Kwa ili hatutendei jukwaa la elimu haki

ruhi

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
3,733
5,399
Kumekua na mada mbalimbali hapa juu ya ubora wa vyuo na ubora wa output vyao bila ya kuwepo na mjadala wa chanzo na suluhisho ya nini kifanyike.Napenda kuwasii sana wanajf tuachane na mada kama izi umu,kwani tunashindwa kujibu swali la kwa nini nchi ya KENYA inatoa wasomi wengi na wenye uwezo mkubwa kuliko TANZANIA,licha ya wao kutumia mfumo wa 1-8-4-4/5(awali-primary-sekondari-chuo kikuu) na sisi TZ tunatumia mfumo wa 1-7-4-2-3/4/5(awali-primary-ordinarisekondari-advancedsekondari-chuo kikuu),tunajikita na kusema chuo kukuu cha udsm ni bora kuliko vingine bila kutaja vigezo tunaozotumia ,je tunatumia vigezo vya mwaka wa kuanzishwa?,waadhiri waliopo?,miundombinu(majengo,barabara ndani ya chuo,vifaa vya kufundishia)?,wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na chuo?,chuo ni cha serikali?,kuwajibika kwa waadhiri pamoja na wanafunzi? au tunaangalia wahitimu wa chuo bila kuangalia mwaka wa kuhitimu kwao?,je tunaangalia mchango wa chuo kwa jamii kwa ujumla?.Nadhain tukijadili kwa kuangalia mambo hapo juu twaweza kujua nini cha kufanya kama sisi vijana tunaotaka kuleta mageuzi hapa nchini.kwa kudokeza tu miaka ya nyuma uko miaka ya 70 udsm wanafunzi walishawai kuandamana kupinga kitendo cha bendera kupepea nusumlingoti uko MSUMBIJI kisa URENO kama koloni lao limefiwa na kiongozi wao ungali MSUMBIJI ikiwa nchi huru,je kwa sasa wanaandamana kwa kudai vitu gani? mkopo au? au kutetea wananchi?
Wakati nchi ya KENYA na UGANDA wanaeshimu vyuo vyote na kuhimiza wanafunzi kusoma kwa bidii sisi tunabaguana kivyuo bila kuangalia elimu tunaopata,je kwa nini kenya ilitoa vyuo viwili kwa mwezi wa saba kwenye ubora wa vyuo vikuu afrika na sisi tukatoa moja.
Watu hawaangalii madhara ya kudharau vyuo vingine kwani wanafunzi wanaopewa sifa ya kusoma vyuo bora kuna madhara ya wao kufanya vibaya kwa kutosoma kwa bidii sana,na wale wa vyuo visivyo na ubora nao wakakata tamaa ya kusoma na mwisho taifa likapata msiba,nawaomba sana wanafunzi mnaoenda kuanza mwaka wa kwanza 2012/2013 msipende sana kujazwa sifa zisizo na maana,kwani mnajuana toka primary,secondary,high level.
Hamjiulizi ni kwa nini wanaojisajili kusoma Phd UDSM hawamalizi vizuri na hawana uhakika wa kumalizia thesis zao,na wanaograduate masters upande wa sayansi wanazidi kupungua tu,UDSM nao bado kuna parttime lectures,bora UDOM ijengwe bila siasa inaweza kuokoa elimu ya TZ.
NAOMBA KUWASILISHA
 
Heading yako yenyewe haionyeshi kama kweli we ni msomi! Afu na wewe ni walewale wahanga wa kuiponda Udsm NB: Mods unganisheni hii thread na zile zingine za kipuuzi..zinazolinganisha vyuo!
 
ni wazo zuri!!!! kweli huu mchezo wa kupendelea vyuo mwisho wake sio mzuri!!! tuungane tukomboe jahaz la elimu tz...wakenya haoooo...sisi bado tunapondana na kupeana sifa za kijinga kwa kuenda vyuo flan flan!!!
 
Tatizo humu kuna watoto wengi ambao hawajaingia chuo wanajadili yale wanayoyasikia mtaani ndo wanayaleta hapa na kuyashupalia. Ukitaka kubishana nao utaumiza kichwa chako tu. Wengi wao ni wale wa kusikia tu kwamba mabibo wanafanya starehe nk, kwa hiyo akipata rum mabibo anaanza kutangaza kuhama badala ya kwenda kuishi ili kuchalenge ideology iliyopo kichwani mwake na kuthibitisha hypothesis iliyopo. Wengi wao wanajua ukisoma chuo fulani basi unapata kazi kirahisi na kusahau kwamba kumaliza chuo ni hatua moja na kupata kazi ni hatua nyingine. Wana mawazo ya kwamba wadada wa chuo ni wahuni kutokana na kusikia au kuwaona wamebadilika wanavyorudi likizo baada ya kuona hawavai tena magauni ya vitenge na kuvaa blauz na skirt/suruali. Wana mawazo kwamba ukifika chuo ni kufaulu na kula bata muda wote na wakisikia mtu amedisco wanasema alifika mjini na kuanza uhuni kumbe kuna wanaosoma zaidi ndo wanapata suplementary pia. Ni kazi ngumu sana kuargue na hawa first year watarajiwa ambao wanatakiwa wakaishi maisha ya chuo kwanza na kujifunza maisha yanavyokwenda. Sina shida na ubora au ubovu wa chuo kwani nchi yetu na serikali ya chama cha mabwepande wanavyoendesha mfumo mzima wa elimu. Ndio maana hushangai kuona medical school bila teaching hospital, watu wanasoma chuo miaka mitatu bila kwenda field, ni hovyo hovyo tu. Lakinh na vyuo vikongwe sasa hivi siasa zimezidi ndo maana hata wanachuo wanaotoka kwenye vyuo hivyo wamekaa kisiasa siasa tu. Malecturer wanafanya utafiti ambao ni kiwango cha kufanywa na wanafunzi, no trial experiments, yaani elimu yetu inatia huruma. Ni elimu ya kujengeana uoga tu ili uonekane hujui ndo maana hata confidence kwa kile unachokijua unakuwa huna! Ni huruma tupu.
 
