Kada wa CHADEMA
JF-Expert Member
- Feb 27, 2016
- 289
- 615
Usisubiri mpaka ugongewe mlango wa kukuambia toka. Jipime mwenyewe na uondoke kabla hujafukuzwa kwa mawe. Najua wapo watakaokutetea kwa kusema hizo ni tuhuma tu. ila niwaambie kitu, kutuhumiwa ni kubaya zaidi kuliko kukutwa ukitenda.
Kwa mtu mwenye akilo timamu, hawezi kuendelea kubeba dhamana ya kuongoza chama huku akiwa na tuhuma lukuki na nyingi zikithibitika kuwa za kweli. Ilianza tuhuma ya kupanga jengo la NHC na kuishi bila ya kulipa pango na hivyo kudaiwa zaidi ya bilioni 13. Ilianza kama tetesi ila Mahakama ikapigilia msumari wa mwisho. Hatimaye vifaa vyote pale Bilicanaz vikatolewa nje kwa aibu.
Zikaja kashfa za kufanya biashara kupitia Hotel bila ya kulipa kodi. Hadi hivi sasa Mwenyekiti wangu Mbowe anadaiwa kiasi kikubwa cha kodi. Awali ilionekana ni uzushi. Ila kadri siku zinavyoenda ukweli unajulikana na Mbowe amekumbwa na aibu tele.
Kashfa hiyo haijapoa linaibuka kasheshe jingine la kutuhumiwa kuharibu vyanzo vya maji huko wilqyq ya Hai na hivyo kusababisha ukame. Kashfa hizi ni visible. Kila mtu anaona na ameridhia. Mwenyekiti wangu ni mharibifu wa mazingira.
Sasa limeibuka hili la kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya. Wapo wapuuzi humu wanamtetea eti kwamba anaonewa kwa maslahi ya kisiasa. Upuuzi wa hali ya juu. Wale waliokuwa wanatembelea pale Bilicanaz Club watakubaliana nami kuwa kilikuwa ni kijiwe muhimu cha mihadarati. Mbowe alikuwa anajua na ndio ilikuwa inampatia kipato kikubwa. Wasanii wengi wameharibiwa na Mbowe kupitia Bilicanaz Club.
Hizi ni kashfa kubwa sana. Ifike wakati Mbowe uone aibu. Si vema kwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni kuwa na rundo la kashfa namna hii. Huaminiki tena katika jamii. Watu wanakuangalia kwa wasiwasi na kijicho upande. Wanaokuambia kuwa unahujumiwa kisiasa hawakutakii mema.
Jiuzulu baba kabla jina lako halijachafuka sana. Kujiuzulu si ujinga. Ni namna ya kutunza heshima na hakika utakumbukwa kwa mchango wako ndani ya chama chetu. Ila ukiendelea kung'ang'ania basi uwe tayari pia kupokea na matokeo yake. Yawe Hasi ama Chanya.