Kwa ili TFF na Bodi ya Ligi hawako sawa

delako

JF-Expert Member
Oct 6, 2012
2,743
1,492
Habari wana JF,

Nimefuatilia baadhi ya Michezo kwa baadhi ya timu na kugundua kuwa kuna uonevu wa makusudi au kutokujua. Michezo inayozihusisha Simba na Yanga zinachezwa jioni saa 10 kama timu hizo zipo nje ya Dar es Salaam au zinacheza saa 1 usiku Kama zipo Dar. Wakati timu hizi zinacheza michezo yake wakati huo kuna timu zinacheza saa 8 mchana!

Kupishana kwa muda ni sawa labda kwa sababu za ukosefu wa viwanja, haki za matangazo n.k Sasa kwa joto na jua Kali hasa kwa kipindi hiki ni haki timu hzo kucheza saa 8 mchana?

Mbona Simba na Yanga hawachezi saa 8mchana?

Timu zinazocheza saa 8 mchana Zinatendewa haki afya za wachezaji na kimatokeo?

Bodi ya ligi ili HALIKO SAWA HATA KIDOGO.

Naomba kuwasilisha
 
Hili Nimekuwa Nikiliwaza Siku Nyingi Ila Nikawa Najipa Matumaini Kwamba Siku Moja Huenda Ma wao Wakacheza Muda Huo....Ila Bora Umesema Mkuu, Hii Ligi Siyo Ya Simba Na yanga Pekee.
 
Mleta mada ongela. Hili ninjambo muhimu kuzingatiwa wahusika kwenye hizo team sijui hawaoni?? Tatizo akili zao ziko kisimba na kiyanga. Mwili uki Singida Unite lakini Akili na nafsi iko Yanga!
 
Wewe mtoa mada mbona hoja yako dhaifu sana?

Pale London sasa hivi ni saa saba na dakika kadhaa mchana, na ifikapo saa saba na nusu mchana Bunley anakipiga na Chelsea!
 
Wewe mtoa mada mbona hoja yako dhaifu sana?
Pale london sasa hivi ni saa saba na dakika kadhaa mchana, na ifikapo saa saba na nusu mchana bunley anakipiga na chelsea!
Umemuelewa hoja yake lakini? Hajakataa timu kucheza mechi saa nane ya mchana bali inahitajika haki sawa kwamaana hata simba na Yanga na wao mechi zao zichezwe saa nane hivyo hivyo na sio kupendelewa kwa kucheza saa kumi na saa moja mechi zao zote.

Huko london wako fair haijalishi timu kubwa wala ndogo na ndio maana umeona chelsea anakipiga mchana mchana.
 
Wewe mtoa mada mbona hoja yako dhaifu sana?
Pale london sasa hivi ni saa saba na dakika kadhaa mchana, na ifikapo saa saba na nusu mchana bunley anakipiga na chelsea!
Hujamuelewa mtoa hoja tatizo siyo muda tatizo ni Simba, Yanga na Azam hawa hakuna mechi hata Moja watacheza mchana wajua Kali wasipo cheza jioni basi watacheza Usiku..kwa kule England kila Timu itacheza usiku ikiwemo ule usiku unoitwa "Monday Night" ambapo mechi inaanza saa4 usiku..na wote wacheza Usiku wa saa7..na Wrot wacheza mchana kama Leo Chelsea wanavyocheza...so kwa England kuna usawa bila kuangalia Jina wala Hadhi ya Team kitu ambacho nitofauti na hapa Kwetu
 
labda tujiulize ni viwanja vingapi vina miundo mbinu ya mpira kuchezeshwa usiku sanasana nia Uwanja wa Taifa na Azam
....Hii siyo 7bu kimsingi Bodi ya Ligi haiko Fair.. Achia mbali hilo la muda nijuzi tu hapa walisimamisha Mechi za Simba na Yanga eti kuwapa muda wakujiandaa na Derby!hili jambo waliona liko sawa kweli? Leo ni El Clasico lakin umesikia wapi mechi zao za nyuma Barca na Madrid zili simamishwa kuwapa time yakujiandaa???
 
Hoja yangu sio dhaifu kiongozi. Kwa mfano jkt Tanzania amecheza game zaid ya 2 saa 8 mchana na ukiangalia Hali ya hewa Juan na joto la saa 8 mchana Tanzania sio Sawa na joto na jua la UK saa 8 mchana
Wewe mtoa mada mbona hoja yako dhaifu sana?
Pale london sasa hivi ni saa saba na dakika kadhaa mchana, na ifikapo saa saba na nusu mchana bunley anakipiga na chelsea!
 
Kila siku Yanga,Simba na Azam wanacheza 1 usiku wakiwa Dar kwanini HAWACHEZI SAA 8 MCHANA?? AU KUWA TEAM NYINGINE MBALI NA HIZO 3 NI ADHABU?? BODI YA LIGI KUWENI FAIR
 
Lipuli mechi zake zote kasoro moja tu ilizocheza nyumbani amecheza saa nane....unajiuliza hii timu inategemea mapato ya mlangoni ili ipate chochote ijiendeshe lakini kwa kucheza saa nane shabiki gani atakuja tena siku yenyewe ya kazi? Kwanini mpira una ubabaishaji hivyo?
 
....Hii siyo 7bu kimsingi Bodi ya Ligi haiko Fair.. Achia mbali hilo la muda nijuzi tu hapa walisimamisha Mechi za Simba na Yanga eti kuwapa muda wakujiandaa na Derby!hili jambo waliona liko sawa kweli? Leo ni El Clasico lakin umesikia wapi mechi zao za nyuma Barca na Madrid zili simamishwa kuwapa time yakujiandaa???
weka rekodi vizuri..mikia ndio waliandika barua TFF wapate muda wa vikongwe vyao vikandwe maji ya moto baada ya uchovu wa Ntwara,Mwanza na Shinyanga..Yanga waliwashangaa TFF
 
Back
Top Bottom