Kwa January Makamba tu

Kwa January Makamba tu

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,252
Reaction score
16,171
Sikudhihaki ndugu yangu wa Bumbui, lakini tofautisha kati ya kazi, fedha, madaraka, huduma na personal satisfaction.
Watu wa kizazi kipya kama chako huwa wanaitazama na kuiona Tanzania kwa jicho la kisasa zaidi na lenye matumaini makubwa kuliko wazee. Tuwashukuru wazee wetu kwa kututafutia uhuru, lakini kazi ya kututafutia maendeleo sio ya kwao tena. Vijana tuna matatizo ya maisha, lakini hatuwezi kutegemea kutatua matatizo yetu kwa kutumia akili ileile na watu walewale waliosababisha matatizo yetu, nilazima tuyatafute majibu hayo nje ya sanduku. Bahati mbaya wazee hawakubali mabadiliko ya haraka na hawana tabia ya kuwaamini vijana hata kidogo kama watawafikisha mbele. Wazee mara zote huwa wana kauli za don't, don't don't nyiiingi kwa vijana kwa kila jambo hadi kufikia kuviua vipaji vya vijana wao.

Kijana kubaki CCM ni sawa na kijana aliyekwenda ng'ambo na kufanya kazi za kutunza wazee kwenye kambi za wezee. Nimewahoji vijana wengi wanaofanyakazi ya kutunza wazee Ulaya na Marekani, wengi wao wanakiri wanalipwa na kupata pesa nyingi lakini hawana raha ya kazi (job satisfaction) kwasababu ya kutumia muda wao mwingi kukaa na vizee.

CCM ni chama cha wazee, huna jipya wewe kijana utakaloweza kuwaambia(status quo), ndio maana vijana wengi wenye akili nyingi kama zako wanatafuta mabadiliko ya nchi nje ya CCM (outside the box) ili kuepuka kukaa karibu na wazee wa enzi za TANU, KANU, UPC, ZANU-PF, Frelimo, nk ambao kumbukumbu yao hadi leo ni harakati za ukombozi tu basi. Nyimbo zao ni zile za akina Salimu Abdalah, Fundi Konde, na Juma Balo.

Watu kama wewe, Angela Kairuki, Bulaya, Nape, Filikunjombe, n.k mtaleta mabadiliko gani mkiwa katikati ya kundi la wazee wa CCM? sio kama mnatafuta kurogwa tu nyinyi?. Najisikia uchungu sana kuona vijana wenzetu kama nyiye wenye maarifa na weledi mkubwa mkijitenga na mkizomewa na vijana wenzenu majukwaani na sehemu mbalimbali za mijumuiko kwa kutetea chama na sera zilizowafikisha vijana hapa walipo. Huhitaji kuwa na fedha nyingi ili kuwa na furaha, ila unaweza kuwa na furaha iliyopitiliza kama ukigundua kuwa mchango wako umesababisha watu wengine kuwa na amani, furaha na nafuu ya maisha. Ninajisikia mwenye furaha tele kumaliza maumivu aliyokujanayo mgonjwa kwangu na kumfanya arudi tena kwenye jamii kuendelea na kazi zake, najisikia furaha ninapokutana naye mitaani mgonjwa wangu akiwa hana matatizo tena. Unajisikiaje wewe kama January Makamba kutetea chama ambacho kina matokeo ambayo yanakufanya kuwaona vijana wenzako wakiiba mifuniko ya chemba ya majitaka, kuitwa vishoka, kukata alama za barabarani wakauze kama chuma chakavu, kufanya kazi ya kuzunguuka na mashati mawili mitaani kuuza, kupanga bidhaa chini barabara za waenda kwa miguu, kukosa ajira, n.k?

January Makamba na vijana wenzako mlioko CCM, mnajisikiaje kuona vijana wenzenu wengi wanashabikia vyama vya upinzani? mnadhani wana shida gani? wamerogwa? hawana akili au kumetokea nini?

Vijana wamekata tamaa, hawaoni kama ndani ya CCM kuna mtu ambaye hatawadanganya tena kuhusu maisha yao. Hamuoni kama mnaweza kutengeneza tanzania mpya yenye matumaini kwa vijana kwa kuungana na vijana wenzenu nje ya CCM?
 
