Yusomwasha
JF-Expert Member
- Dec 5, 2014
- 2,092
- 838
Habari wakuu
Nimekuwa moshi kwa takriban wiki kadhaa sasa nimetembelea rombo,marangu,old moshi,kibosho,machame,masama,na,siha.
Kiukweli hawa jamaa wachaga sijapata kuona tangu nizaliwe
Nimeyaona maendeleo makubwa sana huko kwao.
Nimetembelea vijijini kwao nimekuta barabara nzuri, nyumba za kisasa na magorofa, maji ya bomba na umeme kila nyumba, huduma nzuri za afya, mashule ya kutosha pamoja ni mipangilio mizuri ya makazi.
Nimebaki nikistaajabu sana hawa jamaa kweli huwa hawasau kwao kwa maendeleo wako vizuri.
Ukikaa huku nahisi niko ulaya kwa maendeleo makubwa ya kutisha
Wanawake wachapakazi, wavumilivu nimewaona huku,
Mashamba yalostawi ya kahawa na migomba kiukweli panavutia.
Huku pia kuna mifereji ya kutosha ya maji ambayo hutumika kwa kilimo cha mazao kama nyanya, na mboga za majani na pia hutumika kumwagilia migomba na mikahawa mara kwa mara.
Kwa kweli wanastahili pongezi
Wenzetu hawa hawasubiri serikali iwafanyie yote hayo bali hujitoa kwa nguvu zao zote kugaramia miradi yao kama barabara, shule, hosptali na mengine mengi.
Excellent wachaga yaani mpo vizuri naomba watanzania wote tuige mfano kwa hawa ndugu zetu.