Kwa madaktari tuu

Software Engineer

JF-Expert Member
Dec 20, 2014
344
137
Naomba Category ya magonjwa yanayowapata/tibiwa/ripotiwa mara kwa mara katika hospitali za Tanzania.

Itapendeza nikipata na kiswahili cha kila category ya kiingereza utakayotoa.

Mfano
1. Cardiology ... MOYO
2. Gynacology ... WANAWAKE

Asante kwa mchango wako
 
Nani kakwambia gynecology ni wanawake..!?

yah..ni kwa wanawake na wasichana mkuu........tuseme ni science of functions and diseases zinazo/yanayo wahusu ao watu... based esp. on their reproductive systesms /organs
ama theres something tofauti na hapo mkuu???
 
yah..ni kwa wanawake na wasichana mkuu........tuseme ni science of functions and diseases zinazo/yanayo wahusu ao watu... based esp. on their reproductive systesms /organs
ama theres something tofauti na hapo mkuu???
Ulivokua umeandika mwanzo nilistuka ungeandika "uzazi"
 
Naomba Category ya magonjwa yanayowapata/tibiwa/ripotiwa mara kwa mara katika hospitali za Tanzania.

Itapendeza nikipata na kiswahili cha kila category ya kiingereza utakayotoa.

Mfano
1. Cardiology ... MOYO
2. Gynacology ... WANAWAKE

Asante kwa mchango wako

TOP TEN DISEASES IN TANZANIA

  1. SHINIKIZO KUBWA LA DAMU/KITAALAMU BLOOD PRESSURE
Maana ya Shinikizo kubwa la Damu: Ni ongezeko la nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa inayochukua damu kutoka kwenye moyo kwenda kwenye viungo na tishu mwilini.

Ukubwa wa shinikizo hilo la damu utegemea wingi na nguvu ya msukumo wa damu kutoka kwenye moyo na ukubwa wa mishipa inayopeleka damu mwilini.

Kiwango cha kawaida cha shinikizo la damu mwilini ni 120/80mmHg au chini yake. Pale kiwango kinapokuwa 140/90mmHg au zaidi hali hiyo huwa ni shinikizo kubwa la damu.

Dalili: Kwa kawaida hakuna dalili za wazi zinazojitokeza pale ambapo una shinikizo kubwa la damu. Utafahamu kama una shinikizo kubwa la damu kwa kupimwa na mtaalamu katika kituo cha tiba. Endapo shinikizo lako la damu litakuwa liko kiwango cha juu sana unaweza:

  • Ukaumwa kichwa mara kwa mara hasa sehemu ya kisogo
  • Kutokwa na damu puani
  • Ukapata kizunguzungu
  • Kupata maumivu ya kifua
  • Moyo kwenda kasi wakati umepumzika
  • Kushindwa kufanya mazoezi kwa kushindwa kupumua
  • Kusikia mapigo ya moyo wako wakati umepumzika
  • Na kupata uchovu wa mara kwa mara.
Muda wa tatizo: Kwa bahati mbaya watu wengi huishi na tatizo hili kwa muda mrefu bila kufahamu kwani hakuna dalili zilizo bayana. Mara nyingi shinikizo kubwa la damu hutambulika pale unapokwenda kituo cha huduma ya afya kupima afya yako au kupata matibabu ya tatizo jingine la kiafya. Hali hii humweka mtu katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo hivyo ni muhimu kuwa na tabia ya kupima afya yako mara kwa mara.

Sababu: Sababu hasa za shinikizo kubwa la damu kwa sehemu kubwa hazijulikani. Hata hivyo shinikizo la damu hubadilika mara kwa mara kutegemeana na shughuli mtu anayofanya, hali ya joto, chakula alichokula, hali ya msongo wa mawazo, ukiwa umelala au kusimama na hata matumizi ya baadhi ya dawa.

Watu wenye umri wa miaka 45 au zaidi wako kwenye hatari zaidi ya kupata shinikizo kubwa la damu kutokana na mabadiliko yanayotokea katika mishipa yao ya damu. Vilevile mafuta, lehemu au madini ya chokaa yakizidi mwilini huwa na tabia ya kujikusanya katika kuta za ndani za mishipa ya damu kidogo kidogo na kusababisha mishipa hiyo kuwa nyembamba na hivyo kupunguza uwezo wake wa kutanuka. Hali hii huchangia kwa kiasi kikubwa kupata shinikizo la damu.

Viashiria vya shinikizo kubwa la damu: Mambo yanayoongeza uwezekano wa kupata shinikizo kubwa la damu ni pamoja na:

  • Kuwa na historia ya shinikizo la kubwa la damu katika familia yako
  • Kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40
  • Kuwa na jinsia ya kiume (huwapata wanaume zaidi kuliko wanawake)
  • Kuwa na uzito uliozidi kiasi (kwa kawaida uzito unaotakiwa ni kilo 70)
  • Kuwa na msongo wa mawazo (stress)
  • Kuwepo na matatizo mengine ya kiafya mwilini, kama magonjwa ya figo, matatizo ya mishipa ya damu, magonjwa ya moyo, kisukari au saratani
  • Matumizi ya chumvi kwa wingi au vyakula vyenye chumvi nyingi
  • Matumzi ya baadhi ya dawa
  • Utumiaji wa pombe na uvutaji sigara
  • Ujauzito
Nifanye nini kujiepusha na shinikizo kubwa la damu?

  • Epuka vyakula vyenye mafuta mengi na chumvi nyingi
  • Epuka mafuta yenye asili ya wanyama
  • Epuka kuwa na uzito uliozidi
  • Punguza kula nyama hasa nyama nyekundu
  • Epuka matumizi ya pombe, sigara na tumbaku
  • Kudhibiti msongo wa mawazo
  • Fanya mazoezi angalau dakika 30 kila siku
Madhara ya shinikizo kubwa la damu:

  • Magonjwa ya moyo(moyo kuwa mkubwa, moyo kushindwa kufanya kazi)
  • Magonjwa ya figo
  • Uharibifu wa macho na kushindwa kuona
  • Kisukari
  • Kiharusi (Stroke)
  • Kifo
Matibabu:

  • Fuata ushauri wa daktari ikiwa ni pamoja na kutumia dawa kama ulivyoelekezwa. Mara nyingi wagonjwa wa shinikizo kubwa la damu huacha kutumia dawa wanapohisi nafuu. Hii si sahihi kwani huongeza uwezekano wa kupata madhara.
  • Epuka vyakula vyenye chumvi nyingi.
  • Epuka mafuta mengi
  • Punguza kiasi cha nyama nyekundu
  • Punguza au epuka matumizi ya pombe
  • Kula matunda na mbogamboga kiasi cha kutosha katika kila mlo
**************************************************************************************

2. UGONJWA WA KISUKARI

Ugonjwa wa kisukari ni nini?

Ni hali ambayo hutokea wakati sukari katika damu inapokuwa nyingi kupita kiwango cha kawaida kwa muda murefu.

Sukari hutumiwa na mwili ili kupata nishati-lishe. Ili mwili uweze kutumia sukari inayotokana na chakula huhitaji kichocheo (hormone) cha insulin. Kichocheo hiki hutengenezwa na kongosho (pancreas).

Kichocheo cha insulin ndicho kinachodhibiti kiwango cha sukari katika damu. Wakati kongosho linaposhindwa kutengeneza kichocheo cha insulin au insulini iliyopo katika damu inaposhindwa kufanya kazi kwa ufanisi husababisha ugonjwa wa kisukari.

Aina za Kisukari

Kuna aina mbili za kisukari:-

  • Kisukari kinachotegemea insulini (Type 1 diabetes): Hiki huwapata zaidi watoto. Katika aina hii ya kisukari, seli za kongosho zinazotengeneza insulin huwa zimeharibika na hivyo kusababisha upungufu au ukosefu wa insulini
  • Kisukari kisichotegemea insulin (Type 2 diabetes): Huwapata zaidi watu wenye umri kuanzia miaka 45 na kuendelea. Katika aina hii ya kisukari, insulini ya kutosha inaweza ikatengenezwa katika kongosho lakini haifanyi kazi na hivyo mwili kushindwa kutumia sukari kwa ufanisi.
Viashiria vya kupata ugonjwa wa kisukari

Mtu yeyote anaweza kupata kisukari, hata hivyo kuna mambo mengi yanayoweza kuongeza hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari. Haya tunaweza kuyaweka katika makundi kutegemeana na aina ya kisukari:

  • Kisukari kinachotegemea insulini (type 1 diabetes) sababu kubwa ni kurithi ugonjwa huo katika familia au magonjwa ya kongosho (kama saratani-pancratic carcinoma au uambukizo-pancreatitis) ambayo huweza kuua seli zinazotengeneza kichocheo cha insulini. Kiashiria kikubwa hapa ni kuangalia historia ya familia kwa pande zote-baba na mama. Kama kuna historia hiyo basi unahitaji kuwa makini. Mambo mengine yanayoongeza hatari ya kupata aina hii ya kisukari kwa mtoto ni:
  • Mtoto kupewa maziwa mbadala (ya kopo au ya wanyama) au kumyonyesha mtoto kwa muda mfupi (mtoto anatakiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama mara baada ya kuzaliwa hadi miaka miwili au zaidi)
  • Mtoto akizaliwa na uzito mkubwa kupita kiasi (kawaida uzito wa kuzaliwa ni kilo 2.5 hadi 3.2)
  • Unene au uzito mkubwa utotoni
  • Mtoto akizaliwa na mama aliye na umri zaidi ya miaka 35
Kisukari kisichotegemea insulin (type 2 diabetes) huhusishwa kwa kiasi kikubwa na mtindo wa maisha usiofaa. Baadhi ya viashiria vya aina hii ni

  • Uzito uliozidi na unene uliokithiri
  • Shinikizo kubwa la damu
  • Mtindo wa maisha usiofaa husasan kutofanya mazoezi, ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na uvutaji sigara na tumbaku
  • Umri zaidi ya miaka 45
  • Kuwepo kwa historia ya kisukari katika familia
Dalili za ugonjwa wa kisukari

  • Kukojoa mara kwa mara
  • Kusikia kiu sana
  • Kusikia njaa sana
  • Kujisikia mchovu wa mwili na kukosa nguvu bila ya kufanya kazi
  • Kupungua kwa uzito na mwili kuwa mdhaifu
  • Kutoona vizuri
  • Kusikia kizunguzungu
  • Kuwa na vidonda visivyopona haraka
  • Kufa ganzi kwa vidole vya miguu na mikono
Ukiona dalili hizi nenda kituo cha huduma ya afya upate ushauri na kupimwa ili kudhibitisha.