Safiiii nakupa like zote, ila sidhani kama watakuelewa walishalipwa kutoona na kutosikia ni vigumu kujinasua.
 
ujana siyo umri kaka bali ni mawazo na matendo ya mtu usika. january makamba ni mtu mwenye mawazo na fikra ya kizee mfano mzuri ni sheria zilizotungwa kuhusiana na matumizi ya internet hakuna kijana hanaweza kuwa na akili ya ku limit matumizi ya internet katika karne hii badala ya ku expand matumizi ya internet. kijana anatakiwa kufikiria namna ya kumsaidia kijana aliyeko kijijini ili apate huduma hiyo ili aweze kuomba kazi na kufanyiwa interview akiwa kijijini ambapo katika ulimwengu wa kileo inawezekana badala ya kutumia muda mwingi kuandika sheria za kubana watu wasiwe na uhuru kamili wa kutumia dhana hiyo kwahiyo ndugu usiwe na mawazo ya kizamani kuangalia ujana kwa umri bali angalia mawzo na fikra za mtu
 
Niseme tu kuwa,hao vijana uliowataja hapo juu wamefika hapo kwa kubebwa na favours. Sio watu wenye akili tofauti sana na kijana wa kawaida wa kitanzania.
Lazima walipe fadhila na kutunza vibarua vyaoz

Nilishawahi kusema hakuna aliyeko ccm anaouwezo wa kutoka ndani ya ccm hata kama anataka,maslahi kwanza nchi baadae,ndio ccm hiyo
 
mpashe huyo anayependa vya dezo mpita bila kupingwa
 
ujana siyo umri kaka bali ni mawazo na matendo ya mtu usika. january makamba ni mtu mwenye mawazo na fikra ya kizee mfano mzuri ni sheria zilizotungwa kuhusiana na matumizi ya internet hakuna kijana hanaweza kuwa na akili ya ku limit matumizi ya internet katika karne hii badala ya ku expand matumizi ya internet. kijana anatakiwa kufikiria namna ya kumsaidia kijana aliyeko kijijini ili apate huduma hiyo ili aweze kuomba kazi na kufanyiwa interview akiwa kijijini ambapo katika ulimwengu wa kileo inawezekana badala ya kutumia muda mwingi kuandika sheria za kubana watu wasiwe na uhuru kamili wa kutumia dhana hiyo kwahiyo ndugu usiwe na mawazo ya kizamani kuangalia ujana kwa umri bali angalia mawzo na fikra za mtu
ukikaa na wazee na wewe na wewe utakuwa na mawazo ya kizee, muda mwingi utautumia kukchekacheka na kujikomba ili kuwaridhisha wao, huwezi kusema hapana mbele ya wazee hata kama wewe unaona ni hapana. Wazee lazima wanawe kwanza ndipo kijana anawe, taifa letu linahitaji vijana wanawe haraka, wale haraka waende wakalijenge taifa lao, maana wao ndio wenye kesho nyingi kuliko wazee. Nina hakika hata sheria ya mtandao January ameshiriki kuiandika na kuitetea kwa kwa shingo upande kwa kutumwa na wazee ili kuwabembeleza wamteue kuwa mgombea urais, na alifanikiwa kufika 5 bora kwa njia ya kujishusha kwa wazee. Kwa mwendo huu tutafika lini vijana wenzangu?
 
Nikiona jina la uyu jamaa naikumbuka mechi ya stars na naigeria pale uwanja wa taifa kipindi cha pili
 
Mabadiliko na el wewe ni tatizo, kuungana na wanywa viroba ni shdaaa
 
Sikudhihaki ndugu yangu wa Bumbui, lakini tofautisha kati ya kazi, fedha, madaraka, huduma na personal satisfaction.
Watu wa kizazi kipya kama chako huwa wanaitazama na kuiona Tanzania kwa jicho la kisasa zaidi na lenye matumaini makubwa kuliko wazee. Tuwashukuru wazee wetu kwa kututafutia uhuru, lakini kazi ya kututafutia maendeleo sio ya kwao tena. Vijana tuna matatizo ya maisha, lakini hatuwezi kutegemea kutatua matatizo yetu kwa kutumia akili ileile na watu walewale waliosababisha matatizo yetu, nilazima tuyatafute majibu hayo nje ya sanduku. Bahati mbaya wazee hawakubali mabadiliko ya haraka na hawana tabia ya kuwaamini vijana hata kidogo kama watawafikisha mbele. Wazee mara zote huwa wana kauli za don't, don't don't nyiiingi kwa vijana kwa kila jambo hadi kufikia kuviua vipaji vya vijana wao.

Kijana kubaki CCM ni sawa na kijana aliyekwenda ng'ambo na kufanya kazi za kutunza wazee kwenye kambi za wezee. Nimewahoji vijana wengi wanaofanyakazi ya kutunza wazee Ulaya na Marekani, wengi wao wanakiri wanalipwa na kupata pesa nyingi lakini hawana raha ya kazi (job satisfaction) kwasababu ya kutumia muda wao mwingi kukaa na vizee.

