambia mwenye nyumba kwa bei yako nyumba itaka sana ni heri upunguze, chukulia mfano nyumba ni ya 300k mteja ana 280k mimi ninachoangalia ni mteja kupanga ili nipate ile ya mwezi, hapo lazima nitaungana na mteja kumwambia mwenye nyumba hali ni mbaya mpunguzie mteja, kwaniyo nyumba ya 300k hata siku moja dalali hawezi kukuambia ni ya 400k hilo sahau, Dalali anatamani nyumba ya 300k mwenye nyumba ashushe 200k ili apate wateja haraka, kumbuka madalali wako wengi, kama ni mteja wa uhakika nisipomshawishi bosi apunguze mteja alipie, badae dalali mwingine akileta nakosa hata ile, kwahiyo swala la kwamba dalali anahusika kwenye swala la kupanga bei halipo, naamini wenye nyumba tunakibaliana na hili na madalali pia,

Wengi wamekua na kawaida sana ya kuwatukana na kuwaponda madalali ila kumbuka wengi wamekua msaada kwa watu kupata nyumba, kama hutaki kuwatumia madalali basi nyanyuka kwenye kiti chako ofisini hapo kazunguke mtaa kwa mtaa kutafuta nyumba ambayo ipo wazi upange,

Kumbuka nakubaliana sana na wazo kua ni lazima madalali wasajiliwe ili kufanya kazi kiufanisi na weledi, na pia kutafuta mfumo mzuri ambao hautaleta vikwazo kwa dalali, mpangaji na mwenye nyumba, kwahiyo nakubaliana kabisa na wazo la kuunda vyama vya madalali na kusajiliwa!

Pia nakubaliana na kuwapa pole waliosumbuliwa na madalali, kumbuka sijakataa kama ni kweli wapo matapeli, wazenguaji, pia waswahili, na ni kweli inasikitisha pale dalali anapompamba mteja kua nyumba kali ipo wahiii itaondoka, mteja akija anakuta banda la kuku, hii ni kwasababu wengi hawajaelewa kua wakifanya hii kazi kwa weledi ni manufaa kwao, wengi wamekua wanaangalia tu pesa ya hapa na pale ya kula na si kuboresha kipato!
Kumbuka si wote binadam wanafanyana, kila kitu kina changamoto zake, kikubwa ni kupunguza changamoto!
 

Attachments

  • TMPDOODLE1495634644645.jpg
    TMPDOODLE1495634644645.jpg
    38.7 KB · Views: 1,033
  • TMPDOODLE1495634701503.jpg
    TMPDOODLE1495634701503.jpg
    26.9 KB · Views: 961
weka na picha at least utapata wateja
Mkuu kama mtu yupo serious anahitaji nyumba atanicheki nyumba zipo nyingi na vyumba vipo vingi hata nikisema napost kila nyumba hapa haina maana na mfano naweka picha hapa then jioni inachukuliwa kwesho mteja anakuja namuonyesha nyingine unadhani itakuaje?

Naamini wakuu niliowapatia nyumba hapa au walionitafuta wataleta ushuhuda.. I just need serious ones, mtu atakaechangia kwa kuponda na kaona namba najua tu sio muhitaji, By the way I have 1 room in my place,here at mwenge near TRA only 90,000/month for 1year hiki hakina dalali mimi ndo faza house mtu akikipenda poa ila nikikupeleka vingine lazima unipe udalali
 
Mwenye kuhitaji nyumba maeneo ya msasani ani PM
 

Attachments

  • 1462332119748.jpg
    1462332119748.jpg
    85.4 KB · Views: 910
Mi naitaji maeneo ya gongo la mbotobtabat kimanga au airport.. chumb kikubwa mazingira mazuri bei kuanzia 25,30,35 mwisho 40 .
 
Hii ni moja ya sekta nyeti sana ambayo inatakiwa kuunganishwa na uhamiaji, usalama wa taifa, TRA na wizara ya lukuvi. Watu wanapiga kazi wanapata hela bila kulipa kodi, wengine ndo hivyo tena wageni wanakuja wanaishi bila vibali etc.
 
Kama unahitaji nyumba maeneo hayo ya chumba au nyumba ya kuanzia chumba na sebule au kuanzia vyumba viwili na kuendelea usisite kunitafuta, maeneo ni hayo ya mwenge,sinza,kijitonyama, na mbezi tangi bovu mpaka makonde na makongo juu pia namba ni 0713415537
Nataka chumba Kinyerezi.sana sana kiwe cha ndani ya uzio hasa detachment ya Kwenye familia Kwa usalama. Bei reasonable kwani mi mwanafunzi
 
Mataka chumba Kinyerezi.sana sana kiwe cha ndani ya uzio hasa detachment ya Kwenye familia Kwa usalama. Bei reasonable kwani mi mwanafunzi
Sawa kwa kinyerezi sina mkuu ila nitakuulizia, mimi nipo zaidi mwenge, sinza na mbezi beach
 
Penye rizki hapakosi fitina.
Hii siyo fitina mkuu asrams. Ni mawazo ya kuboresha sekta ya udalali ili wengi wao watambulike na wawe msaada zaidi. Chukulia dalali awe na TIN number, awe na kijisehemu chake cha kuacess (user interface) katika mfumo wa immigration system, awe na ramani ya sehemu husika (GPS)...

Na katika kulipia pango la nyumba, mwenye nyumba aweze kulipia kodi pia etc. Hapo hakuna fitna na siwezi kufanya fitna bali nikutoa mawazo ya kuboresha mfumo, siko huko ulikowaza na sina connection ya kazi zangu na hiyo kazi.
 
Back
Top Bottom