Madhara ya ugonjwa wa kisukari

  1. Madhara ya muda mfupi: Kushuka kwa kiwango cha sukari katika damu (damu sukatiti au hypoglaycaemia) : Hali hii hutokea wakati kiwango cha sukari kinaposhuka kuliko kawaida kwa sababu ya kutumia dawa kuzidi kipimo, kufanya mazoezi bila kula au kutokula kwa muda mrefu na kunywa pombe bila kula chakula. Dalili za kushuka kwa kiwango cha sukari katika damu hujitokeza kama ifuatavyo:
Dalil za awali

  • Kusikia njaa sana
  • Kuwa na hasira
  • Mwili kukosa nguvu
  • Kupungua uwezo wa kufikiri na
  • Kuchoka sana
Dalili za kati

  • Kutokwa jasho kwa wingi
  • Mwili kutetemeka
  • Moyo kwenda mbio
  • Kichefuchefu
  • Kuumwa kichwa
  • Kusikia kizunguzungu
  • Kuona vitu viwili viwili (double vision) na
  • Kuchanganyikiwa
Dalili za baadae

  • Kukata kaul
  • Hali hii ikizidi unaweza kupoteza fahamu na hatimaye kifo kama hutapata matibabu mapema. Kama ukipatwa ha hali hii kula au kunywa kitu chenye sukari kama sukari, glukosi, soda au juisi
Tahadhari: Mgonjwa aliyepoteza fahamu asipewe kinywaji au chakula. Anaweza kuwekewa glukosi kidogo kati ya shavu na fizi. Awahishwe hospitali haraka iwezekanavyo.

  1. Kupanda kwa kiwango cha sukari katika damu (damu suziada au hyperglycaemia): Hali hii hutokea wakati kiwango cha sukari kinapokuwa juu kuliko kawaida baada ya kuacha kutumia dawa au unapoacha kufuata masharti ya ulaji, unapopata maambukizo au magonjwa kama malaria, mafua, nimonia.
Dalili za kupanda kwa kiwango cha sukari katika damu ni

  • Kupumua harakaharaka
  • Kukojoa mara kwa mara hasa wakati wa usiku
  • Kuwa na kiu au kukauka koo
  • Kunywa maji mengi
  • Kutoona vizuri
  • Kuchoka bila sababu
  • Kizunguzungu
  • Mapigo ya moyo kwenda mbio
  • Kuchanganyikiwa
  • Kupungukiwa na maji mwilini
  • Kupoteza fahamu. Mgonjwa asipewe kitu chochote
Madhara ya muda mrefu:

  • Kupata mtoto wa jicho na upofu
  • Magonjwa ya figo
  • Kupata magonjwa ya kinywa na kung’oka kwa meno
  • Shinikizo kubwa la damu
  • Magonjwa ya moyo
  • Kufa ganzi na kupoteza hisia hasa mikononi na miguuni
  • Miguu na mikono kuchomachoma
  • Vidonda kutopona upesi na hatari ya kukatwa miguu
  • Kiharusi na kupoteza kumbukumbu
  • Kupungua nguvu za kiume au kukosa nguvu kabisa
  • Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake na
  • Kupata fangasi ukeni.
Kumbuka: Madhara ya muda mrefu huweza kuzuilika. Fata masharti unayopewa na daktari.

Chakula kwa wagonjwa wa kisukari

  • Kula mlo kamili
  • Kula vyakula vya nafaka kama ulezi, mtama, uwele na mtama, uwele na dona, ngano na shayiri
************************************************************************************


3. UGONJWA WA MOYO

Ugonjwa wa Moyo ni nini?

Ugonjwa wa moyo au magonjwa ya moyo yanahusisha yale magonjwa yoyote yanayoathiri moyo na mishia yake. Magonjwa ya moyo yanajumuisha coronary heart disease, myocardia infaction (heart attack), congestive heart failure, atherosclerosis, angina, cerebrovascular diseases, stroke (kiharusi), aneurysm na peripheral vascular disease.

Sababu:

Tafiti zimeonyesha kuwa ugonjwa wa moyo huanza pale ambapo mambo Fulani yanaposababisha sehemu ya ndani ya kuta za mishipa ya damu kuharibiwa. Mambo hayo ni pamoja na:

  • Uvutaji wa sigara
  • Kuwepo na kiwango kikubwa cha aina Fulani za mafuta na lehemu katika damu
  • Shinikizo kubwa la damu; na
  • Kisukari
Kuta za mishipa ya damu zikiharibiwa, mafuta hujikusanya katika sehemu ya mishipa iliyoharibiwa na kutengeneza utando wa mafuta (plaque). Kadiri muda unavyoendelea ndivyo mafuta haya yanavyozidi kujijenga katika sehemu hiyo hadi kufanya mishipa hiyo kuwa myembamba na hivyo kupunguza kiasi cha damu kinachobeba hewa ya oksijeni na virutubishi kwenda kwenye misuli ya moyo. Hatimaye sehemu hiyo ya mshipa inaweza kupasuka. Kama sehemu hiyo ikipasuka, sehemu ya seli za damu zinazoitwa platelets ambazo husaidia mwili kuponya kidonda hujigandisha kwenye mpasuko na hivyo kuanza kujikusanya. Hali hii huongeza mkusanyiko, hivyo kuendelea kufanya mishipa hiyo kuwa myembamba zaidi na hali hiyo husababisha moyo kushindwa kufanya kazi na mtu hupata ugonjwa wa moyo (heart attack). Mkusanyiko wa mafuta na platelets wakati mwingine huweza kumeguka kama mabonge na kusafiri kwenda kuziba mishipa midogo ya damu ya kichwani. Hali hii ikitokea mtu hupata kiharusi. Hali ya kujijenga kwa mafuta na platelets hutokea polepole, huchukua muda mrefu na huweza kujitokeza kwa dalili kama kupanda kwa shinikizo la damu.

Dalili za ugonjwa wa moyo:

Mara nyingi hakuna dalili inayojitokeza mpaka pale moyo unaposhindwa kufanya kazi ghafla (heart attack), au mtu anapopata kiharusi. Zaidi ya hayo, dalili za ugonjwa wa moyo hutofautiana kutegemeana na aina ya ugonjwa wa moyo. Hata hivyo, hazijitokezi mapema na kama zikijitokeza dalili za ugonjwa huu ni pamoja na:

  • Maumivu ya kifua (hii ni dalili kuu ya ugonjwa wa moyo);
  • Kujisikia udhaifu na kuchoka sana;
  • Moyo kwenda mbio na kukosa pumzi au kushindwa kupumua;
  • Kuvimba miguu, tumbo na mishipa ya shingo hujitokeza
  • Kukohoa
  • Maumivu ya mgongo, mabega, shingo na taya;
  • Tumbo kujaa, kichefuchefu, na kutapika
  • Kukosa usingizi na
  • Kupoteza fahamu
Hadi mtu kuanza kupata dalili hizi amekuwa ameishi na ugonjwa huo kwa muda mrefu. Hivyo, njia bora ya kugundua mapema dalili ya ugonjwa /magonjwa ya moyo ni kuchunguzwa afya yako mara kwa mara.

Mambo yanayoongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo:

  • Kutozingatia ulaji bora . Ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, sukari nyingi, chumvi nyingi, kutokula mbogamboga na matunda ya kutosha;
  • Uvutaji wa sigara na tumbaku kwa kutafuna au kunusa (ugoro)
  • Unywaji wa pombe na utumiaji wa madawa ya kulevya
  • Kuwa na uzito uliozidi au unene
  • Kutofanya mazoezi ya mwili na viungo mara kwa mara
  • Kuwa na shinikizo kubwa la damu
  • Kuwa na ugonjwa wa kisukari
  • Kuwa na umri zaidi ya miaka 50
  • Kuwa na historia ya ugonjwa wa moyo katika familia; na
  • Jinsia (wanaume huweza kupata tatizo hili mapema zaidi)
Mambo ya kufanya ili kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo

  • Epuka kula vyakula vyenye mafuta mengi kama jibini, siagi, nyama iliyonona, maini na figo, ngozi ya kuku, samli
  • Punguza ulaji wa nyama, hususan nyama nyekundu (isizidi nusu kilo kwa wiki)
  • Ongeza matumizi ya nafaka hasa zile kama unga wa dona, jamii ya kunde, mbogamboga na matunda.
  • Fanya mazoezi ya mwili angalau dakika 30 kila siku
  • Dhibiti uzito wa mwili
  • Epuka msongo wa mawazo
  • Epuka uvutaji wa sigara au utumiaji wa tumbaku
  • Kuwa na tabia ya kupima afya yako mara kwa mara ili kujua hali yako ya afya.
Ushauri kwa wenye ugonjwa wa moyo: Fuata kwa makini taratibu za matibabu kama ulivyoshauriwa na daktari ikiwa ni pamoja na:

  • Kula mbogamboga na matunda kwa wingi kila siku
  • Kula zaidi vyakula vya jamii ya kunde na nafaka zisizokobolewa kama dona na ngano, vilevile ulezi na mtama
  • Punguza matumizi ya mafuta na epuka mafuta yatokanayo na wanyama, pamoja na nyama yenye mafuta
  • Punguza ulaji wanyama hususan nyama nyekundu (isizidi nusu kilo kwa wiki)
  • Punguza vyakula vyenye lehemu kwa wingi kwa mfano mayai, maini, moyo, figo, mafuta yenye asili ya wanyama (kama samli na siagi) na nyama nyekundu
  • Epuka vyakula au vinywaji vinavyosababisha ongezeko la uzito, ikiwa ni pamoja na vyakula vyenye mafuta mengi, sukari nyingi (soda, juisi bandia) na pombe
  • Punguza kiasi cha chumvi na acha kula chumvi ambayo haijapikwa
  • Fanya mazoezi ya mwili angalau dakika 30 kila siku
  • Hakikisha una uzito unaoshauriwa kutegemeana na urefu wako.
*************************************************************************************



  1. UGONJWA WA UTI/URINARY TRACT INFECTION
Ugonjwa wa UTI ni nini?

UTI kitaalamu ni “Urinary Tract Infection” ni magonjwa au maambukizi yanayoathiri mfumo wa kutengeneza na kutoa mkojo nje ya mwili. Mfumo huu unahusisha kibofu cha mkoja, figo pamoja na milija inayounganisha kibofu cha mkoja na figo. Pindi wadudu yaani bacteria wanapoingia katika mfumo huu wanaweza kusababisha maambukizi ambayo mara nyingi wataalamu hupenda kuyaita UTI.

Mara nyingi maambukizi ya mfumo huu wa mkojo huwa ni maambukizi ya kibofu cha mkojo (Bladder infections). Maambukizi ya kibofu cha mkojo kawaida hayana madhara makubwa kama yakitibiwa haraka. Yasipotibiwa yanaweza kusambaa hadi kwenye figo zako. Maambukizi ya figo yana madhara makubwa sana kwani huaribu figo ambapo unaweza kupata magonjwa ya figo ambayo tunayaita Kidney au Renal Deseases.

Nini usababisha UTI?

Kawaida Bakteria uingia kwenye mfumo wako wa mkojo kupitia kwenye mlija mdogo wa mkojo ujulikanao kitaalamu kama urethra mlija unayobeba mkojo kutoka kwenye kibofu cha mkojo kwenda nje ya mwili. Bakteria wanaosababisha maambukizi uishi katika utumbo mkubwa wa chakula na upatikana kwenye choo au kinyesi. Mara nyingi bacteria hawa wanaitwa E. Coli. Bakteria hawa upitia kwenye urethra na kusafiri hadi kwenye kibofu cha mkojo hadi kwenye figo na kusababisha maambukizi.