CCM ni chama cha wazee, huna jipya wewe kijana utakaloweza kuwaambia(status quo), ndio maana vijana wengi wenye akili nyingi kama zako wanatafuta mabadiliko ya nchi nje ya CCM (outside the box) ili kuepuka kukaa karibu na wazee wa enzi za TANU, KANU, UPC, ZANU-PF, Frelimo, nk ambao kumbukumbu yao hadi leo ni harakati za ukombozi tu basi. Nyimbo zao ni zile za akina Salimu Abdalah, Fundi Konde, na Juma Balo.

Watu kama wewe, Angela Kairuki, Bulaya, Nape, Filikunjombe, n.k mtaleta mabadiliko gani mkiwa katikati ya kundi la wazee wa CCM? sio kama mnatafuta kurogwa tu nyinyi?. Najisikia uchungu sana kuona vijana wenzetu kama nyiye wenye maarifa na weledi mkubwa mkijitenga na mkizomewa na vijana wenzenu majukwaani na sehemu mbalimbali za mijumuiko kwa kutetea chama na sera zilizowafikisha vijana hapa walipo. Huhitaji kuwa na fedha nyingi ili kuwa na furaha, ila unaweza kuwa na furaha iliyopitiliza kama ukigundua kuwa mchango wako umesababisha watu wengine kuwa na amani, furaha na nafuu ya maisha. Ninajisikia mwenye furaha tele kumaliza maumivu aliyokujanayo mgonjwa kwangu na kumfanya arudi tena kwenye jamii kuendelea na kazi zake, najisikia furaha ninapokutana naye mitaani mgonjwa wangu akiwa hana matatizo tena. Unajisikiaje wewe kama January Makamba kutetea chama ambacho kina matokeo ambayo yanakufanya kuwaona vijana wenzako wakiiba mifuniko ya chemba ya majitaka, kuitwa vishoka, kukata alama za barabarani wakauze kama chuma chakavu, kufanya kazi ya kuzunguuka na mashati mawili mitaani kuuza, kupanga bidhaa chini barabara za waenda kwa miguu, kukosa ajira, n.k?

January Makamba na vijana wenzako mlioko CCM, mnajisikiaje kuona vijana wenzenu wengi wanashabikia vyama vya upinzani? mnadhani wana shida gani? wamerogwa? hawana akili au kumetokea nini?

Vijana wamekata tamaa, hawaoni kama ndani ya CCM kuna mtu ambaye hatawadanganya tena kuhusu maisha yao. Hamuoni kama mnaweza kutengeneza tanzania mpya yenye matumaini kwa vijana kwa kuungana na vijana wenzenu nje ya CCM?

Kama ni kwa January Makamba tu, y utuandikie sisi? Si umuinbox huyo Makamba aupate ujumbe huo?
 
na wewe kwanini umeusoma na kumjibu? Kwani wewe ndio Makamba J?
Fasihi inakusumbua na ilikusumbua darasani. Dhima ya andiko hilo ni kwa vijana wote mlio wagumu kubadili mfumo wa siasa na utawala wa nchi kwa maslahi yenu na wanenu. Wazee yao ilikuwa jana na leo na kesho ni ya vijana. Kubalini matokeo japo yana gharama zake zinazorekebishika kuliko mfumo huu kandamizi mnaoutetea. Na kwanini vijana wengi mlioajiriwa mnakuwa rigid and conservative kwa kiasi hiki? Badilikeni bwana msiwe kama kanuni za hisabati.
 
Kijana wa Bumbuli aka Janu anatembelea nyota ya kijana wa Mwandiga aka Zana za Kilimo teh...teh...teh....kunani pale? Tanga?
 
Mimi katika watu ninaoshangaa ikisemekana ana uwezo ni pamoja na January. Huyu kijana ni baadhi ya watu wanaobebwa sana bila uwezo. Nilimdharau zaidi juzi alivyotaka kupita bila kupingwa, kama kweli ana uwezo na anadhani anakubalika kwa kile alichofanyia wananchi wake nini kinamfanya atake kupita bila ushindani!? Hawa ndio wale vijana aina ya kina Nkurunzinza ambao wanalazimisha kubaki madarakani. Kwani kama una uwezo mchango wako kwa taifa ni lazima uwe kiongozi? Na kama ni lazima uwe kiongozi ni kwa kulazimisha kupita bila kupingwa?
 
Back
Top Bottom