"Kwa jina la....... Utafaulu", 'Mambongwa'

"Kwa jina la....... Utafaulu", 'Mambongwa'

dalalitz

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2013
Posts
3,475
Reaction score
2,078
Ni kauli ya Mama Mzazi kwa bintiye wa Darasa la Saba akiwa ndio anarejea kutoka Shule siku ambayo binti alipaswa kufanya Mtihani.

Na nukuu,
Mama,
".... Marahabaa mwanangu,
Pole kwa Uchovu,
Enhee, Vipi?
Mtihani ulikuwaje?

Mtoto,
" Mh, Kiasi mgumu Ila, nitafanya vizuri tu Mama.

-Ukakasi kwangu:

Mama,
"Kwa jina la..... ..... (akamtaja mchungaji mmoja maarufu),
Utafaulu tu,
Chezea............ (Akamtaja tena)
Si ulikumbuka kunywa yale Maji ya Uzima?
Utaona mwanangu, - Nambari- moja".
Mwisho wa kunukuu.

Sina ngendembwe na kuwajenga watoto kuwa na Imani.
Ila katika hili japo halinihusu limenifikirisha na kupata ukakasi kiasi.

Nimeamini kuwa kuna mambo na Mambongwa pia,
Sijui wewe mdau Unaonaje?
 
imani na kusoma, kama kasoma atafaulu hata bila hayo maji
 
Back
Top Bottom