Wanawake hupata UTI zaidi ya wanaume kwa sababu milija yao ya kutoa mkojo kwenye kibofu cha mkojo ni fupi zaidi ya wanaume na hivyo kuwezesha bacteria kusafiri kwa urahisi zaidi hadi kwenye kibofu cha mkojo. Pia kufanya tendo la ndoa au kujamiana pia kuna rahisisha bacteria kuingia kwenye urethra.

Pia unaweza kupata UTI kwa kutokunywa maji ya kutosha kwani maji husaidia kutengeneza mkojo wa kutosha na hivyo unapokojoa unasafisha milija yako ya kutoa mkojo nje ya mwili.

Pia watu wenye ugonjwa wa kisukari wana hatari ya kupata UTI mara kwa mara kwani kinga ya mwili hushuka na hivyo kusaidia kupata maambukizi kirahisi na pia mkojo anaotoa huwa na kiasi kikubwa cha sukari ambacho husaidia wadudu kukua vizuri. Pia mama mjamzito hupatwa na UTI zaidi. Uwezekano wa kupata maambukizi ni makubwa endapo unatatizo linalosababisha mkojo kushindwa kutoka nje ya mwili kama vile, mawe kwenye figo yaani kidney stones au ongezeko la tezi la kibofu cha mkojo yaan enlarged prostate kitaalamu BPH.

Wanawake upata UTI mara kwa mara na hizi zinaweza kuwa sababu zinazoongeza uwezekano wa kupata UTI mara kwa mara:

  • Usafi wakati wa kujitawaza wakati wa haja kubwa; baadhi ya wanawake hupenda kufuga kucha ndefu kwa ajili ya urebo hivyo wakiwa na haja kubwa uogopa kugusa choo hivyo ujimwagia maji ambayo yanaweza kupiga vipande vya choo hadi kwenda kwenye njia yao ya mkojo na hivyo kuweza kupata maambukizi. Pia wengine ujitawaza kwa kuelekea njia ya ukeni hivyo kuongeza nafasi za kupata maambukizi.
  • Choo chafu: Vyoo vya watu wengi vya kukalia pia ni chanzo za kusababisha maambukizi.
  • Taulo za kuogea na nguo za ndani
  • Kufanya tendo la ndoa kinyume na maubile
  • Kusafisha ukeni na sabuni hususan sabuni ambazo ni medicated kama delto kwani uondoa kinga za sehemu husika (normal flora).
Dalili za UTI

  • Kujisikia maumivi au kuwashwa wakati wa kukojoa
  • Kujihisi haja ya kukojoa lakini unapoenda kukojoa mkojo hautoki wa kutosha badala yake unatoka kidogo
  • Tumbo kulihisi kubwa au zito
  • Mkojo kutoa harufu mbaya au mkojo kuwa kama wingu
  • Kupata maumivi mgongoni hususani chini ya mbavu haya ni maambukizi ya figo
  • Kupata homa na kutetemeka
  • Kichefuchefu na kutapika
Matibabu:

Nenda hospitali ili upimwe mkojo wako ili kugundua kama una UTI au maambukizi mengine kama Malaria, kisukari, magonjwa ya figo, kinga ndogo ya mwili na pia ujauzito.

UTI inatibiwa kwa dawa za antibiotics na pia ukiwa msafi huwezi kupata UTI mara kwa mara.

************************************************************************************



5. MAGONJWA YA VIUNGO VYA NDANI VYA UZAZI/PELVIC INFLAMATORY DIEASE (PID)

Utangulizi:

Mpenzi msomaji wa Health Media Tanzania leo tunaangalia magonjwa yanayoathiri viungo vya ndani vya uzazi kwa wanawake. Kitaalamu magonjwa haya yanajulikana kama Pelvic Inflammatory Disease kwa kifupi PID. PID kawaida au mara nyingi inawasumbua au kuwashambulia wanawake kwenye nchi zinazoendelea, ikiwemo nchi yetu Tanzania. Zaidi ya asilimia 60 ya wanawake wanaohudhuria kliniki za nje za magonjwa ya akina mama (outpatient) wenye matatizo ya ugumba yaani walioshindwa kupata mimba au watoto wanasumbuliwa na PID.

PID/Pelvic Inflammatory Diseae maana yake ni nini?

PID inamaanisha maambukizi (yaani infection) yanayoathiri viungo vya ndani vya uzazi vya mwanamke. Maambukizi haya yanajumuisha maambukizi katika kuta za ndani za tumbo la uzazi yanayojulikana kitaalamu kama “endometritis”, maambukizi katika milija ya kusafirishia mayai yajulikanayo kitaalamu kama“salpingitis”, maambukizi katika sehemu inayotoa mayai ya mwanamke yaani ovaries maambukizi haya kitaalamu yanaitwa “oophoritis” na mwisho maambukizi katika eneo lote la viungo vya uzazi yaana kitaalamu pelvic peritoneum na parametrium; maambukizi haya yanaitwa “Parametritis”. Kwa mantiki hiyo, maambukizi haya yote yanajumuishwa katika tafsiri ya neno moja ijulikanayo kama “Salpingoophoritis”. Hata hivyo, maambukizi madogo (mild infection) yanaitwa Pelvic Inflammatory Disease (PID).

AINA ZA PID

Kwa kawaida yapo makundi mawili ya aina za PID yanayojulikana kama “Primary” na “Secondary”.

  • Primary PID ni pale ugonjwa unapotokea mara ya kwanza kwenye viungo vyako vya uzazi. Mara nyingi inasababishwa na bakteria waitwao Kisonono kitaalamu aina ya Nesseria gonorrhea na Clamydiaambao bakteria hawa upanda kirahisi wakati mwanamke anapokuwa kwenye hedhi (menstruation) ambapo kunakuwa na damu ya kutosha na kuwapa bakteria hawa nafasi ya kukua vizuri. Kipindi cha hedhi bakteria hawa usambaa hadi kwenye kuta za tumbo la uzazi yaani kwenye “endometrium” na baadae kufika kwenye milija yaani “fallopian tubes” Kutokana na kuwepo kwa maji yanayotolewa kwenye ngozi ya fumbatio la viungo vya ndani yaani “peritoneum” usaidia bakteria hawa kutoka katika mijija (fallopian tubes) uweza kufika kwenye ovari kusababisha maambukizi katika ovari hizo yaani mayai ya kike. (oophoritis)
Maambukizi katika milija usababisha kukusanyika kwa maji (oedema) na usaha au maji maji meupe kama usaha. Hii hali usababisha maambukizi makali ambayo uweza kutengeneza jipu baada ya kusambaa katika fumbatio la viungo (peritoneum) ambapo jipu hili uitwa “pelvic abscess”. Hapa mgonjwa upata maumivu makali sana chini ya kitovu au kinene, upata homa kali sana, maumivu wakati wa kukojoa.

Kumbuka: Kisonono au gonorrhea unakipata kwa njia ya kujamiana.

  • Secondary PID ni pale ugonjwa unapotokea kama madhara yaliyotokana na ugonjwa wa kwanza au baada ya upasuaji katika viungo vya uzazi.
Madhara haya yanaweza kutokana na:

  • Upasuaji/operation ndogo ya kutoa mimba ambapo uishia kusababisha maambukizi yajulikanayo kama “post abortion sepsis”,
  • Maambukizi yatokanayo baada ya kujifungua yaani “postpartum sepsis”
  • Mimba iliyotungwa nje ya kizazi na kuharibika yaani “infected ectopic pregnancy”
  • Madhara ya kutoa uvimbe (fibroids) katika tumbo la uzazi yaani “myomectomy”
  • Upasuaji mkubwa wa kuondoa kizazi cha kike yaani “vaginal hysterectomy”
  • Kufunga kizazi yaani “tubal ligation”
  • Upasuaji katika milija wakati wa kuizibua yaani “tubal surgery”
Maambukizi katika madhara haya mara nyingi ni bakteria wanaotokana na choo/kinyesi. Bakteria hawa wanajumuisha E. Coli, Klebsiella, Salmonella, Proteus vulgaris, peptostreptococcus na streptococcus.

Utatambuaje kuwa una PID?

  1. Dalili:
  • Kawaida utajisikia maumivu chini ya kitovu yaani kitaalamu lower abdominal pain.
  • Homa kupanda
  • Mapigo ya moyo kwenda mbio
  • Kuvimba tumbo
  • Kutokwa na maji machafu ukeni na yanatoa harufu mbaya na pengine kutokwa na damu ukeni yaani “vaginal bleending”.
Ushauri: Ukiona dalili hizi nenda kituo cha afya ukamuone daktari ili aweze kukupatia tiba sahihi kwani PID inasababisha ugumba usipotibiwa vizuri na kupona kabisha.

  1. Matibabu:
Kawaida matibabu yanategemea na ukubwa wa tatizo. Ukubwa wa tatizo umegawanywa katika makundi makuu matatu:

  • Acute PID
  • Mild Acute PID
  • Chronic PID
Kundi la kwanza na la pili yanatibiwa kwa kupewa dawa/tiba na mtaalamu wa afya hususan daktari. Kundi la tatu yaani Chronic PID mara nyingi tiba yake ni dawa za kupunguza maumivu na pia kupata ushauri wa daktari. Hakuna dawa unayoweza kupewa ili tatizo hili liondoke au liishe badala yake unatuliziwa maumivu tu. Kama unapata maumivu wakati wa tendo la ndoa basi upasuaji (surgical intervention) unaweza kutumika kama njia ya tiba.

Madhara ya PID

PID isipotibiwa vizuri na kupona inaweza kuathiri afya ya mwanamke kimwili, kijamii na kisaikolojia. Mgonjwa anaweza kuishia na kupata ugonjwa sugu yaani “chronic PID” ambayo uweza kumsababishia maumivu makali wakati wa kujamiana na pia kupata matatizo ya mzunguko wa hedhi. Na pia inaweza kusababisha jibu na pia maambukizi katika fumbatio la viungo vya ndani yaani “severe peritonitis” ambayo ni hatari kwa maisha. Pia inaweza kuishia kutengeneza uvimbe katika milija na ovari yaani “Tubal Ovarian Masses TOM”. Hii inaweza kupelekea kupata ugumba wa muda yaani “sub fertility” au ugumba wa kudumu yaani “infertility”. Haya madhara umsababishia mwanamke kuathirika kijamii na kisaikolojia na pia umletea msongo wa mawazo.

Talaka, kutengana na hata kujiua (suicide ) ni matokeo ya kijamii na kisaikolojia ya PID.

Hitimisho:

PID ni sababu kubwa ya kusababisha madhara kwa wanawake. Inasababisha madhara si tu kwa wanawake na pia kwa jamii nzima. Ina madhara kimwili, kijamii na kisaikolojia.