tatizo humu kuna watoto wengi ambao hawajaingia chuo wanajadili yale wanayoyasikia mtaani ndo wanayaleta hapa na kuyashupalia. Ukitaka kubishana nao utaumiza kichwa chako tu. Wengi wao ni wale wa kusikia tu kwamba mabibo wanafanya starehe nk, kwa hiyo akipata rum mabibo anaanza kutangaza kuhama badala ya kwenda kuishi ili kuchalenge ideology iliyopo kichwani mwake na kuthibitisha hypothesis iliyopo. Wengi wao wanajua ukisoma chuo fulani basi unapata kazi kirahisi na kusahau kwamba kumaliza chuo ni hatua moja na kupata kazi ni hatua nyingine. Wana mawazo ya kwamba wadada wa chuo ni wahuni kutokana na kusikia au kuwaona wamebadilika wanavyorudi likizo baada ya kuona hawavai tena magauni ya vitenge na kuvaa blauz na skirt/suruali. Wana mawazo kwamba ukifika chuo ni kufaulu na kula bata muda wote na wakisikia mtu amedisco wanasema alifika mjini na kuanza uhuni kumbe kuna wanaosoma zaidi ndo wanapata suplementary pia. Ni kazi ngumu sana kuargue na hawa first year watarajiwa ambao wanatakiwa wakaishi maisha ya chuo kwanza na kujifunza maisha yanavyokwenda. Sina shida na ubora au ubovu wa chuo kwani nchi yetu na serikali ya chama cha mabwepande wanavyoendesha mfumo mzima wa elimu. Ndio maana hushangai kuona medical school bila teaching hospital, watu wanasoma chuo miaka mitatu bila kwenda field, ni hovyo hovyo tu. Lakinh na vyuo vikongwe sasa hivi siasa zimezidi ndo maana hata wanachuo wanaotoka kwenye vyuo hivyo wamekaa kisiasa siasa tu. Malecturer wanafanya utafiti ambao ni kiwango cha kufanywa na wanafunzi, no trial experiments, yaani elimu yetu inatia huruma. Ni elimu ya kujengeana uoga tu ili uonekane hujui ndo maana hata confidence kwa kile unachokijua unakuwa huna! Ni huruma tupu.

mkuu umenena na tunatakiwa kubadilika sana,tunatakiwa kubadilika sana
 
punguza magazeti...ulitakiwa ueleze short and clear..ungeeleweka tu..!! ila unachokinena ni cha kweli!
 
mkuu umenena na tunatakiwa kubadilika sana,tunatakiwa kubadilika sana

mkuu sasa hivi watu wamebakia kujisifu tu kuwa mi nimesoma chuo fulani! Ni wavivu, non creative yaani ni balaa tupu. Mtu anamaliza chuo hata haki zake na wajibu wake hajui, sasa unajiuliza: huyu chuoni alienda kuelimika au kukariri masomo. Tunakoelekea tunahitaji watu ambao wameelimika sio watu waliokariri masomo. Unakutana na mtu anasoma pspa, sociology nk hata katiba hajawai kuiona!! Ukiingia mtaani unatakiwa ujue haki za msingi za kwako na jamii inayokuzunguka.
 
Mkuu mi naona ufate yako yanayokuhusu achana na ya wa2,ndio nilisomea chuo chenye cfa ila nikapata lower clas je!utaajiriwa ww aachwe yule wa upa clas wa chuo kisichocfika?bwana acha wajicfu ila chuo co cfa ni akili yako
 
mkuu mi naona ufate yako yanayokuhusu achana na ya wa2,ndio nilisomea chuo chenye cfa ila nikapata lower clas je!utaajiriwa ww aachwe yule wa upa clas wa chuo kisichocfika?bwana acha wajicfu ila chuo co cfa ni akili yako

kinachozidi kushusha elimu yetu kwa kasi ni suala la wanafunzi kutomaliza field zao na kutokomea pale ambapo walimu wanamaliza kuwatembelea/kuases,je ni kwa nini mwalimu anamwita mwanafunzi pembeni tofauti na pale anakofanyia field? Ili kuongea nae?,tukizingatia kua hakuna mazoezi kwa vitndo za kutosha tuwapo chuoni.
 
Back
Top Bottom