Kakalende , nipo katika rekodi ya kuonyesha bunge la katiba litakavyokuwa. Rejea nyuzi za duru.Mkuu Nguruvi3, heshima mbele. Nimefuatilia huu uzi naona kama unatumia nguvu ya ziada kumpiga mawe SS kunani? Hata ka mwenyekiti wa BMLK angekuwa mtu mwingine unadhani ccm wangeacha kutumia wingi wao kushawishi matokeo ya mchakato huu?
Wapenda mabadiliko na demokrasia inabidi waangalie walipojikwaa na sio wanapoangukia, inabidi kujiuliza imekuwaje ccm wakawa wengi kwenye mabunge haya na iwapo wao ccm wanaona status quo inawapendelea kwa nini wasifanye kila hila mambo yabaki hivi yalivyo?
Kuna kambi fulani za wasaka uraisi ccm wamewekeza sana kiasi kwamba wasingependa katiba mpya kama ilivyoletwa kwenye rasimu na watafurahi zaidi iwapo mchakato huu utakwama. Tishio la wana-ukawa kujitoa, ni sawa na kumsusia ngedere shamba baadhi ya watu watasherehekea.
Sehemu IV
BUNGE LA KATIBA LITAVUNJIKA, SITTA ATAHITIMISHA SAFARI YA KISIASA
Bunge la katiba lina mvutano wa mudakuanzia mchakato hadi lilipofikia.
Kuna uvumilivu kwa mwanadamu na kipo kiwango.
Wapenda mabadiliko wamevumilia mengi ikiwemo la Sitta kubadilisha kanuni kwasababu ana 'busara sana' kuliko kamati zailizoandika kanuni hizo.
Chuki zilianza siku za nyuma, zikahamania bunge la katiba katika kanuni.
JK analaumiwa kwa hotuba ya kumfedhehesha Warioba. Hata kama yalikuwa maagizo yake, bado mzigo wa kukiuka kanuni na kuwasaliti wananchi upo begani kwa Sitta.
Lau angewasikiliza wanakamati wenzake leo asingekuwa anazungumziwa.
Sitta akaamua, kwanza kuitukana kamati iliyoandaa kanuni kwa kitendo cha kusema 'Yeye anabusara na ndizo zinamuongoza' tafsiri ya kwamba kamati haikuwa na busara katika maamuzi.
Pili, mzigo wa dhalili ya tume Warioba ni matokeo ya Samwel Sitta kupindisha taratibu
Tatu,kuunda kamati za CCM utakaopelekea machauko ni matokeo ya Sitta kuendekeza UCCM katika mambo ya kitaifa.
Wakati mswada wa kwanza unatolewa, Samwel Sitta alipangwa Zanzibar.
Huko alikumbana na nguvu ya wananchi kwa kuchoma mswada mbele kukiwa na vurugu kubwa.
Wananchi wa znz walimheshimu Sitta japo kwa kumsikiliza.
Ingekuwa akina Nap moto ungewaka zaidi.
Sitta akarudi kwa JK na kumshauri suala la muungano lijadiliwe kama masuala mengine.
Ni kwa kuona busara hizo na bila kumjua Sitta, wazanzibar walioko Dodoma wakampa uenyekiti
Huyu ni ndumila kuwili sasa anatumia upande wa pili kashughulikia wzn kama alivyo ahidi
Sitta kaweka wazi msimamo wa serikali 2 na kwamba muungano ni lazima.
Huu ni ujumbe maridhawa kwa wazanzibar, yale matumaini kuhusu malalamiko yanafikia hatima
Sitta keshasema atawashughulikia na salama ya wazanzibar ni ukimya.
Kama hiyo ndiyo njia waliyoamua, basi tunawatakia heri wznz na Sitta.
Mbele ya safari ni kweusi. Kama wapenda mabadiliko na nchi kwanza wataamua kwa dhati kusimama kidete wakiamini nchi na wananchi kwanza, hakuna sababu za kuwepo Dodoma.
Wananchi watawaelewa pale watakapoondoka Dodoma na kuzunguka nchi nzima wakieleza uhuni unaoendelea Dodoma chini ya uratibu na usaliti wa mzee wetu Sitta
CCM wataandika katiba, wakimaliza wananchi watakuwa wanaelewa nini kinatokea.
Tunakumbuka bajeti iliyoongeza bei za mafuta ya taa ilivyopingwa na wabunge wa upinzani chini ya Sitta. Ilimlazimu Spika atoe mawaziri bungeni kwenda kueleza uzuri wa bajeti ambako walikumbana na mawe na kila rabsha.
Wananchi wanafuatilia kwa umakini nini kinaendelea Dodoma. Kama lipo jambo wanalosubiri ni kusikia bunge maalumu la katiba la CCM na Samwel Sitta linafikia tamati haraka.
Sitta, kwa kujitoa 'mhanga' anakabiliwa na mambo mawili
1. Hasira za wabunge wa upinzani
2. Hasira za wazanzibar
3. Hasira za Watanganyika
4. Hasira za kamati ya kanuni
5. Hasira za umma dhidi ya dhalili kwa maoni yao kupitia Warioba.
Ingawa Sitta haonekani kujali kwa kuangalia masilahi yake 2015, bunge hili la katiba litahitimisha safari yake ya kisiasa. Hadi sasa hivi umma unafahamu kama msaliti wao na mtu anayeweza kutumika kama karatasi za maliwato, baada ya hapo hakuna thamani.