*************************************************************************************



6. UVIMBE KATIKA TUMBO LA UZAZI/FIBROIDS

Utangulizi:

Uvimbe katika tumbo la uzazi la mwanamke ukiondoa mimba kawaida ujulikana kitaalamu kama “pelvic tumour in women”. Uvimbe huu utengenezwa na tishu za misuli ya tumbo la uzazi ambayo uitwa “Fibroids” au “Fibromyoma” au “Uterine Myoma”.

Mara nyingi uvimbe wa aina hii uanzia 5 hadi 30 kwa namba. Ufanana kama umbo la yai au kiazi ulaya na huwa na nundu nundu yaani “lobulated surface”. Uvimbe huu huwa mgumu (Hard).

Sababu:

  • Sababu kuu hasa ya uvimbe huu katika tumbo la uzazi la mwanamke kitaalamu haijulikani.
  • Ila uvimbe au fibroids zimeonekana au kuusishwa na mambo makuu matatu yaani Umri, Uzao (Parity) na Genetics au Race.
Ni mara chache wanawake chini ya miaka 20 kupata uvimbe katika tumbo la uzazi. Mara nyingi huwapata wanawake wenye umri kati ya miaka 35 hadi 45.

Wanawake ambao hawajapata uzao au kuzaa (nulliparous) au wenye ugumba.

Kawaida huwapata wanawake wa jamii ya watu weusi na pia hutokea katika familia.



Maeneo ambayo uvimbe utokea:

Mara nyingi uvimbe utokea maeneo yafuatayo:

  • Juu ya kuta za tumbo la uzazi kwa nje yaani (on surface) uvimbe huu uitwa Subserous fibroids.
  • Katikati ya misuli ya tumbo la uzazi (within muscle wall of uterus) uvimbe huu uitwa Intramural
  • Ndani ya tumbo la uzazi (within endometrial cavity) uvimbe huu uitwa Submucous.
Dalili:

  • Uvimbe mdogo na mkubwa kidogo mara nyingi hauna dalili zozote.
  • Mzunguko wa hedhi kusumbuliwa: Dalili kubwa za uvimbe (fibroids) ni kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi kuliko ulivyozoea kama ulikuwa unaenda hedhi kwa siku 3 basi inaweza kwenda hadi siku 8 na damu inakuwa nyingi kuliko kawaida kwa sababu zifuatazo:-
  • Kuongezeka kwa ukubwa wa misuli ya tumbo la uzazi na zile sehemu zinazotoka damu
  • Kuongezeka kwa misuli ya tumbo la uzazi (vascularity of Uterus)
  • Mzunguko wa hedhi kubadilika kuwa mfupi na wakati mwingine mrefu na kutokwa damu utokea mara chache.
  • Kujibambua kama una uvimbe tumboni wenye ukubwa wa mimba ya miezi mitano (14 weeks) na kuendelea
  • Kupungukiwa na damu (anaemia) na kuchoka kwa mwili na pia kupungua mwili kwa sababu ya kutokwa damu nyingi.
  • Dalili zinazohusiana na ujauzito:-
  • Ugumba (infertility)
  • Mimba kutoka (abortion) na kuzaa kabla mimba haijatimiza muda wake (premature labours)
  • Mtoto kulala mlalo mbaya (malpresentation)
Uvimbe unaweza kugunduliwa vipi?

  • Kushika uvimbe kwenye tumbo la uzazi ambao ni mgumu (hard), hauna maumivu (painless) na hauna sababu (causeless).
  • Uvimbe ni wa duwara au kama kiazi mviringo au yai
  • Unatembea (mobile) kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine
  • Unatoka kwenye pelvis
  • Kawaida hauna maumivu.
Madhara ya Uvimbe huu (fibroids)

  • Kusababisha maambukizi
  • Tumbo kujaa maji (ascites)
  • Kubadilika na kuwa saratani-Hii ni mara chache (rare)
  • Kuzaliana au kukua tena (degeneration) ni jambo la kawaida.
Matibabu:

  1. Hakuna tiba kwa uvimbe mdogo ambao haujaonesha dalili nilizotaja hapo awali (mgonjwa anashauriwa kuwa kwenye uangalizi wa daktari)
  2. Upasuaji kama njia ya tiba- Sababu za kuhitaji kufanya upasuaji:
  • Uvimbe kama ni mkubwa zaidi ya wiki 12 za ujauzito yaani mimba ya miezi 3 hapa unaweza kufanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe huo.
  • Kama uvimbe unakuwa haraka kwa muda mfupi
  • Kama uvimbe uko nje ya tumbo la uzazi (subserous fibroids)
  • Kama uvimbe unasababisha ugumba na kutokwa mimba mara kwa mara.
Upasuaji upo wa aina mbili:

  • Kwa wanawake chini ya miaka 35 wenye kuhitaji mtoto uvimbe unatolewa na kubakiza tumbo la uzazi. Ufanyiwa upasuaji ujulikanao kama “Myomectomy”.
  • Kwa wanawake zaidi ya miaka 40 na ambao hawahitaji tena mtoto; uvimbe pamoja na tumbo la uzazi yaani “uterus” utolewa vyote pamoja na upasuaji huu ujulikana kama “Hysterectomy”.
Ushauri: Hili tatizo uwapata sana wanawake wenye umri kati 35 na 45, wanawake ambao hawana watoto. Hivyo ninawashauri wanawake wajitahidi kupata ujauzito kabla ya kufikia miaka 35 ili kuondokana na hatari ya kupata uvimbe huu.

*************************************************************************************



7. TATIZO LA UGUMBA (UTASA) /INFERTILITY

Maana ya Ugumba/Utasa

Ugumba ni kushindwa kupata mimba /ujauzito baada ya mwanamke kukutana kimwili/kujamiana/kufanya tendo la ndoa na mwanaume kwa kipindi cha miezi 12 (mwaka mmoja) bila kutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango.

Pia ugumba ni kushindwa kwa mwanaume kutungisha au kumpa mimba mwanamke baada ya kukutana nae kimwili/kujamiana nae au kufanya nae tendo la ndoa kwa kipindi cha miezi 12 (mwaka mmoja) bila kutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango.

Hivyo ugumba unatokea pande zote mbili yaani mwanaume na mwanamke. Watu wengi ufikiri kuwa ugumba ni kwa mwanamke peke yake. La hasha! Ugumba pia uwapata wanaume kwa kushindwa kutungisha mimba kama tutakavyoona kwenye sababu za ugumba.

Aina za Ugumba/Utasa

Ugumba umegawanyika kitaalamu katika makundi makuu mawili:

a) Ugumba wa asili/wa kwanza (Primary Infertility): Hapa hakuna mimba au ujauzito uliowahi kutokea kwa kipindi cha miezi 12 ya kujamiana au kufanya tendo la ndoa bila kutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango.

b) Ugumba wa pili (Secondary Infertility): Kushindwa kupata mimba au ujauzito baada ya mimba ya kwanza au zaidi. Hii ina maana kwamba mwanamke amewahi kupata mimba au kuzaa mtoto mmoja au wawili lakini sasa anashindwa kupata mimba nyingine. Pia mwanaume wamewahi kutungisha mimba au kumpatia ujauzito mwanamke lakini sasa hawezi tena kumpatia ujauzito.

Jinsi tatizo linavyoathiri/Incidence

Karibu asilimia 15 ya wanandoa ni wagumba au tasa. Kiwango kikubwa cha magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiana katika jamii usababisha zaidi tatizo la ugumba au utasa. Magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiana ni kama:

  • Kaswende, Kisonono, Pangusa na Klamidia husababishwa na bakteria
  • Virusi vya Ukimwi (VVU), Malengelenge, Hepatitis B na Virusi papilloma vya binadamu (VPB) husababishwa na Virusi (Virus).
  • Trichomoniasis husababishwa na protozoa (parasites)
  • Kandidiasisi
Utambuzi wa ugumba / Utagunduaje kuwa una ugumba?

Kama nilivyoeleza hapo awali katika maana ya ugumba dalili kuu ya ugumba ni kutopata mimba au ujauzito katika kipindi cha mwaka mmoja kama hutumii njia yoyote ya uzazi wa mpango. Hivyo ukiwa na hali hiyo ni vema kwenda hospitali kwa uchunguzi zaidi wa kuweza kubaini tatizo ni nini?

Kwa kawaida sababu za ugumba kwa wanaume uchangia asilimia 30, mwanamke asilimia 40 na asilimia 30 hutokea kwa pande zote mbili yaani mwanaume na mwanamke. Hivyo ukiwa na tatizo hili katika ndoa yako ni vema mwende kumuona daktari wa magonjwa ya akina mama ili aweze kuwafanyia uchuguzi zaidi na pia kuwapatia ushauri jinsi ya kupata mtoto.

Sababu za Ugumba kwa Mwanaume

Mwanaume anaweza kushindwa kutungisha mimba au kumpatia ujauzito mwanamke kwa sababu zifuatazo:-

  • Magonjwa ya zinaa (STDs) kama nilivyokwisha yataja hapo awali, maambukizi katika milija ya kusafirisha mbegu za kiume (epididymitis), mumps orchitis, pombe za kupindukia, ugonjwa wa kisukari na pia kama unashinikizo kubwa la damu na unatumia dawa zinazosababisha ugumba.
  • Kama amewahi kufanyiwa upasuaji wa hernia (herniorrhaphy), maumivu ya tests (injury to tests), upasuaji wa mabusha.
  • Mionzi ya kemikali katika sehemu za uume kama Xray
  • Maumbile ya uume kama hayako sahihi.
  • Historia ya kujamiana kama unaweza kutoa mbegu za kiume (ejaculation inatokea?) Mara nyingine mwanaume anaweza kuwa anahisi kuwa shahawa zinatoka lakini kumbe zinarudi nyuma na hivyo hazifiki kwenye “cervix”. Hali hii kitaalamu inaitwa “Retrograde ejaculation”.
  • Hali ya viungo vyake vya uzazi yaani ukubwa wa pumbu zake (testicular size) kawaida ukubwa wa pumbu ni sentimita 4.5*2.5, uwepo wa milija ya kusafirishia shahawa, tezi la kibofu cha mkojo, ujazo wa shahawa (kawaida inatakiwa iwe mililita 2), idadi ya mbegu za kiume inatakiwa isipungue milioni (20,000,000) kwa mililita moja, uwezo wa mbegu kutembea baada ya masaa 4 tangu ejakulasheni itokee inatakiwa iwe zaidi ya asilimia 40 ili iweze kufika pale yai la kike lilipo likisubiri kutungishwa. Mwisho umbo la mbegu linatakiwa liwe kawaida angalau zaidi ya asilimia 60.
Haya yote yanaweza kutambuliwa na wataalamu wa afya tu baada ya kukufanyia uchunguzi wa kitaalamu hivyo ninakushauri kama unatatizo hili uende kumuona daktari ili akusaidie kugundua tatizo liko wapi.

