Kwa kweli CCM mwaka huu imetia fora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa kweli CCM mwaka huu imetia fora

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Quinine, Jul 31, 2010.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,201
  Trophy Points: 280
  haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa tanganyika rushwa nje nje, ngumi mkononi, takukuru kama chui wa karatasi.

  [​IMG]
  Wasimamizi wa mkutano wa wanachama wa CCM Kata ya Kigogo, Dar es Salaam wakimtoa nje ya ukumbi mmoja wa mwanachama aliyesababisha vurugu kutokana na kumuuliza swali la utatanishi mgombea, Shyrose Bhanji (kushoto) wakati wa mkutano wa kuomba kura wa wagombea Ubunge jimbo la Kinondoni, uliofanyika kwenye kata hiyo jana.
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Si kwamba wametia fora ila ndo yamebumburuka manake ilikuwa hivi tu!
   
 3. rancosys

  rancosys Member

  #3
  Jul 31, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli Yameonekana wazi yalikua yamefichika! Lakin nisawa na mwenda wazim kuvua nguo mbele ya kadamnasi ya watu,, Hawato mshangaa. Japo nihatari katika macho ya wanajamii wa lika mbalimabli.
  Kinacho fanyika sasa nikua Haki na sheria Ni dhahiri kua hazina maana yeyote katika taifa BUBWI hili.
  Mengi yanayo keuka sheria yanafanyika na yakiwa na ushaidi Dhahiri, lkn Hatua za KIJUHA zitachukuliwa kumlinda muharifu.

  stano-corruption.jpg flag.jpg
   
 4. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,201
  Trophy Points: 280
  WATU wanne wanashikiliwa Polisi mkoani Singida kwa tuhuma za kuvamia kituo cha kupigia kura na kupora sanduku la kura za maoni kwa wanachama wa CCM na kuzichoma moto kabla hazijahesabiwa .

  Uvamizi huo ulifanyika juzi kwenye Kijiji cha Iglansoni katika jimbo jipya la Singida Magharibi na kusababisha matokeo ya kura za maoni kutotolewa mpaka jana mchana.

  Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Celina Kaluba uvamizi huo ulifanyika Agosti mosi mwaka huu majira ya saa 12:30 jioni.

  Kaluba aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Shambuli Shija (44), Manyanda Lazima (46), Clement Richard (36) na George Petro (38) wote wakazi wa Kijiji hicho cha Iglansoni katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida.

  Alisema siku ya uvamizi, baada ya kumalizika kwa upigaji kura za maoni kwa wana-CCM, watuhumiwa hao walipora sanduku la kura kabla ya kuhesabiwa na kisha kuchoma moto.

  Kaluba alisema ingawa haijafahamika rasmi sababu za kufanya hivyo, lakini inadhaniwa kuwa huenda walifikia uamuazi huo ili kuharibu matokeo baada ya kuona dalili za kushindwa kwa mgombea waliyekuwa wakimuunga mkono.

  Kutokana na hali hiyo alisema wanaendelea kuwashikilia watu hao kwa ajili ya uchunguzi zaidi kabla ya kupandishwa kizimbani.
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Jamani mie naojionea raha tupu. Kama visa vyenyewe ndo hivi siasa tamu jamani. lkn nadhani tunakoelekea huko watu watakuwa na majeshi saas na si wapambe
   
 6. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,201
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa ukiangalia hali inayoonyeshwa na CCM haihitaji kuwa na wapambe tu bali jeshi la wapambe waliojiandaa ngumi mkononi, wizi nk, lakini mbona mwakalinga alikuwa na jeshi na halijamsaidia?
   
Loading...