Itaendelea sehemu ya mwisho.....
Ni kweli uyasemayo, sehemu ya V tutaeleza jinsi mkakati huo utakavyomuumiza Sitta personal na CCM kwa ujumla kama watatumia.Big up mkuu kwa uchambuzi makini...
Niweke tu chorus kwa kusema hili BMK liko very delicate. Lakini pia CCM wameshaamua kuwa mchakato wa katiba unaishia hapa. Mbinu zao zote ni kuhakikisha uchaguzi mkuu ujao unafanyika chini ya katiba mbovu iliyopo. Wanajiaminisha kwamba watashinda uraisi. Then wanajua katiba mpya ikipatikana chini ya raisi mpya, huyo raisi atakuwa na maslahi kwenye kila muundo atakaoufanya. Kuanzia tume ya utumishi, jaji mkuu, Mwanasheria mkuu nk. JK sasa hivi anaelekea ukingoni. Katiba mpya ikipatikana chini ya JK hawana uhakika wa control kwenye tume ya utumishi wala tume ya uchaguzi.
Bila shaka hayo yalishaamuliwa katika vikao vyao kuwa hawaendi kwenye uchaguzi ujao na katiba mpya. Sitta anafahamu na yuko tu pale kuuza sura kwa maslahi ya uraisi 2015 CCM huku akifanya delaying techniques za kuahirisha bunge kila siku na kuvuruga kanuni ili mda uishe. Aliyosema Pinda kuwa huenda bunge la katiba likaahirishwa hadi mwakani kupisha mambi mengine ya kitaifa ni uthibitisho kuwa wamejiandaa katika hili...
Mtanganyika,
Non-CCM walijua mchezo huu wakati wa kupitisha sheria lakini as you said CCM had the upper hand hivyo sheria ikapita na sasa, statistically, wana wajumbe wengi.
Lakini za mwizi arobaini, hitaji la 2/3 kwenye kupitisha vifungu inawarudisha kwenye ground zero. CUF na CCM zanzibar wako sawa. Yes Non-CCM hawawezi kupitisha vifungu lakini wana uwezo wa kukwamisha na kusambaratisha mambo.
Lakini mtihani mkubwa uko uraini Zanzibar. Hapa ndio CCM (kwa uelewa wangu) waliuziwa mbuzi kwenye gunia! Kati ya wana CCM Zanzibar wanaon-cooperate na CCM makao makuu hakuna hata mmoja mwenye ubavu wa kuzima moto uraiani.Hakuna.Watapayuka sana lakini mwisho wa siku watanyukwa vibaya na wananchi.
Kwa maoni yangu mchakato wote wa katiba mpya mwenye upper hand ni CUF Zanzibar.
Mkuu hata huko Zanzibar ni fact kwamba CCM wanajua kwamba kelele zitakuwepo for few days, watadeploy wanaume kutoka Tabora watakwenda huko na vibao vitatembea na mwisho wa siku kila mtu atabaki na mkewe chumbani. CCM wa Zanzibar au Tanzania Bara wanafanana, wanapenda madaraka na wanajua fika kabisa ukigeuza mkondo basi VX zinaamia kwa jirani. Ukweli CCM wamewakea mfukoni USA na EU (wapigaji kelele wa haki za binadamu) ambao wao wote wanataka muungano ubaki kama ulivyo kwa hofu zao kwamba Ukikatika tuu basi Vijana wenye mlengo wa kigaidi wataamia Visiwani. Na hii ni hofu na ujinga lakini ukweli upo palepale. Kwamba CCM wanafahamu kwamba karata zao ni madume na majike na Majokeli yote wanayo wao. Hivyo hili jambo la katiba kura za wazi za siri ni kutimiza hesabu na kusema mlitaka katiba mpya hii hapa na dunia imeona.
Kwenye USA, EU etc uko sahihi maana hata press release ya No 10 juzi kuhusu maongezi ya Cameroon na mkulu walitaja "hatari ya kuongezeka kwa extremists!'
Kuhusu kubwaga vijana toka Tabora itakuwa kosa of historical proportion. CNN wataweza kutupa counts! Unajua success waliyokuwa wanapata vijana wa Tabora huko nyuma ilitokana na 'ushirikiano'. Sasa hakuna kitu cha namna hiyo, sasa hivi ni Zanzibar kwanza.
Na moja ya mapungufu ya Muungano wa sasa (sio ule wa Nyerere) ni kutofahamiana kati ya ccm Zanzibar na Bara. and post 2010 mambo ni mabaya zaidi.
Sitta alichaniwa makaratasi Bwawani, na kama angekuwa ni mtu wa kuona mbele angewaongoza ccm wenzake huko Dodoma ili waachane na 'cosmetic' thinking. So far ccm wanacheza mkanda ule ule wa zamani. kosa.
CNN au BBC ni walewale kaka, yaani kama kuna jambo ambalo Wazanzibar watakosea ni kulianzisha, kwani watachapwa na hakuna atake ingilia. Ndio maana nimewai kusema Zanzibar hawana strategic, politicaal, economical au geographic advantage kwenye hili. Wanapigana mikono yao ikiwa imefungwa nyuma, kusema kwamba watoe macho hilo litafanyika kwa week tuu kama Mtwara, leo bomba la gesi lipo Kinyerezi.
Advantage ya CCM ni kwamba wanao wapa mkono ndio vilanja wa dunia and that is sad fact.