Sababu za Ugumba kwa Mwanamke

Kama nilivyoeleza awali mwanamke anachangia asilimia 40 katika tatizo la ugumba katika ndoa.

Sababu za ugumba katika mwanamke zinaweza kuwa kama ifuatavyo:

  • Historia kama amewahi kuwa kwenye uzazi wa mpango kwa muda mrefu (length of contraceptive)
  • Historia ya idadi ya mimba na utoaji mimba (abortions)
  • Magonjwa ya zinaa kama nilivyokwisha yataja hapo awali
  • Uvimbe katika tumbo la uzazi, milija na mayai (myoma, tubal or ovarian masses)
  • Kukosa tumbo la uzazi au uke (absence of uterus or vagina)
  • Kuwa bikira (imperforated hymen)
  • Kutokwa na uchafu au maji kwenye uzazi (discharge)
Sababu za ugumba kwa pande zote mbili

  • Kushindwa kugundua lini muda yai la kike linapokuwa limekomaa (Ovulation)
  • Kutambua kama “ovulation” imetokea.
  • Je, milija ya uzazi iko vizuri kuruhusu mbegu za kiume na yai la kike kukutana ili kutungishwa.
  • Je, wanandoa wako vizuri kimwili na kisaikolojia kwa ajili ya kujiandaa kupata mimba.
Ni vizuri kumuona daktari ili aweze kuwasaidia kutambua lini yai la kike linakuwa limekomaa tayari kwa kutungishwa ili tarehe zinapokaribia basi mnakutana kimwili.

Vipimo.

Vipimo vipo kwa ajili ya Mwanamke na Mwanaume.

Vipimo kwa pande zote mbili

  • Vipimo vya damu kuangalia magonjwa ya zinaa, mkojo, vipimo vya shinikizo kubwa la damu, kisukari na joto la mwili.
Vipimo kwa Mwanaume

  • Mkojo (Urinalysis)
  • VDRL (kuangalia magonjwa ya zinaa)
  • Kupima shahawa (Complete Seminal fluid analysis)
Vipimo kwa Mwanamke

  • Wingi wa damu (Hb)
  • Mkojo (Ulinalysis)
  • VDRL
  • HSG (Hysterosaloingography) kuangalia milija inayosafirisha mayai kama iko sahihi au imeziba kutokana na magonjwa ya PID kama tulivyozungumza katika kipindi kilichopita.
  • Laparascopy and Dye: Pia inasaidia kuangalia milija inayosafirisha mayai kama iko sahihi.
  • BBT (Basal Body Temperature Chart)
  • Endometrial biopsy
Matibabu

Vipimo vinavyofanyika ni kwa ajili ya uchunguzi wa tatizo na pia ni tiba. Kwani tatizo likishagundulika ni nini na likatibiwa basi ujauzito hupatikana. Asilimia kati 15 hadi 20 ya wanandoa wenye tatizo la ugumba wanaofanyiwa uchunguzi wa kitaalamu upata uzazi (mimba).

Hivyo ninawashauri wale wote wenye tatizo la ugumba kwenda kuwaona madaktari bingwa wa magonjwa ya akina mama ili waweze kuwasaidia kupata watoto.

**************************************************************************************

8. UGONJWA WA MALARIA

Malaria ni nini?

Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na kimelea (mdudu) kinachonyonya damu ya binadamu. Kimelea hiki kinajulikana kama “parasite”. Lakini watu wengi uelewa kwamba malaria husababishwa na mbu. Kuna aina nne ya vimelea (parasites) vinavyosababisha malaria navyo ni:

  • Plasmodium Vivax
  • Plasmodium Falciparum
  • Plasmodium Malariae
  • Plasmodium Ovale
Kimelea ambacho ni hatari na kina madhara makubwa kwa binadamu ni Plasmodium Falciparum. Plasmodium Vivax hakina madhara makubwa ingawa kimesambaa sana kuliko kile cha Falciparum. Plasmodium Falciparum husababisha vifo kwa haraka.

Kimelea cha malaria hubebwa au uishi katika utumbo wa mbu jike aina ya Anopheles.

Jinsi gani mtu anapata maambukizi ya vimelea vya malaria?

  • Vimelea (parasites) vinaingia kwenye mwili wa binadamu baada ya mbu jike aliyeathirika na vimelea hivi vya malaria wakati akinyonya damu ya binadamu kama mlo au chakula chake.
  • Mbu huyu umg’ata binadamu kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa kumi na mbili asubuhi. Mbu ukaa ndani au nje ya nyumba.
  • Vimelea uzaliana ndani ya utumbo wa mbu na baadae usafiri hadi kwenye tezi za mate yake. Wakati mbu unamng’ata binadamu utoa mate kama ganzi ili binadamu asigundue kama anang’atwa na hapo ndipo vimelea vya malaria umuingia binadamu.
  • Baada ya kuingia kwenye mwili wa binadamu vimelea hivi usafiri hadi kwenye ini ambapo huzaliana kwa wingi na hatimaye kuingia kwenye mzunguko wa damu na kusababisha uharibifu wa seli nyekundu za damu. Hapa ndipo mtu huanza kujihisi homa, kutetemeka na dalili nyinginezo.


Makundi gani ya watu huathirika sana na ugonjwa wa malaria?

  • Watoto chini ya miaka 5
  • Wanawake wajawazito
  • Watu wanaoishi na virusi vya ukimwi
  • Watu wanaosafiri kutoka maeneo yasiyokuwa na mbu wanaobeba vimelea vinavyosababisha malaria.
Kwa nini malaria ni muhimu?

  • Karibu watu milioni 300-500 uugua malaria
  • Watu milioni 1 kila mwaka ufariki dunia kutokana na ugonjwa wa malaria
  • Karibu watu 310,000 barani Africa ufariki dunia kutokana na ugonjwa wa malaria
  • Katika watoto watano wanaofariki dunia kila mwaka barani Africa malaria ni mojawapo ya sababu ya vifo vya watoto hao.
Mzigo utokanao na ugonjwa wa Malaria

  • Malaria huzuia maendeleo ya biashara za kimataifa.
  • Maeneo yanayoathiriwa sana na ugonjwa wa malaria wanaishi watu masikini wenye kipato cha dola 1.25 kwa siku.
  • Malaria ni chanzo kikuu cha utoro kazini na shuleni barani Africa.
  • Malaria inapunguza uzalishaji, nguvu kazi na hata vifo.
  • Malaria barani Africa husababisha kupotea kiasi cha fedha bilioni 12 dola za Kimarekani.
Malengo ya Millenia

Lengo 1: Kutokomeza umaskini uliokithiri na njaa

Lengo 2: Kufikia elimu ya msingi kwa wote

Lengo 3: Kukuza usawa, jinsia na kuwawezesha wanawake

Lengo 4: Kupunza vifo vya watoto wadogo kwa asilimia 20% barani Africa

Lengo 5: Kupunguza vifo vya mama wajawazito hususani vinavyotokana na malaria

Lengo 6: Kupambana na Virusi vya Ukimwi na Ukimwi, Malaria na magonjwa mengine.

Lengo 7: Kuhakikisha mazingira endelevu

Lengo 8: Kuendeleza ushirikiano wa maendeleo kimataifa

Malengo ya Milllenia yanayolenga Malaria ni

Lengo 1: Kutokomeza umaskini uliokithiri na njaa

Lengo 4: Kupunza vifo vya watoto wadogo kwa asilimia 20% barani Africa

Lengo 5: Kupunguza vifo vya mama wajawazito hususani vinavyotokana na malaria

Lengo 6: Kupambana na Virusi vya Ukimwi na Ukimwi, Malaria na magonjwa mengine.

Mpango wa kuzuia au kupambana na Malaria

Historia inaonesha kuwa kwenye miaka ya 50 (1950s) kulikuwa na mpango au mkakati wa kutokomeza malaria ulimwengu mzima. Kwa matokeo hayo ya mpango huo, malaria ilitokomezwa takribani nchi nyingi duniani.

Mwaka 1969 Mpango huu au mkakati huu ulisitishwa kwa sababu zifuatazo:-

  • Vimelea (parasites) hawa walikuwa sugu kwa dawa waliyokuwa wanaitumia kuwatokomeza (Insecticide resistance).
  • Dawa za kutibu ugonjwa huu zilikuwa sugu na kushindwa kuua vimelea hivi (Drug resistance).
  • Miundo mbinu mibovu mfano barabara hususan barani Africa (Poor infrastructure particularly in Africa).
Hivyo Mpango au mkakati wa kutokomeza kabisa malaria ulibadilishwa na kuwa Mpango wa Kuzuia Malaria.

Kipindi cha Miaka ya 70 (1970s) na 80 (1980s) malaria haikupewa kipaumbele au umuhimu.

Mpango wa Kuzuia Malaria

Hali halisi ya sasa:

  • Malaria imeibuka (re-emerge) kama tatizo la kiafya kimataifa kuanzia miaka 90 (1990s)
  • Mwaka 1992 Mpango au mkakati wa kuzuia Malaria ulikubaliwa na Umoja wa Mataifa
  • Mipango mingine ni pamoja na Roll Back Malaria 1998, Abuja Declaration 2000 na Strong political commitment and partnership.
Roll Back Malaria

Mpango huu ulizinduliwa rasmi mwaka 1998 lengo likiwa ni kupambana na Malaria barani Africa.

Mashirika yaliyokubaliana kushirikiana katika mpango huu ni WHO, UNDP, UNICEF, na WB (Benki ya Dunia).

Lengo kuu ni kupunguza mzigo au tatizo la Malaria ifikapo mwaka 2010.

Mikakati iliyowekwa kufikia lengo hili ilikuwa:-

  • Kutumia vyandarua vilivyowekewa dawa ya kuua mbu kwa watoto chini ya miaka 5 na mama wajawazito
  • Kuwapatia matibabu ya malaria bure watoto chini ya miaka 5
  • Kuzuia na kutibu malaria kwenye ujauzito
  • Kugundua mapema na kupambana na malaria katika maeneo yaliyo na vimelea vya malaria.
Tatizo la Malaria Duniani (Ulimwenguni)

Mwaka 2012 wagonjwa wa malaria walikadiriwa kufikia milioni 219.

  • 86% za wagonjwa walikuwa barani Africa na 10% kutoka Kusini Mashariki ya Asia
  • 98% ya ugonjwa wa malaria barani Afrika na 56% ya ugonjwa Kusini Mashariki ya Asia ilisababishwa na Plasmodium falciparum
  • Watu bilioni 3.3 wapo katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa malaria
  • Congo, India na Nigeria inachukua 40% ya ugonjwa
Mwaka 2012 vifo vilivyotokana na ugonjwa wa malaria vilikadiriwa kufikia laki sita na elfu sitini (660,000).

Jamhuri ya Kidemocrasia ya Kongo na Nigeria ilichangia 40% ya vifo vyote.

85% ya vifo barani Afrika walikuwa watoto chini ya miaka 5.

5% ya vifo hivyo ilikuwa watoto chini ya miaka 5 kutoka Kusini Mashariki ya Asia.

Nchi zilizo na maambukizi au tatizo la malaria ni 104.

Maambukizi ya malaria yanaendelea kwenye nchi 99.

Mpango wa kuzuia Malaria upo katika nchi 79

Mpango wa awali wa kuondoa malaria (Pre-elimination phase) upo katika nchi 10

Mpango wa kuondoa malaria (Elimination Phase) upo katika nchi 10

Prevention and Reintroduction phase nchi 5

Malengo

Nchi 50 (9 barani Afrika) kupunguza maambukizi mapya ya malaria kwa 75% ifikapo 2015

Nchi 4 kupunguza kwa asilimia kati ya 50 na 75.

Haja mahususi kwenye nchi 41 zenye maambukizi kwa asilimia 85.

Uchunguzi wa vimelea, ugonjwa na matibabu yake.

Kwa kawaida mtu akishaambukizwa vimelea vya ugonjwa wa malaria; vinachukua muda wa nusu saa (dakika 30) kusafiri hadi kufika kwenye ini lako. Vikifika kwenye ini vinaanza kuzaliana kwa wingi na hatimaye vinaingia kwenye mzunguko wa damu yako na hapo ndipo vinaanza kutafuna seli nyekundu ya damu yako. Vikiwa kwenye damu ndipo mtu anajisikia dalili za kupanda na kushuka kwa homa, kutetemeka mwili.

Dalili za Malaria

Dalili za malaria zinategemea mtu na mtu kutokana na nguvu za kinga yake. Hata hivyo dalili zinazowapata wagonjwa wa malaria ni zifuatazo:-

  • Kuchoka kwa mwili wote au viungo kuuma kitaalamu tunasema “General Body Weakness”
  • Homa (fever)
  • Kichwa kuuma (Headache)
  • Tumbo kuuma (Abdominal pain)
  • Kutapika (Vomiting)
  • Kuharisha (Diarrhoea)
  • Kukooa (Cough)\
Kumbuka: Hizi dalili pia utokea katika magonjwa yanayoambukizwa na bakteria mfano Homa inaweza kuwa dalili ya UTI, Pneumonia, Typhoid.

Kukooa kunaweza kuwa sababu ya maambukizi katika mapafu mfano pneumonia, kifua kikuu n.k

Kutapika na kuharisha inaweza kuwa dalili za magonjwa ya maambukizi ya tumbo pia. Hivyo ni vema ukipata dalili hizi usichukue dawa bila kupata uchunguzi wa kitaalamu na pia ushauri kutoka kwa madaktari. Unapopata dalili hizi wahi hospitali ili wataalamu wakuchunguze na kujua ni ugonjwa gani ulionao.

Matibabu ya malaria:

Matibabu yanatolewa kulingana na aina ya malaria uliyonayo. Kuna aina mbili za malaria

  • Malaria ya kawaida isiyokuwa kali au sugu kitaalamu inaitwa “Uncomplicated Malaria”. Hii haijasababisha madhara makuwa katika mwili.
  • Malaria sugu kitaalamu “Complicated Malaria”. Hii imeishasababisha madhara kama kuharibu viungo muhimu mwilini kama, ubongo (cerebral coma), figo (renal failure), ini (liver failure, moyo (heart failure), mapafu( pulmonary failure), upungufu wa sukari mwilini (hypoglycaemia). Na pia kuwa na vimelea vingi (hyperparasitaemia)
Malaria isiyosugu tunatumia dawa ya Mseto (ALU) na mgonjwa anatumia dawa akiwa nyumbani kwake

Malaria sugu tunatumia dawa ya Quinine kwa njia ya dripu na mgonjwa anapatiwa matibabu chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya. Mgonjwa analazwa hospitalini hadi anapopata nafuu na kuweza kula mwenyewe.

Ushauri: Kama tulivyozungumza malaria ni ugonjwa hatari unaoua kwa haraka hivyo ninawashauri pindi unapohisi una dalili tulizozizungumza hapo awali, wahi katika kituo cha kutoa huduma za afya kilichokaribu na wewe ili upatiwe uchunguzi na kupata tiba sahihi. Usitumie dawa bila kumuona daktari kwani kwa kufanya hivyo utakuwa unaongeza usugu wa dawa mwilini mwako bila sababu ya msingi na pia unahatarisha maisha yako.

**************************************************************************************

9. UGONJWA WA SARATANI

Saratani ni nini?

Saratani hutokana na seli za mwili zilizopoteza mfumo wake wa kugawanyika na hivyo kutokuwa katika hali yake ya kawaida. Seli hizo hukua na kuongezeka bila utaratibu maalum na huweza kusababisha uvimbe. Seli hizi huweza kusambaa sehemu nyingine za mwili kwa mfumo wa damu au limfu (lymph).

Sehemu gani za mwili saratani huweza kutokea?

Saratani huweza kutokea sehemu mbalimbali za mwili zikiwemo matiti, koo, mapafu, kinywa, utumbo mpana, shingo ya kizazi, ovary, tezi ya kiume (prostate), ini, ngozi na damu.

Watu wangapi wanakadiliwa kupoteza maisha kutokana na ugonjwa wa saratani?

Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadilia ifikapo 2030 vifo vitokanavyo na ugonjwa wa saratani itakuwa milioni 12 ikilinganishwa na mwaka 2005 ambapo vifo vitokanavyo na saratani vilikuwa milioni 8. Hivyo kutakuwepo na ongezeko la kiasi cha milioni 4. Hii itakuwa ni idadi kubwa sana ya vifo ikilinganishwa na magonjwa mengine kama malaria, Ukimwi, Kifua Kikuu, vifo vya watoto wachanga, ajali za barabarani, maambukizi ya kifua, kiarusi, na magonjwa ya moyo. Inakadiliwa ifikapo mwaka 2030 idadi ya vifo vitokanavyo na malaria itakuwa chini ya milioni 2. Idadi ya vifo vitokanavyo na Ukimwi na Kifua Kikuu pia vitapungua na vitakuwa milioni 2 kwa ugonjwa wa Ukimwi na chini ya milioni 2 kwa kifua kikuu. Wakati huo huo vifo vitokanavyo na magonjwa ya moyo na kiarusi vitakuwa vinaongezeka sambamba na saratani. Vifo vitokanavyo na magonjwa ya moyo vitakuwa milioni 10 wakati vifo vitokanavyo na kiarusi vitakuwa milioni 8 ifikapo 2030. Kwa hiyo tunaweza kuona jinsi gani saratani inavyozidi kusababisha madhara kwa binadamu hususan wa kizazi kipya.

Inakadiliwa pia kutakuwepo na ongezeko la wagonjwa wapya wa saratani katika nchi zinazoendelea ikilinganishwa na nchi zilizokwisha endelea ifikapo 2020. Wagonjwa wapya kwa mwaka wanakadiliwa kuwa milioni 9 katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania wakati wagonjwa wapya katika nchi zilizoendelea itakuwa chini ya milioni 6 kwa mwaka. Hii inahashiria kwamba saratani itakuwa inaongezeka kwa kasi katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania hivyo kuna haja ya kuchukua tahadhari kukabiliana na tatizo hili ili kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na kuongezeka kwa ugonjwa wa saratani.

Kuzuia saratani ndo jibu sahihi katika nchi zetu zinazoendelea.

Inakuwaje mtu anapata saratani/Saratani inatokeaje?

Kwanza kabisa tujue jinsi gani saratani inavyotokea.

Hatua za Saratani:-

  1. Mtu anajiweka (expose) katika mazingira au vitu kama kemikali au mionzi vinavyoathiri sehemu ya DNA (vinasaba vyake) kwa muda mrefu ambapo vinasaba hizo vinaharibika (DNA damage). Kwa kawaida vinasaba vinaweza kuharibika kwa sababu za kijenetiki wakati seli zinapokuwa zinagawanyika au kutokana na sababu za kimazingira (kemikali, mionzi au dawa za viwandani, aina ya madini kama risasi, zebaki, madini joto, uranium na nyuzinyuzi kama asbestos. Pia baadhi ya virusi kama Hepatitis B usababisha saratani ya ini na human papiloma virus (HPV) usababisha saratani ya shingo ya kizazi). Hali hii ikitokea kuna vinasaba vinavyojaribu kuzuia mugawanyiko huu usitokee na pia kuzuia seli zisife. Vinasaba hivi vinajulikana kama DNA repair na apoptosis. DNA repair inatengeneza au kurekebisha DNA iliyoharibika wakati apoptosis inazuia seli zisife. Hatua hizi zikishindikana kufanya kazi basi vinasaba vilivyoharibika vinakwenda hatua nyingine.
  2. Mgawanyiko wa vinasaba (DNA replication). Kadiri mtu anavyozidi kujiweka katika mazingira hatarishi (continued exposure to carcinogens) basi vinasaba vinagawanyika kwa wingi na pia vikisaidiwa na jeni zinazojulikana kama precursor. Basi mgawanyiko huo unaongezeka sana na hivyo kutengeneza uvimbe ambao tunauita “malignant tumor”. Hatua hizi zinatokea kadiri muda unavyoongezeka. Hii inachukua miaka mingi. Mtu anaweza kuanza tatizo hili akiwa na miaka 5 na ugonjwa ukatokea akiwa na miaka 40.
Changamoto za kuzuia Saratani

Baadhi ya njia au mbinu za kuzuia saratani hazitokani kabisa na njia za utoaji huduma za afya au elimu ya afya kwa umma. Mfano:-

  • Kutofanya mazoezi -physical exercise
  • Sera za mazingira -environmental policies-lower exposures
  • Makubaliano ya kimataifa juu ya kulinda afya-Trade agreements
  • Kodi na mapato yatokanayo na bidhaa za tumbaku na shughuli za viwanda ni ndogo sana
  • Hatua madhubuti zinashindwa kuchukuliwa dhidi ya vitu vyenye nguvu kama sigara na tumbaku, uchafuzi wa mazingira kutokana na shughuli za viwanda na kemikali.
Tufanye nini ili kupunguza uwezekano wa kupata saratani

  • Kwanza kabisa kuwa na sheria kali zinazozuia uharibifu wa mazingira na matumizi ya mazao ya viwanda hususan kemikali na mionzi
  • Kuwepo na kodi kubwa kwenye bidhaa za sigara na tumbaku na pia kemikali na madini kama risasi, zebeki, madini ya joto, uranium na nyuzinyuzi kama asbestos.
  • Kubadili tabia juu ya mtindo wa maisha usiofaa kama ulaji wa vyakula visivyofaa kama vyakula vilivyosindikwa kama bacon, soseji, “hot-dogs”, jibini, baadhi ya vyakula vya makopo na pombe aina ya bia vina kemikali zinazoitwa nitrosamines ambazo husababisha saratani za kinywa, koo, tezi la kiume, utumbo mpana, mapafu na tumbo na vyakula vilivyoota ukungu kama karanga, mkate na nafaka huwa na kemikali zinazojulikana kama aflatoxins ambazo husababisha saratani ya ini.
  • Uvutaji wa sigara na bidhaa za tumbaku husababisha saratani ya mapafu, kinywa na koo.
  • Unywaji wa pombe husababisha saratani yam domo, koo, koromeo, matiti, utumbo mkubwa na ini.
  • Unene husababisha saratani ya matiti, kongosho na ya kizazi na kutofanya mazoezi ya mwili kunahusishwa na sarataniya utumbo mpana, matiti, kizazi, mapafu na tezi la kiume.
  • Kuchukua hatua za pamoja za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kimazingira ili kuzuia sababu za awali zinazosababisha saratani kama kemikali, uhalibifu wa mazingira, kujiweka wazi kwenye mionzi. Hapa tunahitaji sheria na hatua za mtu binafsi (law and individual action)
  • Kuchukua hatua za ulaji (diet) na madawa (drugs) hizi zitasaidia kuzuia sababu za pili zinazosababisha saratani
Hatua za awali za kuzuia saratani (Primary cancer prevention)

  • Ondoa au epuka vitu vinavyosababisha saratani mfano kuepuka utumiaji wa tumbaku au sigara
  • Epuka vyakula vilivyoota fangasi au ukungu
  • Epuka matumizi ya nyama zilizosindikwa na matumizi ya nyama nyekundu
  • Epuka matumizi ya pombe
  • Fanya mazoezi ya mwili
  • Kuwa na uzito wa mwili ulio sahihi
  • Tumia zaidi vyakula vitokanavyo na mimea
  • Punguza matumizi ya chumvi
  • Tibu kabisa wadudu wanaosababisha vidonda vya tumbo (H. Pylori eradication) na pia pata chanjo ya kuzuia virusi vya shingo ya uzazi Human Papilloma Virus Vaccination
  • Epuka mionzi itokanayo na shughuli za viwandani (occupational hazards e.g. asbestos)
  • Epuka uharibifu wa mazingira kwa kumwaga kemikali kwenye mito kutoka viwandani na pia maeneo wanayoishi watu.
  • Kuchunguza vichocheo vya saratani (screening of precursors) kwa mfano uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya utumbo mpana.
  • Kupata chanjo dhidi ya virusi vya Human Papilloma Virus (vinasababisha saratani ya shingo ya kizazi) na Hepatitis B na C Virus (usababisha saratani ya ini)
Hatua za pili za kuzuia saratani (Secondary cancer prevention)

  • Uchunguzi wa saratani mapema (screening-early detection) unasaidia kugundua saratani mapema hivyo vifo vitokanavyo na saratani vitapungua kwani matibabu uanza mapema kabla saratani haijasambaa.
Uchunguzi wa matiti

Uchunguzi wa mapafu

Uchunguzi wa tezi la kiume

Uchunguzi wa utumbo mpana

Na pia hatua zote za awali za kuzuia saratani

Hatua ya tatu ya kuzuia saratani (Tertiary Cancer Prevention)

  • Dawa
  • Hatua za awali za kuzuia saratani
**************************************************************************************

10. MAGONJWA YA KURITHI KUTOKANA NA NDUGU WA DAMU KUOANA

Nini madhara ya kiafya yatokanayo na ndugu wa damu au wajomba kuoana?

Kwa kawaida binadamu wana nakala (copy) mbili za jeni yaani sehemu ya DNA inayorithisha tabia au umbile fulani inayoitwa kitaalamu “XY sex Chromosome”. Watu wengi kwenye jamii asilimia 99% wana nakala mbili za jeni zilizona afya nzuri yaani (“Healthy D gene”) DD.

Asilimia 1%, wana jeni moja yenye ugonjwa ambayo kitaalamu inaitwa (“One copy of the diseased gene”) Dd.

Jeni iliyo na ugonjwa inaitwa “Recessive”. Jeni hii iko kwa mama (mwanamke). Jeni isiyo na ugonjwa iko kwa baba ambayo uitwa “Dominant gene”.

Kwa kawaida watu wana afya nzuri isipokuwa wakiwa na jeni mbili zenye ugonjwa yaani “diseased gene” (dd).

Iwapo mama yako amebeba nakala moja ya jeni (Dd) iliyona ugonjwa, basi unakuwa na asilimia 50% ya kurithi hiyo jeni na pia watoto (siblings) utakaowapata watarithi hiyo jeni.

Ukioa mwanamke au kuolewa na mwanaume yeyote kwenye jamii ambaye hamna uhusiano wa kuzaliwa pamoja (hapa tunaongelea ile asilimia 1%, una asilimia 0.5% yakupata jeni yenye ugonjwa.

Kama unaoa ndugu yako, uwezo wa kupata jeni yenye kasoro (ugonjwa) itaongezeka hadi kufikia asilimia 25%. Kwa hiyo kama mtu atamuoa ndugu yake bado asilimia ni ndogo ya kupata jeni iliyo na ugonjwa. Lakini ukizidisha asilimia ya kuwa na jeni iliyona ugonjwa; hivyo itaongezeka na kuanza kuwa na hofu.

Kawaida watu wanaooana ndugu kiwango cha kuenea kwa jeni yenye ugonjwa ni mara mbili zaidi ya watu wasio ndugu. Ndugu wa baba na mama mmoja ni asilimia 50% ya kuwa na jeni ya ugonjwa. Wajomba (cousin) ni asilimia 12.5%.

Magonjwa ya kurithi:-

  • Hemophilia-Ugonjwa wa damu kushindwa kuganda kwa mfano ukijikata au kupata ajali na kukatia sehemu yeyote katika mwili na hivyo kushindwa kuganda damu sehemu inayovuja.
  • Miguu mifupi au small feet.
Ndoa za ndugu katika jamii yetu:

Kutokana na Sheria ya Ndoa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1971 (The Law of Marriage Act, Reversed Edition 2002) kifungu cha 14 kinakataza ndoa za ndugu wadamu kuoana. Pia baadhi ya dini hususan za Kikristu zinazuia ndoa za aina hii. Baadhi ya madhehebu mengine yanaruhusu ndoa za aina hii. Lakini madhehebu haya sidhani kama yapo katika nchi yetu.

Lakini ndoa za aina hii zimekuwa zinatokea sana katika familia za kifalme maeneo kama:

  • Kusini Mashariki mwa Asia (India, Nepal, Bangladeshi, Pakistan)
  • Israel
  • Saudi Arabia


11. MAUMIVU YA TUMBO WAKATI WA KUANZA HEDHI

Maumivu wakati wa hedhi kitaalamu hujulikana kama “Menstrual cramps” au “Dysmenorrhea” au “Period Pains”. Ni maumivu ambayo wasichana ujihisi chini ya kitovu na huzitokeza kabla ya kuanza hedhi na pia wakati wa hedhi.

Wakati wa kupata hedhi, msichana huwa na mabadiliko katika via vyake vya uzazi. Ukuta wa mfuko wa uzazi, ambao umehifadhi damu ulikuwa tayari kupokea mimba humomonyoka kama yai halikurutubishwa. Damu ndani ya mfuko wa uzazi hufanya misuli ya mfuko huo kujikamua ili damu itoke nje. Kujikamua huku kwa kizazi ndiyo kunasababisha hayo maumivu na wanawake wengi huwa na maumivu kama haya.

Aina ya maumivu wakati wa hedhi:

Kuna aina mbili za maumivu wakati wa hedhi.

  1. Maumivu ya awali wakati wa hedhi (Primary dysmenorrhea): Aina hii ya maumivu ndo huwapata sana wasichana. Ni maumivu ambayo hutokea kwenye tumbo wakati wa hedhi hususan hutokea chini ya kitovu na pia nyuma ya mgongo kwa chini karibu na kiuno. Huanza siku 1-2 kabla ya kuanza hedhi na huendelea siku ya 2 hadi ya 4. Hakuna tatizo lolote la kiafya linalosababisha maumivu haya.
  2. Aina ya pili ya maumivu wakati wa hedhi (Secondary dysmenorrheal): Ni maumivu ambayo hutokana na tatizo la kiafya kama kuongezeka kwa misuli ya tumbo la uzazi kwa nje (endometriosis), uvimbe katika tumbo la uzazi (uterine fibroids) au maambukizi katika viungo vya ndani vya uzazi (Pelvic Inflammatory Disease-PID).
Nani hupata maumivu wakati wa hedhi?

Karibu nusu ya wanawake wote hupata maumivu wakati wa hedhi na karibu 15% ya wanawake hueleza kupata maumivu makali wakati wa hedhi. Imeonekana pia kuwa wanawake wasiofanya mazoezi hupatwa na maumivu wakati wa hedhi.

Mambo mengine hatarishi yanayohusishwa na maumivu wakati wa hedhi ni kama:

  • Kuwa msichana chini ya miaka 20
  • Kuvunja ungo katika umri wa miaka 11 au chini ya hapo
  • Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi kitaalamu tunaita “Menorrhagia” (Heavy bleeding during periods)
  • Kama mwanamke hajawahi kuzaa au kupata mimba.
Nini husababisha maumivu wakati wa hedhi?

Kila mzunguko wa hedhi, kama hakuna mbegu ya kiume ya kurutubisha yai la kike, ukuta wa mfuko wa uzazi, ambao umehifadhi damu iliyokuwa tayari kupokea mimba humomonyoka kama yai hilo halikurutubishwa. Damu ndani ya mfuko wa uzazi hufanya misuli ya mfuko huo kujikamua ili damu itoke nje. (the uterus contracts to expel its lining). Kujikamua huku kwa kizazi ndiyo kunasababisha hayo maumivu na wanawake wengi huwa na maumivu kama haya. Hatua hii huchochewa na hormone zenye vitu vijulikanavyo kama “Prostaglandins” ambavyo huhusishwa na maumivu haya na pia maambukizi katika hatua za juu. Pia vitu vingine ambayo hujulikana kama “Leukotrienes”hutolewa kwa kiasi kikubwa wakati wa hedhi na hivi husababisha maumivu wakati wa hedhi.

Nini dalili za maumivu wakati wa hedhi?

Dalili za hedhi ni:

  • Maumivu yanayochoma kwenye tumbo husasan chini ya kitovu
  • Maumivu nyuma ya mgongo karibu na kiuno na pia kwenye mapaja
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Kutokwa jasho
  • Kizunguzungu
  • Maumivu ya kichwa
  • Kupata choo chepesi au kukosa choo kabisa
Utatambuaje kuwa una maumivu wakati wa hedhi?

Mara nyingi wanawake hujitambua kuwa na maumivu wakati wa hedhi hata bila msaada wa Daktari. Kama ni mara ya kwanza inaweza kuwa vigumu kujitambua na hivyo kukulazimu kwenda kumuona daktari na pia kama unahusisha maumivu hayo na tatizo lolote la kiafya. Hapa Daktari anaweza kukusaidia kutambua kama maumivu haya ni maumivu yanayotokana na mabadiliko katika mzunguko wa hedhi au maumivu yanatokana na tatizo la kiafya.

Matibabu ya maumivu wakati wa hedhi.

Maumivu wakati wa hedhi hutibiwa na dawa zinazojulikana kama “Anti-prostaglandins” ambazo hupunguza maumivu katika kuta za mfuko wa uzazi na kufanya hedhi kutoka nyepesi na kukupatia nafuu. Mfano wa dawa hizi ni Ibuprofen au naproxen.

Wakati mwingine Daktari anaweza kutoa vidonge vya uzazi wa mpango ili kuzuia kukua au kukomaa kwa yai la kike na hivyo kupunguza maumivu wakati wa hedhi.

Unawezaje kuepuka na maumivu wakati wa hedhi?

Unaweza kuepuka maumivu wakati wa hedhi kwa kufanya yafuatayo:

  • Kula matunda na mboga za majani
  • Kuepuka vyakula vya mafuta, pombe, caffeine, chumvi na peremende
  • Kufanya mazoezi mara kwa mara
  • Kuepuka au kupunguza msongo wa mawazo
  • Yoga au relaxation therapy
  • Acupuncture au acupressure
Ushauri: Iwapo maumivu yatakuwa makali sana nap engine kutokwa na damu nyingi kuliko kawaida au kuendelea na hedhi kwa siku zaidi ya sita; basi hii ni dalili ya kuwa na tatizo la kiafya. Ninakushauri umwone mtaalamu wa afya kwa uchunguzi na tiba.



12. TATIZO LA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI KWA WANAWAKE/ VAGINAL ITCHING

UTANGULIZI

Nimekuwa nikipokea ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa wapenzi wasikilizaji wa kipindi chetu cha “IJUE AFYA YAKO” wengi wakilalamika kusumbuliwa na muwasho sehemu za siri. Ninapenda kutumia fursa hii kuwaelimisheni kwa ujumla kwani maswali yamekuwa yakifanana.

Leo katika kipindi chetu cha Ijue Afya Yako tutaongelea tatizo la kuwashwa sehemu za siri kwa Wanawake.

Kwa kawaida kuwashwa sehemu za siri husababishwa na maambukizi ya fangasi na maambukizi mengine ya bakteria watokanao na kujamiana. Wakati mwingine alegi pia inaweza kusababisha mwasho.

Muwasho maeneo ya ndani ya uke au kwenye mashavu ya uke husababishwa na mambo mengi. Muwasho ndani ya uke (vagina) unaweza kutokana na matumizi ya kemikali, sabuni zilizowekewa dawa ya kuua bakteria ( detergents or soaps), kuosha ndani ya uke na sabuni zenye dawa ya kuua wadudu au kuondoa harufu (kitaalamu tunasema vaginal douching) kitendo hiki husaidia kuua bakteria wanaoishi kwenye uke (normal flora) kwa ajili ya kuulinda, kutumia cream kwenye uke, karatasi za chooni (toilet papers), sabuni za bafuni (bath products), madawa ya usafi kwa akina mama (feminine hygiene products) na njia za uzazi wa mpango.

Wanawake ambao wameacha kuingia kwenye hedhi wanaweza kupata mwasho kutokana na kubadilika kwa kiwango cha homoni ya Oestrogen. Kwa kipindi hiki kuta za uke huwa nyembamba na kukauka na hivyo kupelekea kupata mwasho.

NAMNA GANI TUNAWEZA KUZUIA MWASHO SEHEMU ZA SIRI?

Wanawake wanatakiwa kuchukua hatua zifuatazo kuzuia mwasho sehemu za siri:

  • Namna ya kujitawaza baada ya haja ndogo na kubwa: Wanawake wanashauriwa kujitawaza kutokea mbele kuelekea nyuma ili kuzuia bakteria wa kwenye njia kubwa ya choo (anus) kuingia kwenye uke (vagina)
  • Kuzuia matumizi ya kemikali, sabuni zilizowekewa dawa ya kuua bakteria ( detergents or soaps), kuosha ndani ya uke na sabuni zenye dawa ya kuua wadudu au kuondoa harufu (kitaalamu vaginal douching), kutumia cream kwenye uke, karatasi za chooni (toilet papers), sabuni za bafuni (bath products), madawa ya usafi kwa akina mama (feminine hygiene products)
  • Kuzuia matumizi ya pads na sabuni zilizowekewa dawa ya kuua wadudu.
  • Kuhakikisha sehemu za siri ni kavu baada ya kuoga.
  • Wanashauriwa kuvaa nguo za ndani ambazo hazibani sana ( Wear loose natural fiber underwear and clothing)
  • Badilisha nguo za ndani angalau kila baada ya masaa 24
  • Hakikisha sehemu za siri ni safi na kavu
  • Jikaushe vizuri baada ya kuoga.
  • Zuia kukaa na nguo zenye unyevunyevu kwa muda mrefu
  • Zuia kufanya ngono zembe.

13. UGONJWA WA FANGASI ZA UKENI/VAGINAL CANDIDIASIS

Fangasi za ukeni ni nini?

Fangasi za ukeni hujulikana kama Candida. Na zile zinazosababisha ugonjwa ukeni zinajulikana kama Candida Albicans. Fangasi hawa husababisha mwasho mkali sana, uvimbe kwenye kuta za ukeni na pia mtekenyo.

Fangasi hawa pia huweza kuambukizwa kwa njia ya kujamiana ingawa wengi hawazihusishi na magonjwa ya kujamiana.

Unapataje fangasi hawa?

Kawaida fangasi hawa kwa asili hupatikana kwenye maeneo ya ukeni. Lakini ukuaji wake huthibitiwa na bakteria wanaoishi ukeni wajulikanao kama “Lactobacillus”. Bakteria hawa huwafanya fangasi hawa wasikue lakini pindi bakteria hawa wanaposhindwa kufanya kazi vizuri basi fangasi hawa ukua na kuanza kusababisha madhara.

Fangasi hawa hutibika kiraisi sana. Kama hunapata fangasi hawa mara kwa mara au wanarudiarudia basi inawezekana kuwa fangasi hao ni wa aina nyingine hivyo Daktari anahitaji kukufanyia uchunguzi zaidi wa kimahabara.

Sababu nyingine zinazofanya mwanamke kupata fangasi za ukeni ni:

  • Matumizi mabaya ya dawa za antibiotikisi. Dawa hizi huua bakteria “Lactobacillus” wanaoishi ukeni kwa ajili ya kulinda uke. Hawa bakteria wanaitwa bakteria wazuri kwani wanatoa ulinzi.
  • Mwanamke akiwa mjamzito huwa kinga ya mwili hupungua au kushuka na hivyo kupelekea kupata fangasi hawa kiraisi.
  • Mwanamke mwenye ugonjwa wa kisukari aliyeshindwa kuuthibiti
  • Kuwa na upungufu wa kinga mwilini hususani kwa wale wanaoishi na Virusi vya Ukimwi
  • Kula vyakula vyenye sukari nyingi
  • Kubadilika kwa homini katika mzunguko wa hedhi
  • Msongo wa mawazo
  • Kuosha ukeni (douching) kwa kutumia sabuni za kemikali na cream
  • Hukosefu wa usingizi wa kutosha
Dalili za Fangasi za ukeni

  • Mwasho ukeni
  • Kujikuna ukeni
  • Kutokwa na uchafu ukeni, mara nyingi unakuwa na rangi nyeupe kama maziwa na pia yanaweza kuwa kama mgando. Wakati mwingine uchafu huu unaweza kuwa kama maji.
  • Maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa
  • Michubuko
  • Viupele
Namna ya kutambua Ugonjwa

Ukienda hospitali Daktari atachukua maelezo yako namna gani tatizo hili limeanza na kama umewahi kuwa na shida kama hiyo hiyo na dawa ulizokwisha tumia na pia kama umewahi kupata magonjwa yoyote ya kujamiana. Kisha atakufanyia uchunguzi kwa kutazama sehemu zako za siri hususan kwenye kuta za uke na pia ndani kuona shingo ya uzazi. Kutokana na Daktari atakayoona anaweza kuamua kuchukua kipimo kwa ajili ya mahabara. Kipimo hiki kinaitwa “Vaginal Culture”

Matibabu ya Fangasi za ukeni

Matibabu yanategemea kiwango cha maambukizi pamoja na madhara ya ugonjwa

a) Maambukizi madogo: Mara nyingi Daktari wako atakupatia dawa za kumeza kwa siku chache, kupaka au kuweka ukeni. Dawa hizi unaweza kutumia siku moja hadi tatu. Dawa zinazotumika ni kama Gynazole (Gynazle), Lotrimin, Monistat na Terazol.

Dozi moja ya dawa ya kumeza inaweza kutumika mfano Diflucan

Ushauri: Husitumie dawa yoyote bila kuandikiwa na daktari. Ukihisi una tatizo hili ni vema uende kituo chochote cha Afya kilichokaribu nawe ili umwone Daktari kwa matibabu na ufuatiliaji pindi tatizo linarudia katika kipindi cha miezi miwili.

b) Maambukizi makubwa: Haya huhitaji matibabu makubwa zaidi.

Ukiwa na dalili hizi ni vema ukamuone daktari:

  • Mwasho mkari
  • Umepata maambukizi ya fangasi mara nne kwa mwaka mmoja
  • Uvimbe
  • Ngozi ya ndani imekuwa nyekundu
  • Una ujauzito
  • Una kisukari
  • Au unaishi na virusi vya ukimwi
Matibabu hapa yanaweza kuwa kama ifuatavyo:

  • Siku 14 za kupaka dawa (cream, ointment), vidonge vya kumeza au kuweka ukeni
  • Dozi mbili au tatu za Diflucan (Hii haitumiki kwa mwanamke mjamzito)
  • Matumizi ya dawa kwa muda mrefu angalau wiki sita hususan Diflucan ambayo unameza kidonge kimoja kwa wiki kwa wiki sita au dawa ya kupaka ukeni kwa kipindi cha wiki sita
  • Kumtibu mwenzi wako la sivyo tatizo litarudiarudia.


Jinsi ya Kuzuia maambukizi ya Fangasi za ukeni.

Ni vema kutambua nini kilikusabibishia kupata maambuki haya. Kwa mfano Wanawake wengine husema walipata maambukizi haya baada ya kutumia dawa za antibiotikisi. Ukitambua kitu kilichokusababishia tatizo hili basi unaweza kuzuia isitokee tena.

Mambo mengine ya kusaidia kuzuia maambukizi haya ni:

  • Zuia kuvaa nguo zinazobana
  • Zuia kuosha ukeni kwa kutumia kemikali za kike, cream, sabuni zilizowekewa dawa, deodorants na pads
  • Husivae chupi mbichi
  • Vaa chupi za pamba
  • Kula chakula chenye virutubisho vya lactobacillus kama yogurt
  • Fua chupi kwa maji ya moto


Kwa ushauri au maswali wasiliana na:

Dr. Willfredius Mugishagwe Rutahoile

Tel: +255755649102 au +255715223646

Email: info@hmtz.co.tz au rutahoile@hmtz.co.tz

chanzo.Health Media Tanzania
 
Back
Top Bottom